Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UHALALI WA KUTAWASALI KWA WAFU 1

0 Voti 00.0 / 5

UHALALI WA KUTAWASAL

Sehemu ya Kwanza

UFAFANUZI KUHUSU KUFAA KUTAWASAL KWA MAWALII WALIOKUFA

AsKwa majina naitwa SAIDI karimu Omari nipo Morogoro ,

Na vp kuhus Tawassul : Ufafanuzi kuhus kufaa kutawassal kwa mawalii ingali wakiw si hai

            MAJIBU

Ndiyo inafaa, inajuzu kwa mujibu wa Qur-ani Tukufu na Matukio haya yaliyofanywa na Maswahaba wa Mtukufu Mtume saww

Wala usidhani wale walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu, bali wako hai wanaruzukiwa kwa Mola wao. 3:169

ولا تحسبن الذين قتلوا في سبيل الله أموتا بل احياء عند ربهم يرزقون ١٦٩ .

Wakifurahia kile walichokipewa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, na wanawafurahikia (wakionyesha furaha zao hizo kwa) walio nyuma yao ambao hawajawafuata (ambao hawajafa), kwamba Hapana khofu juu yao wala wao hawatahuzunika.3:170

فرحين بما آتاهم الله من فضله ويستبشرون بالذين لم يلحقوا بهم من خلفهم لا خوف عليهم ولا هم يحزنون .

Tuwaulize wakufunzi wetu (wanazuoni wakubwa maarufu waliotangulia)

Mwanachuoni maarufu wa Ahlisuna ambaye alikuwa Mufti wa Makkah, Sayyid Ahmed bin Dahlan ameeleza katika kitabu chake "Taqriibul Usuul Litas'hilil Usuul:

 

Kuwa: "Wajuzi wengi wameeleza kuwa Walii baada ya kifo chake roho yake hutungikwa kwa wafuasi wake, na huwafikia (walio hai) baraka zake na neema."

Mwanachuoni aliyeyasema maneno hayo ni Sayyid Abdullah bin Alawi Al Hadadi. Yeye aliongeza kusema kuwa: "Walii anakuwa ni mwenye kuwaneemesha zaidi walio karibu na walio na mapenzi naye baada ya kifo chake kuliko alivyokuwa akiwaneemesha wakati wa uhai wake.

Sababu ni kuwa katika uhai wao ni wenye kutenda mambo kwa taklifu, lakini baada ya kifo ni wenye kufanya jambo mahususi,"

Kutbu Al Hadid ameendelea kusema kuwa:  Hakika Mawalii wanapokufa hakuna kinachopotea kwao isipokuwa viwiliwili vyao na kutoonekana. Lakini dhati zao zinadumu nao ni hai katika makaburi yao.

Na ikisha kuwa Walii ni hai kaburini mwake, basi hakipotei chochote katika elimu, akili na nguvu zake za kiroho isipokuwa huzidi zaidi akawa ni mwenye kuwa na elimu zaidi kwa kuelekea kwa Mwenyezi Mungu. Roho za Mawalii zinapoekekea kwa Mwenyezi Mungu kwa jambo lolote Mwenyezi Mungu hulikubali."

Sayyid Abil Mawahibi Shadhily kuwa: "Nilimsikia Sheikh wetu Abu Uthamani Al Magharibiy akisema: "Mtu anapozuru kaburi la Walii, Walii huyo humtambua. Na anapoktolea salamu naye humrejeshea. Na Mtu aliyemzuru Walii akimtaja Mwenyezi Mungu katika kaburi lake naye huyo Walii humtaja Mwenyezi Mungu pamoja naye,hususan Dhikir yenyewe ikiwa ni "LAILAHA ILLALLAHU MUHAMMAD RASULULLAH". Hakika Walii huyo husimama na akakaa pamoja naye.

Kisha Sheikh akaendelea kusema hali akionya kuwa, "Wajiepushe wajuzi kutoa maelezo wasiyoyajua." Lililo hakika ni kuwa Mawalii wako hai katika makaburi yao isipokuwa wamehama kutoka nyumba moja hadi nyingine.

Heshima wanayotakiwa kuwekewa wakati wamekufa ni sawa sawa na ile ya wakati wa uhai wao. Na kadhalika wafanyiwe adabu inayolingana na ile waliyokuwa wakifanyiwa wakiwa hai.

Nao Mawalii wanapofariki huombewa na roho za Mawalii wengine wote ikiwa ni pamoja na Mitume as.

Rejea: Ashawahidul haq UK 149-150, cha Sheikh Yusuf'Ismail Nabahani ambacho kimekusanywa pamoja na Kitabu "Ulamaul Muslimina wal wahhabiyyin cha Sheikh Abdul Wahhab Sha'aran.

Hadithi nyingine ambayo inaonyesha kuwa Mtukufu Mtume saww ana uwezo wa kuwaombea Waumini hata baada ya kifo chake, ni ile hadithi ya Ut biyu aliponukuliwa akisema;

Nilikuwa nimekaa katika kaburi la Mtukufu Mtume saww akaja Bedui ( mkaa jangwani) akasema; "Amani iwe kwako Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu.'  Nimesikia Mwenyezi Mungu amesema "Na lau wanapojidhulumu nafsi zao wangekujia wewe (Muhammad), na wakamtaka msamaha Mwenyezi Mungu naye Mtume akawatakia msamaha, bila shaka Mwenyezi Mungu angekuwa ni mwenye kupokea Msamaha, mwenye kuwarehemu". 4:64

ولو أنهم إذ ظلموا أنفسهم جآءوك فاستغفروا الله واستغفر لهم الرسول لوجدوا الله توابا رحيماً.

(Bedui akaendelea,  kusema). Nami kwa hakika nimekujia wewe (Mtume Muhammad) hali ni mwenye kutaka msamaha kwa makosa yangu, na mwenye kukutaka uniombee kwa Mwenyezi Mungu."

Kisha akatoa beti hizi;

   Ewe mbora wa waliozikwa katika bonde, likawa bora bonde hilo katika mabonde na vilima. Nafsi yangu ni fidia katika kaburi ambalo wewe ni mkazi wake, (Kwani) ndani yake mna nafuu na utukufu na heshima.

Ut biyu anasema: Kisha Bedui akaondoka na nikapatwa na usingizi nikamuona Mtukufu Mtume saww katika usingizi akaniambia, "Mfuate Bedui na umpe habari njema kuwa Mwenyezi Mungu amemsamehe.

Rejea:  Al Adhkar mlango wa sita UK 498: Tafsir Ibn Kathir ya Al Hafidh Ibn Kathir Jz 1 UK 410: Al Mughny ya Sheikh Muhammad bin Qudama Jz 3 UK 556:; Asharhul Kabir cha Sheikh Abi Farji bin Qudama Jz 3 UK 495.:; Al Kashful Qanuu cha Sheikh Mansur bin Yunus Jz 5 UK 30.

Hadith nyingine imepokewa na Amirul Muuminina Imamu Ally bin Abi Twalib as ya kwamba: Alikuja Bedui baada ya kuwa tumemzika Mtume saww kwa siku tatu. Akajitupa kwenye kaburi la Mtukufu Mtume saww na kujitia michanga ya kaburini kichwani, akasema;

Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ulikuwa ukitueleza nasi tukasikia usemi wako na ulitekeleza kutoka kwa Mwenyezi Mungu, nasi tukatekeleza kutoka kwako. Na ilikuwepo Aya katika yale aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu kuwa:-

Na lau wao wanapojidhulumu nafsi zao wangekufikia na wakamtaka msamaha Mwenyezi Mungu na wakatakiwa msamaha pia na Mtume; bila shaka wangemkuta Mwenyezi Mungu ni mwenye kupokea Msamaha na mwenye kuwarehemu.4:64.

ولو أنهم إذ ظلموا أنفسهم جآءوك فاستغفروا الله واستغفر لهم الرسول لوجدوا الله توابا رحيماً.

Mimi nimedhulumu nafsi yangu na nimekuijia unitakie Maghfira.' Ikanadiwa kutoka kaburini kwamba umesamehewa."

Rejea: Tafsiri Al Qurtubi Jz 5 UK 265

Fuatana nami Sehemu inayofuata tujifunze zaidi.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini