Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

HISTORIYA YA IMAMU HUSSEIN (A.S) 8

0 Voti 00.0 / 5

IMAMU HUSSEIN (A.S)

Sehemu ya nane

JIHADI YA IMAMU HUSSEIN BIN ALIY (A.S). 5

JIBU LA IMAMU HUSSEIN (A.S)

Zilizopokusanyika kwa Hussein (a.s) barua zilizojaa kapu mbili, aliandika barua moja kwao akampa Hani bin Hani as Sabaniy na Said bin Abdullah Al Hanafiy, na humo mlikuwa na:  Nimeshafaham mliyoyasema katika barua zenu miongoni mwa mapenzi ya kuja kwangu kwenu, na mimi namtuma kwenu ndugu yangu na mtoto wa ami yangu na mwaminifu wangu katika AhIul Bait wangu Muslim bin Aqiil ili anifahamishe ukweli wa jambo lenu, na aniandikie yale yatakayobainika kwake katika mkusanyiko wenu ikiwa jambo lenu ni kama zilivyonijia barua zenu na walivyonieleza wajumbe wenu nitakuja haraka kwenu.

Kisha akamtuma Muslim bin Aqiil pamoja na Qays bin Musahari as Saidawiy, Ammarah bin Abdillahi as Saluliy, na Abdurrahmaan bin Abdullah Al Asadiy, na akawaamuru kumcha Mwenyezi Mungu na kutazama yale waliyokusanyika kwayo watu wa Kufah, ikiwa ataona watu waliyokusanyika ni waaminifu amwandikie barua haraka.

Muslim bin Aqiil (a.s) alitoka Makkah katika nusu ya mwezi wa Ramadhan kupitia njia ya Madina, na baada ya kupita siku tano za mwezi wa Shawwali aliingia Kufah, akafikia katika nyumba ya al Mukhtaar bin Abi Ubaidah at Thaqafiy. Wafuasi wake wakaja kumpa kiapo cha utii, idadi yao ikafikia 18,000 kumi na nane elfu, na inasemekana ilifikia 25,000 ishirini na tano elfu, na katika hadithi ya as Sha'aby walifika 40,000 Arubaini elfu.

Muslim bin Aqiil (a.s) akampa habari ya kukusanyika watu wa Kufah katika utii wake na kumgonjea kwao kuwasili kwake na humo anasema :. Kiongozi hawadanganyi watu wake, na wameshanipa kiapo cha utii miongoni mwao watu wa Kufah kumi na nane elfu, njoo haraka ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika katika mji wa Kufah una panga mia moja elfu hivyo usichelewe.

Kundi miongoni mwa wenye tamaa katika Bani Umayyah liliharibu Mkusanyiko huu, kati yao ni Umar bin Saad bin Abi Waqqas, Abdallah bin Muslim bin Rabi'i al Hadharamiy, Ammarah bin Uqba bin Abi Muit, ambao walimwandikia barua Yazeed wakamweleza kuwasili kwa Muslim bin Aqiil (a.s) na kitendo cha watu wa Kufah kumkubali, na kwamba Nu'man bin Bashir hana uwezo wa mapambano,.

Ndipo Yazeed l.a alimwambia Ubaid bin Ziyad l.a Gavana wake wa Basra akimhimiza kwenda Kufah ili amtafute Ibn Aqiil amfunge na amuuwe au amfukuze. Ibn Ziyad akafanya haraka kuelekea Kufah pamoja na Muslim bin Amru al Bahiliy, Al Mundhir bin al Jarudi, Shariku al Harithiy, na Abdallah bin al Harithi bin Nawfal, wakiwa ni Viongozi wa askari mia tano.

Kwa kuhofia kuchelewa Ibn Ziyad hakuwa anawajali wala kuwatizama wale waliokuwa wakiondoka njiani miongoni mwa askari zake, kiasi kwamba Shariku bin al A'war na Abdallah bin Harithi waliondoka njiani, lakini hakuwajali kwa kuhofia kwamba asichelewe kwa ajili yao, na akihofia kwamba Hussein (a.s) asije kuwasili Kufah kabla yao.

Alipofika al Qadasiya alianguka aliyekuwa Mtumwa wake wa Maharan, Ibn Ziyad l.a akamwambia kama utaweza kujizuia na hali hii ukafika Kasri, basi utapata laki moja, Mtumwa akasema, hapana, Wallahi siwezi.

Ubaid akamuacha na kuendelea na safari. Akavaa nguo ya Yemen na kilemba cheusi na akawa anatembea peke yake, na kila alipopita kundi la watu walidhani kuwa ni Hussein (a.s), na hivyo walikuwa wakimwambia: Karibu ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. "Naye alikaa kimya hadi akaingia sehemu ya Kufah inayopakana na Najaf.

Watu wakampokea kwa sauti moja :. Karibu ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu." Hali hii ikamuudhi, na mwisho akaingia ndani ya Kasri la utawala, Nu'man hakumfungulia mlango wa Kasri, akamchungulia akiwa juu ya Kasri akasema :. Mimi sitakupa amana yangu ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ibn Ziyad l.a akamwambia fungua usiku wako umekuwa mrefu, ndipo mwanaume mmoja akamsikia na akamjua, akawaambia watu hakika ni Ibn Ziyad na akaapa kwa Mola wa Alkaaba.

Wakatawanyika kwenda majumbani, asubuhi Ibn Ziyad alikusanya watu katika msikiti mkuu akawahutubia na akatahadharisha, akawatamanisha mali (hongo na rushwa) na akasema: Yeyote akikutwa mgeni miongoni mwa wale wanaomchukia Amirul Muuminina (Yazeed l.a) na wala hakumleta kwetu, atasulubiwa juu ya mlango wa nyumba yake. Ndipo Muslim bin Aqiil akaogopa kukamatwa kwa hila bila kujua, hivyo akafanya haraka kutoroka kabla ya ahadi iliyo baina yake na watu, akamwamuru Abdallah bin Hazim awaite wafuasi wake na alikuwa kawaandaa katika nyumba za karibu yake. Wakakusanyika kwake watu elfu nne wakitamka tamko la siku ya Badr "" "Yaa Mansuur ummat.

Kisha akampanga Ubaidullah bin Amru kiongozi wa Kindiy katika kikosi cha Kindiy na Rabi'ah, akamwambia tangulia mbele yangu kwa Farasi. Na akampa Muslim bin Ausajah al Asadiy katika kikosi cha Mudhihaji na Asad, akamwambia ongoza waendao kwa miguu. Na akampa Abu Thamamat as Swaidiy katika kikosi cha Tamiym na Hamdani, na akampa Abbas bin Ja'ddah al Jadliy katika kikosi cha Madina.

Na wakaelekea kwenye Kasri la Ibn Ziyad, lakini Ibn Ziyad akajificha humo akafunga milango na hakuweza kupambana kwa sababu hawakuwa pamoja naye isipokuwa wanaume thalathini miongoni mwa askari na wanaume ishirini miongoni mwa waungwana na watumwa.

Lakini unafiki wa Kufah na kile walichonacho miongoni mwa hiyana hawakuiacha "bendera ipepee," hawakubaki katika watu elfu nne isipokuwa watu mia tatu. Na walipaza sauti waliokuwepo katika Kasri :. Enyi watu wa Kufah mcheni Mwenyezi Mungu na wala msizipeleke nafsi zenu kwenye Farasi wa Sham, kwani tumeshawaonja na kuwajua. Hawa watu mia tatu wakasambaa hadi ikawa mtu anamwendea mwanae, ndugu yake, mtoto wa ami yake na kumwambia ondoka, na mwanamke anamwendea mume wake Anamng'ang'ania anarejea.

Muslim bin Aqiil aliswali swala ya Ishaa pamoja na watu thalathini kisha akaondoka kuelekea upande wa Kindah (milimani) pamoja na watu watatu, hakutembea isipokuwa kidogo, ikawa hamuoni anayemuongoza njia, akateremka juu ya Farasi wake akatembea kwa kutaabika katika vichochoro vya Kufah, hajui ataelekea wapi.

Watu waliposambaa kwa Muslim bin Aqiil (a.s) na fujo zao zikatulia na Ibn Ziyad akawa hasikii sauti za wanaume, aliwaamuru waliokuwa pamoja naye katika Kasri wachungulie katika kivuli cha msikiti ili watazame je, wamejificha humo? Basi walikuwa wananing'iniza vibatari na kuviwasha moto katika milingoti na wanavining'iniza kwa kamba hadi katika uwanja wa msikiti, lakini hawakumuona mtu, ndipo wakamjulisha Ibn Ziyad, naye akaamuru mwitaji awaite watu wakusanyike msikitini na walipokuja msikitini alipanda juu ya mimbari na kusema :. Hakika Ibn Aqiil ameleta ambayo mmeshayajua miongoni mwa ikhitilafu na mparaganyiko, basi nimeshaondoa kinga kwa mwanaume ambaye tutamkuta Ibn Aqiil katika nyumba yake. Na atakaye mleta atakuwa ameshikamana na dini yake, basi mwogopeni Mwenyezi Mungu waja wa Mwenyezi Mungu, na jilazimisheni na utii wenu na Njia zenu na wala msizijaalie nafsi zenu njia nyingine. Kisha akamwamuru mkuu wa askari wake al Hasiyn bin Tamiym kutafuta katika nyumba na vichochoro, na akamtahadharisha kuwa atamuua ikiwa Muslim bin Aqiil atatoroka na kutoka Kufah.

Fuatana nami sehemu ya tisa ya historia ya Maasum Hussein bin Aliy (a.s).

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini