Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

HISTORIYA YA IMAMU HUSSEIN (A.S) 18

0 Voti 00.0 / 5

IMAMU HUSSEIN A S

Sehemu ya thelathini na mbili

JIHADI YA IMAMU HUSSEIN AS 29.

SIKU YA ASHURA

BWANA WA MASHAHIDI 3

FARASI WA IMAMU HUSSEIN (A.S)

Farasi akawa anazunguaka pembezoni mwa Hussein (a.s) akawa amapaka kichwa chake kwa damu ya Hussein (a.s), Ibn Saad I.a akapiga kelele :. Jihadharini na Farasi kwani ni katika Farasi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu saww. Farasi akazunguka akawa anapiga mateka kwa miguu yake hadi akauwa watu Arubaini na Farasi wenzie kumi. Ibn Saad I.a akasema :. Mwacheni tuone atafanya nini, alipofanya aliyoyataka akaelekea kwa Hussein (a.s) akawa anapaka uso wake kwa damu ya Hussein (a.s), anamnusa na anapiga kelele kwa sauti ya juu.

Abu Ja'far Muhammad Baqir (a.s) amesema :. Alikuwa anasema :. Ni Dhulma katika umma uliouwa mtoto wa Nabii wake. Akaelekea upande wa Mahema kwa sauti hiyo, wanawake walipoona Farasi amehuzunika wakatoka bila ya mitandio, nywele wazi, wakijipiga mashavu na kwa vilio wakisema: Baada ya huzuni ni udhalili, twendeni haraka kwenye maiti ya Hussein (a.s). Ummu Kuluthumu akaita: Eee Muhammad! Ewe baba yangu,! Ewe Ally! Ewe Ja'far! Ewe Hamza! Hussein huyu hapa Jangwani amekufa Karbalaa.

Zainabu akaita: Eee ndugu yangu! Ewe bwana wangu! Ewe Ahlul Bayt! Natamani mbingu ingeanguka juu ya ardhi, Laiti milima ingeporomoka juu ya ardhi. Hadi akafika kwa Hussein (a.s), na tayari Umar bin Saad l.a alikuwa ameshakaribia kwake akiwa na kikundi cha wafuasi wake huku Hussein (a.s) akiwa anagaragara, Zainabu akapiga kelele :. Ewe Umar! Anauliwa Abu Abdillahi na wewe unamtazama? Akageuza uso kwake huku machozi yake yakitiririka kwenye ndevu zake,,, Zainabu akasema Ole wenu, hakuna miongoni mwenu Mwislamu? Hakumjibu yeyote.

Umar bin Saad l.a akawapigia watu kelele :. Teremkeni na mpumzisheni. Shimir Bin Dhilijawshen I.a akajitokeza akamkanyaga kwa miguu yake na akakaa kifuani mwa Hussein (a.s). Mara Sukaina mtoto wa Hussein (a.s) aliyekuwa na miaka minne wakati huo alijipenyeza kwenye miguu ya Farasi na ngamia hadi akamfikia baba yake, alipo mkuta Shimir Bin Dhilijawshen I.a yuko kifuani mwa baba yake, alianza kumlilia baba yake, Shimir Bin Dhilijawshen I.a akashuka juu ya kifua cha Hussein (a.s) akamtandika kibao Sukaina na akamshika akamrusha mbali, akarudi kifuani mwa Hussein (a.s) akabusu ndevu zake tukufu na akampiga na panga lililobutu mapigo kumi na mbili ndipo kichwa kitukufu cha Imamu Hussein (a.s) kikakatika..

Innalillahi wainna ilayhi rajiuun.

ألا لعنة الله على الظالمين وسيعلم الذين ظلموا أي منقلب ينقلبون.

  WAMPORA IMAMU HUSSEIN (A.S) NGUO

watu wakaja, Umar bin Saad akachukua nguo ya Hussein (a.s), Is'haqa bin Hawaiya akachukua shati, al Khanas bin Murthad bin Alqam al Hadharamiy akachukua kilemba, Al As'wadi bin Khalid akachukua kanda mbili, Jami'i bin al Khaliq al Awadiy akachukua upanga, na inasemekana aliyeuchukua ni mwanaume kutoka Bani Tamiym jina lake ni al As'wadi bin Handhalah.

Ndipo alipokuja Bajandal, alipoona Pete katika kidole cha Hussein (a.s) na kina damu akakata kidole cha Hussein (a.s) na akachukua Pete. Qays bin al Ash'ath akachukua tandiko alilokuwa anakaa juu yake, ndiyo maana Qays Anaitwa tandiko. Ama Ja'unah bin Hawiya al Hadharamiy yeye alichukua nguo chakavu ya Hussein (a.s), Rahil bin Khathiymah al Ja'afiy, Haniy bin Shabibi al Hadharamiy, na Jarir bin Mas'uud al Hadharamiy walichukua upinde pamoja na mishale.

Mwanaume miongoni mwao akachukua mkanda wa Suruali na ulikuwa na thamani na hiyo ni baada ya watu kumpora, alisema :. Nilitaka kumvua mkanda, akaweka mkono wa kulia juu yake, sikuweza kuunyanyua. Nikakata mkono wake wa kulia, akaweka mkono wake wa kushoto juu yake, sikuweza kuunyanyua, nao nikaukata. Nikataka kuvua Suruali nikasikia sauti ya tetemeko nikaogopa nikamuacha mimi nikazimia, na katika hali hii nilimuona Nabii Muhammad saww, Amirul Muuminina Aliy bin Abi Talib as, Fatimah na Hassan (a.s) na Fatimah alisema :.

Ewe mtoto wangu wamekuuwa, Mwenyezi Mungu awalaani. Akamwambia :. Ewe mama yangu amenikata mikono huyu aliye lala, ndipo akaniombea dua mbaya akasema :. Mwenyezi Mungu akate mikono yako na miguu yako, apofushe macho yako, na akuingize motoni. Macho yangu yalipofuka, mikono yangu na miguu yangu imeshakatika, na haikubakia katika dua ya bi Fatumah (a.s) isipokuwa ni kuingia Motoni tu.

Kisha wakakata vichwa vya Mashahidi wote na kuvitungika juu ya mikuki. Na miili wakaikanyaga kanyaga kwa wanyama wao.

Wakayageukia Mahema ya Ahlul Bait wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakachoma Mahema yote moto wakawanyang'anya wanawake na watoto vipambo vyao na hijabu zao, wakanyofoa masikio yaliyokuwa na hereni bila huruma kana kwamba hawana watoto. Wote wakatekwa kama mateka wa kivita.

Usiku wa kumi na moja walilala hapo Jangwani mchangani chini ya ulinzi mkali pasipo stara yoyote. Baridi la usiku lote liliwaishia.

Asubuhi waliwapelekwa Kufah kwa Ibn Ziyad l.a na baadaye Shamu kwa Yazeed l.a.

Siku tatu baada ya mauaji ya kizazi cha Mtukufu Mtume Muhammad saww, ndipo wenenyeji na majirani wa Karbala wakajitokeza kutaka kuzika miili ya Ahlul Bait wa Mtume wa Mwenyezi Mungu iliyoachwa bila kuzikwa.

Lakini walishindwa kujua huu ni mwili wa nani na ule ni wa nani maana haina vichwa. Mara Akatokea Ally bin Hussein Zainul Abidina (a.s) akasimamia shughuli ya mazishi, akawa anawaambia huyu ni Hussein (a.s) tumzike hapa na huyu ni Abbas tumzike pale na huyu ni Allyyul akbar tumzike pale hadi wakazikwa wote.

Eee laana ya Mwenyezi Mungu iwaendee watu madhalimu.

ألا لعنة الله على الظالمين وسيعلم الذين ظلموا أي منقلب ينقلبون

Innalillahi wainna ilayhi rajiuun. Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Fuatana nami sehemu inayofuata katika historia ya Maasum Hussein bin Aliy (a.s).

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini