Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

HISTORIYA YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W) 1

0 Voti 00.0 / 5

WATU WA KWANZA KUMKUBALI MTUKUFU MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) NA KUTAMKA SHAHADA NI

1- KHADIJA BINT KHUWAILID AS

     Baada ya Bibi Khadija Bint Khuwailid kumtuliza, kumliwaza na kumthibitishia kushinda vikwazo vyote baada ya kipindi kifupi, Jibril as alitokea tena mbele ya Mtukufu Mtume Muhammad saww wakati alikuwa ndani ya pango la Hira, na akawasilisha kwake Wahyi wa pili:

يا أيها المدثر. قم فأنذر. وربك فكبر.

"Ewe uliyejifunika (shuka). Simama na uonye. Na Mola wako mtukuze. 74:1-3

Hii amri ya Mwenyezi Mungu ya "Simama na uonye" ilikuwa ni ishara kwa Muhammad saww (aliyefunikwa na shuka) kuanza kazi yake. Jibril as alimweleza yeye kazi zake mpya ya kwanza kabisa ilikuwa ni kuangamiza ibada ya miungu ya uongo, na kusimamisha beram ya Tawhidi - imani ya Upweke wa Muumba - Ulimwenguni; na alikuwa awaite wanadamu kwenye dini ya haki (kweli) - Uislamu. Uislamu maana yake ni kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumkubali Muhammad kama mja na Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Jioni ile Muhammad saww alirudi nyumbani mwenye fahamu na dhamira juu ya kazi yake mpya kwamba alikuwa anapaswa kuutangaza Uislamu, na kwamba alikuwa aanzie kutoka nyumbani kwake mwenyewe - kwa kuutangaza Uislamu kwa mke wake.

Muhammad saww alimweleza Khadija juu ya kutembelewa kwa mara ya pili na Jibril as, na wajibu uliowekwa juu yake na Mwenyezi Mungu Mtukufu wa kumuita yeye Khadija kwenye Uislamu. Kwa Khadija, historia na ukamilifu wa uadilifu wa mume wake vilikuwa ni uthibitisho usiopingika kwamba alikuwa ni mjumbe wa ki ungu, na aliukubali Uislamu bila kusita.

Kwa kweli, kati yake na Uislamu, kulikuwa na uhusiano wa kiitikadi fulani uliokuwepo kabla. Kwa hiyo, wakati Mtukufu Mtume Muhammad saww alipoleta Uislamu kwake, Khadija aliutambua mara moja, na akaufuata kwa matumaini. Aliamini kwamba Muumba ni mmoja, na kwamba Muhammad saww alikuwa ni Mtume wake, naye akatamka:

أشهد أن لا إله إلا الله؛ وأشهد أن محمدا عبده ورسوله.

Nashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mtumwa na Mtume wake."

Muhammad; huyu Mtume mpya wa Mwenyezi Mungu, alijishindia mfuasi wake wa kwanza Khadija Bint Khuwailid mke wake. Alikuwa ndiye wa kwanza, wa kwanza kabisa kuthibitisha imani yake katika Tawhidi (Upweke wa Muumba), na alikuwa ndiye wa kwanza kabisa kumkubali Muhammad kama Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wanadamu wote. Alikuwa ndiyo Mwislamu mwanamke wa kwanza.

Muhammad aliutambulisha Uislamu kwa Khadija. Alimwelezea maana yake, na akamwiingiza kwenye Uislamu.

Heshima ya kuwa mtu wa kwanza katika Ulimwengu mzima kushuhudia Upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuukubali Utume wa Muhammad, ni ya Khadija kwa wakati wote.

F.E. Peters anasema:

"Yeye (Khadija) alikuwa wa kwanza Kuukubali ukweli wake wa wahyi wake (Muhammad saww), Mwislamu wa kwanza baada ya Mtukufu Mtume saww mwenyewe. Alimtia moyo na kumsaidia Muhammad wakati wa miaka migumu ya mwanzo ya mahubiri yake ya hadhara, na katika miaka ishirini na tano ya ndoa yao hakuoa mke mwingine. Ndoa yao ilikuwa, kwa kiwango chochote cha akili cha kuamua, ni uwiano wa mapenzi na vilevile ubia wa ushirikiano.

Rejea: (Allah s.w.t.)'s Commonwealth, New York. Na vitabu vinginevyo vingi vya historia ya Kiislamu

Fuatana nami Sehemu ya ishirini historia ya Mtukufu Mtume Muhammad saww tujifunze mtu wa pili Kuukubali Uislamu.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini