Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE 6

0 Voti 00.0 / 5

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

Sehemu ya Sita

KUTOKUVAA HIJABU NA MADHAMBI YA UBAKAJI

Miongoni mwa athari mbaya zinazosababishwa na tabia ya wanawake ya kutokuvaa Hijabu ni yale makosa ya jinai ya kuwabaka wanawake na kuwaingilia kwa nguvu bila hiyari yao. Ni jambo lisilofichikana pindi mwanamke anapouacha wazi mwili wake na mapambo yake, hali hiyo huamsha hisia za kijinsia kwa wanaume. Kwa hakika ni juu ya mwanamke mwenyewe kuulinda mwili wake, mapambo yake na utu wake kutokana na hatari hiyo inayoweza kumkabili.

Hapana shaka kwamba, macho ya vijana wasiokuwa na msimamo wa dini, pindi wanpomuangalia mwanamke ni sawa na macho ya mbwa mwitu anapomuangalia kondoo. Pia tunaweza kuyalinganisha macho hayo na macho ya paka anapomuona panya, au tuseme yanafanana na macho ya mnyama mkali wa porini, anapomuona mnyama mwingine au kitu kimngine ambacho kinamfaa kwa chakula. Siyo ajabu kabisa kwa mazingira kama haya kumkuta mwanamke amenasa ndani ya mtego aliojitegea mwenyewe kutokana na tabia ya kujitangaza mbele ya watu waovu.

Tabia hii ya ubakaji mara nyingi inatokea katika sura ya kutisha huko kwenye nchi za magharibi ambazo zimeporomoka mno katika suala zima la maadili. Katika ripoti moja kati ya matoleo ya gazeti la The Gurdian la nchini Uingereza iliandikwa kwamba: "Takwimu za polisi zinaonesha kuwa, makosa ya jinai ya kubaka yanaongezeka mwaka hadi mwaka. Katika mji wa Washington peke yake kila baada ya dakika kumi na tano huwa kuna tukio la kubaka, na katika mji mkuu wa Uingereza (London) yalitokea matukio 2095 ya kubaka wanawake na wasichana mnamo mwaka wa 1970 peke yake[1]." Haya ni machache katika mengi ambayo tungeweza kukuorodheshea.

Na miongoni mwa matukio ya kubaka kutokana na wanawake kutokujali kujisitiri kwa mujibu wa sheria na maumbile yao, mimi nimesikia kwamba, kuna rais fulani anayeongoza nchi moja miongoni mwa nchi za Kiarabu, yeye hufanya ziara za mara kwa mara kuvitembelea vyuo vikuu akitafuta mabinti katika vyuo hivyo na kuwachagua wale wazuri na wanaopendeza. Kisha humtoa nje ya msitari binti anayemuona kuwa atamfaa. Baada ya muda mfupi askari wa usalama wa taifa huwa wanakwenda nyumbani kwa binti huyo na kumweleza baba yake kwamba rais wa jamhuri anamtaka binti yake akakeshe naye katika usiku wa siku hiyo!!

Hali kama hii husababisha msiba mkubwa kwa baba, mama, binti huyu na hata familia nzima huingia ndani ya mtihani huu. Msiba huu huwagubika watu hawa kwa sababu wanafahamu wazi kwamba rais huyu ataishi na binti yao kwa usiku huo mmoja tu!! Sasa je, watu hawa watalikataa ombi la rais? Na je, inawezekana kwa watu hawa kuuepuka unyanyasaji unaowasubiri kutoka kwa rais wao? Basi je, matokeo ya jambo hili yatakuwaje? Hapana jambo jingine litakalotokea hapo isipokuwa msichana itamlazimu kuuendea uovu kwa miguu yake mwenyewe. Ataifuata fedheha na aibu hiyo kubwa bila kupenda, na kisha atarudi nyumbani hali ya kuwa amekwishapata hasara ya kuvunjika kwa heshima yake na utu wake pia kagubikwa na kiza la ulimwengu machoni mwake.

Ewe msomaji mpendwa, hapana shaka kwamba watu wanaosoma au kusikia unyanyasaji huu, utawaona wanamlaani na kumshtumu rais huyu muovu. Lakini hebu tufikiri kidogo juu ya misingi inayosababisha mateso haya na tujiulize swali lifuatalo: Je! Ni nani mwenye makosa? Hivi kweli mwenye makosa siyo yule baba ambaye toka hapo mwanzo alimruhusu binti yake atoke ndani hali ya kuwa maungo yake yako wazi na uzuri wake unaonekana kwa kila mtu? Lau binti huyo angekuwa ni mwenye kujisitiri, hivi unadhani yule rais mpumbavu angelimtamani na kumfanya kuwa kiwindo chake? Ni baba ndiyo mwenye kustahili lawama tangu ile siku aliponunua television (ambayo ni adui mkubwa muovu aliyemo ndani) ili kuistarehesha familia yake kwa kuangalia vipndi viitwavyo kuwa ni vya watu walioendelea!! Baba huyo huyo ndiyo mwenye lawama siku zile alipokuwa akiichukua familia yake kwa ajili ya kwenda sinema kuangalia filamu za watu walio uchi. Na mama pia anastahili lawama… Je ! Siyo yeye yule ambaye alikuwa akizifumua nywele za binti yake na kumpamba utadhani siku hiyo ndiyo siku ya harusi yake na kisha akamwacha kwenda shuleni akiwa katika mazingira kama hayo?

Ni huyo mama aliyekuwa akimchagulia binti yake asiyejuwa kitu mavazi mafupi yanayobana mwilini ambayo hayamsitiri inavyopasa? Binti naye anapaswa kulaumiwa kutokana na matokeo hayo yenye kiza kinene cha majonzi kwa kuwa ni yeye mwenyewe ndiye aliyechagua tabia ya kuuweka wazi mwili wake, na pia akachagua kupita njia ngumu iliyojaa miba na mawe. Naam, watu hawa ndiyo tabaka la mwanzo la kulaumiwa, na baada ya hapo ndio mnapaswa kumlaani rais yule!!

 


[1]. Majallatud-Dastuur Lebanon.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini