Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME (S.A.W.W) 3

0 Voti 00.0 / 5

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME(S.A.W.W)  KUFARIKI

Sehemu ya Tatu

KUTOPATA HEDHI KWA HADHRAT FATIMA.

Imenukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (A.S)ya kuwa amesema:

(( Fatima (A.S) tangu alipo itwa Fatima aliepushwa na damu ya hedhi))

FATIMA AME EPUSHWA NA MOTO WA JAHANNAM.

Mtume (S.A.W.W)alisema((Je unafahamu kwanini umeitwa Fatima?wakati huo Imam Ally (A.S)akauliza,Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kwa nini ameitwa Fatima?Mtume akajibu:Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu amemuepusha huyu na kizazi chake kutokana na moto wa jahannam.

MALIPO KWA WENYE KUMPENDA FATIMA.

Imam Ridhaa (A.S) amenukuu kutoka kwa mababa zake,kutoka kwa Mtume imenukuliwa ya kuwa amesema: Mwenyezi Mungu amemuepusha mwanangu Fatima na watoto wake na kila mwenye kumpenda Fatima kutokana na moto wa jahannam.

FATIMA NI MALAIKA WA KIBINADAMU.

Ibnu Abbas amenukuu kutoka kwa Mtume (S.A.W.W)ya kuwa alisema :Mwanangu Fatima ni malaika wa kibinadamu,hapati hhedhi na wala hana uchafu mwingine,Mwenyezi Mungu amempa jina la Fatima basi yeye na wapenzi wake wameepushwa kutokana na moto wajahannam.

MACHUNGU YA FATIMA NI MACHUNG YA MTUME.

Mtume (S.A.W.W)amesema ((Fatima ni kipande cha mwili wangu,mwenye kumuudhi Fatima ameniudhi mimi.

FATIMA NI MBORA WA WANAWAKE WA DUNIANI.

Mtume (S.A.W.W)amesema :mwenyezi Mungu amewachagua wanawake wanne bora miongni mwa wanawake wa ulimwenguni nao ni Maryam,Asia,Khadija na Fatima.

Pia Mtume alimwambia Fatima :je huridhiki kuwa ni mbora wa wanawake wa duniani?na kuwa mbora wa wanawake katika umma huu?.

Pia Mtume alimambia Fatima :je huridhiki kuwa mbora wa wanawakewa pepni?

NAFASI YA FATIMA KWA MTUME.

Mwana Aisha amesema :Sijamuona mwnye kumfanana zaidi Mtume katika uzungumzaj mfano wa Fatima,kila wakati Fatima alipo kuwa akiingia nyumbani Mtume akimnyanyukia na kumbus na kumkaribisha na kumshika mkono na kumkalisha katika sehemu yake.

FATIMA NI MTU WA MWANZO KINGIA PEPONI.

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema ((Mwenye kunadi atanadi,enyi jamii ya viumbe fumbeni macho yenu mtoto wa Mhammad apite.

N imenukuliwa katika baadh ya riaya :Inamisheni vichwa na fumbeni macho mpaka Fatima avuke siraat (njia)bsi atapita hli ya kuwa ameandmana na watmishi sabini elfu wa pponi.

Mtume wa Mwenyzi mungu limwambia Ally :Watu wa mwanzo kuingia peponi watakuwa ni mimi,wewe,Fatima,Hassan,na Hussen.Hadhrat Ally akaliza je vipi kuhusu masha wetu?Mume akasema wtaingia nyuma yetu.

Fuatana nami katika makala ijayo kuhusu Maisha ya Mtukufu Huyu Baada ya Mtume (s.a.w.w) .

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini