Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME (S.A.W.W) 5

0 Voti 00.0 / 5

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME (S.A.W.W) KUFARIKI

Sehemu ya Tano

KUCHOMWA MOTO KWA NYUMBA YA FATIMA.(A.S)

Mmoja katiya waandishi wa hadidhi aitwae masood anatubainishia;Siku ya baia lilipelekwa kundi nyumbani kwa Fatima na kuunguza mlango,na walimtoa Ally kwa nguvu ndani ya nyumba yake na walimbana mbora wa wanawake yaani Fatima kati ya mlango na ukuta hadi mimba ya muhsin kutoka. Na vile vile bwana nadhaam anaelezea kuhusu tukio hili na anasema:Katika siku ya baia omar alisukuma mlango na dharuba ya mlango ilimfikia Hadhrat Faima Zhraa (A.S)na dharuba lile lilipelekea mimba ya fatima kutoka. Hivi ndivyo ilivyo unguzwa nyumba ya wahyi na utume,nyumba ambayo kizazi cha Ahlul baiti kitaendelea kupitia hapo.

Omar binil khatwab akiwa n kijinga cha moto mkononi alielekea nyumbani kwa Fatima akifuatana na khalid bin waliid,Mohammad bin Muslim,usaidi ban khudhair qunfudh, pamija na watu wenye kuabudu Dunia na walio tawaliwa na shetani,na hapo omar akampa qunfudh kijinga cha moto na kumuamrisha achome mlango wa nyumba na qunfudh akafanya kama alivyo amrishwa.Wakati huo Fatim alikuwa nyuma ya mlango akizungumza nao,na mlango wa nyumba ukasukumwa kwa nguvu na kumbana Fatima kati ya mlango na ukuta.Wakati huo Omar alikwenda mbele na kupiga tumbo la Fatima na mimba ya muhsin kutoka huku Fatima akipiga kelele ((Ewe baba,ewe Mtuma wa Mwenyezi Mungu))

SHAMBA LA FADAKI.

Fadaki ni zawadi ya Mtume kwa Fatima,baada ya Mtume kufanya mkataba wa suluhu na mayahudi ndipo alipo pata shamba hili.Na aya ikateremka ikisema ((Wape watu wako wa karibu haki zao))na ndio akamzawadia Fatima shamba hilo la Fadak.Alimzawadia katika zama za uhai wake ili iwe ni mali yake.Fadak lilikuwa ni shamba kubwa na lenye kutoa mazao kwa wingi.Baada ya kifo cha Mtume abubakar alidai ya kuwa Fadak ni mali ya waislaam,na mavuno yapatikanayo kwaka shamba hilo la Fadak ni mali ya baitul maal,kwa sababu Mitume hawarithiwi baada kufari kwao. Hii ilikuwa ni hukumu ya Abubakar na hukumu hii ya bwana huyu inapingana na Qur an tukufu. Wakati Fatima alipo kuwa akimiliki shamba la fadaki mapato yote ya shamba hilo aliwapatia wanyonge na wasio jiweza. Fatima alimwambia Abubakar :je katika Qur an ime elezewa ya kuwa wewe umrithi baba yako na mimi nisimrithi baba yangu?kwa hakika umeongopa na umezua uongo (umeleta jambo jipya)je unajua ya kuwa Qur an inasema((Na Sulaiman alimrithi Daud)).Navile vile katika kisa cha Zakaria ((Na unipe mimi walii atakae nirithi na atakae rithi kizazi cha yaquub)) Abubakar alitoa dalili kuwa amesikia hadithi kutoka kwa Mtume na riwaya hiyo hakuna alie inakili aspokuwa Abubakar na mwanae Aisha.Amesema nilimsikia Mtume akisema : ((Mitume hawarithiwi na waviachavyo ni sadaka))na yeye hajui ya kuwa haya ni madai yake na tuhuma kwa Mwenyezi Mungu,kwa sababu haiwezekani Mwenyezi Mungu asajili hukumu kwa Abubakar peke yake na wengine wasiwe na habari.wakati ambapo wahyi ulitelemka katika nyumba ya Fatima.Na vile vile Mtume katika kila hkumu iliyo teremka,kwanza alianza kwa kuwafahamisha watu wa nyumbani kwake akiwemo Fatima na Ally (A.S). Na lengo la Fatima lilikuwa ni kuonyesha kwamba kilicho fanyika ni makosa na upingaji.Na alitaka maneno haya ya Mwenyezi Mungu yawafikie watu na akasema ((Hakuwa Mohammad ispokuwa ni Mtime wa Mwenyezi Mungu na walipita kabla yake Mitume je akifa au kuuwawa mtarudi katika imani zenu ?)) kwa hivyo basi tuna kuta katika haya yaliyo tokea ilikuwa ni kutaka kuonyesha na kuwafahamisha watu haki ya Ahlul bayti na Dhuluma waliyo fanyiwa.

Fuatana nami katika makala ijayo kuhusu Maisha ya Mtukufu Huyu Baada ya Mtume (s.a.w.w) .

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini