Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

NI NANI AHLULBAYT (A.S) 2

0 Voti 00.0 / 5

AHLUBYT WA MTUME MUHAMMAD s.a.w.w kWA MUJIBU WA QUR'AN NA HADITHI ZA MTUME SAWW ZILIZO SAHIHI NA ZENYE KUKUBALIKA NA KUANDIKWA NA WANAZUONI WA AHLISUNA NA SHI'AH NI WATU MAALUM, AMBAO NI YEYE MTUME  MUHAMMAD SAWW NA ALLY BIN ABI TWALIB , FATIMAH BINT YA MTUME MUHAMMAD SAWW  HASSAN NA HUSSEIN NA TISA KATIKA KIZAZI CHA HUSSEIN AS

Wanazuoni wa Ahlisuna wakubwa wakubwa wamekiri hilo na kuandika vitabuni mwao.

Sunnah na Nyumba ya Mtume saww, Ahlul Bayt.

Ni nani hao wanaounda Nyumba ya Mtume saww?

HOJA YA PILI:

Tumeona hapo mbeleni kwamba kizazi cha Mtukufu Mtume saww kimepewa hadhi ya hali ya juu kabisa. Mtukufu Mtume saww amewataja wao kuwa baada ya Quran :.

إني تارك فيكم ثقلين أولهما كتاب الله وأهل بيتي لن يفترقا حتى يرد علي الحوض.

"Naacha miongoni mwenu vizito viwili, Qur-an na watu wa Nyumbani kwangu, na hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh ."

 Hivyo kizazi cha Mtukufu Mtume saww wakati wote wapo na Qur-an na siku zote watakuwa hivyo ; hawatapingana nayo. Kwa kuzingatia kigezo hiki kwenye vichwa vyetu, hebu na tuchunguze ile historia ya awali kabisa ya uislamu ili kuweza kuwaona wale miongoni mwa ndugu wa Mtume ambao wanaendana sawa na Qur-an.

Watu pekee Mtukufu Mtume saww amewataja kama amana yake na kuwa pamoja mshirika wa Quran ni Ally, Fatimah, Hassan na Hussein a.s.

Hakuna muislamu, awe Ahlulusuna au Shi'ah anayedai kwamba ndugu wengine wa Mtume walikuwa na elimu kubwa ama uchamungu zaidi kuliko familia hii, Ally, Fatimah, Hassan na Hussein a.s. Au wametumikia uislamu zaidi ya familia hii, Ally, Fatimah, Hassan na Hussein a.s. Zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kusema kwamba maneno "Nyumba ya Mtume" yanaweza kujumuisha ndugu wote wa Mtukufu Mtume Saww, kwa vile baadhi yao kama Abu Lahab walikuwa ni makafiri na hata wale walioamini uislamu hawakuwa wote katika kiwango kimoja. Wengi wao walikuwa ni watu wa kawaida tu na walisilimu baadaye kabisa, walichelewa.

Kwa kweli, watu pekee ambao kwamba nafasi hii kuandamana na Qur-an daima, kwa maneno mengine "Maasumina" (kuhifadhiwa kutofanya makosa) ni sifa yao, watu hao ni Ally, Fatimah, Hassan na Hussein a.s. Kadhalika kama muislamu ataulizwa ni nani anayeweza kuwa Ma'asum, Asiyefanya makosa, yeye ama atataja kundi hili, kwa mujibu wa Imani ya Shi'ah, au asitaje mtu yeyote kabisa, kwa sababu wale wasiokuwa Shi'ah (Ahlisuna) hawadai Uma'sum kwa kundi lolote la watu zaidi ya Mtume saww. Kuliweka tofauti kabisa, yeye hatamuweka mbele mtu yeyote mwingine kama mwenye kuunda muambatano wa kudumu na Qur-an.

Suala la Uma'sum litajadiliwa baadaye katika haki yake lenyewe.

Hapa hoja yetu ni kwamba, kwa mujibu wa hadithi za Mtukufu Mtume saww, Kuna umuhimu wa lazima kuwepo kikundi cha familia yake ambacho kitakuwa pamoja na haki wakati wote, na kwa vile nafasi hii imetangazwa kipekee kwa ajili ya watu hawa, ni wazi kwamba Mtukufu Mtume saww alikuwa nao akilini mwake wale ambao pekee walikuwa wamethibitishwa kwa ajili ya Uma'sum. Kama Ahlisuna wangekuwa wanasema kwamba watu fulani mbali na wale walioainishwa na Shi'ah walikuwa ni Ma'asum, mtu atapaswa kuamua kati ya madai haya mawili.

Hata hivyo, hili sio suala lenyewe, msimamo wa Shi'ah kwa hiyo unaelekea kutoa ufumbuzi pekee.

Ufumbuzi wenyewe ni kuwa Mtukufu Mtume saww mwenyewe ameeleza wazi ni nani Ahlul Bayt wake au al Itrah.

Hili linabainishwa na hadithi zifuatazo zinazo patikana katika Vyanzo vikuu vya Ahlisuna.

Ibun Jariir Tabariy ameandika katika kitabu chake Jaamiul Bayan, hadithi kumi na nne na zaidi ambazo zote amekiri kuwa Aya ya Utakaso imeshushwa juu ya watu hao wanne Ally, Fatimah, Hassan na Hussein a.s.

Mimi nakuonesha hadithi moja tu, imepokewa kutoka kwa Abu Said al Khudury kutoka kwa Ummu salama amesema :. "Pindi ilipoteremshwa Aya hii :.

إنما يريد الله ليذهب عنكم الرجس أهل البيت ويطهركم تطهيرا.

Hakika anataka Mwenyezi Mungu kukuondoleeni uchafu, Enyi watu wa Nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa. 33:33.

Mtukufu Mtume saww alimwita Ally, Fatimah, Hassan na Hussein a.s akawafunika kishamia (kisaa) chake cha Khaybar, kisha akasema :. "Ewe Mwenyezi Mungu, hawa ndio Ahli zangu" Ewe Mola wangu waondolee uchafu na uwatoharishe tohara ya kabisa kabisa.

"Ummu salama akasema :." Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi si katika AhIul Bait wako? Mtukufu Mtume saww akasema :. Hakika wewe upo katika Kheir, wewe ni miongoni mwa wake wa Mtume saww.

Kwa mujibu wa hadithi Ummu salama si Ahlul Bayt wa Mtume saww yeye ni mke wa Mtume saww.

Qurtubi katika tafsir yake kuhusiana na aya ya Utakaso :.

إنما يريد الله ليذهب عنكم الرجس أهل البيت ويطهركم تطهيرا.

Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul Bayt...33:33. ".

Qurtubi anasema :. Jambo hilo limeelezwa katika habari mbali mbali kwamba Mtukufu Mtume saww pindi ilipoteremshwa Aya hii kwake alimwita Ally, Fatimah, Hassan na Hussein a.s, akawafunika kishamia (kisaa) chake, kisha akainua mkono wake na kuelekeza mbinguni akasema :. Ewe Mola wangu hawa ndio Ahlul Bayt wangu waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.

Ibun Kathir ameandika hadithi zaidi ya tano kuhusiana na aya ya Utakaso.

Mimi nakuletea moja tu kati ya hizo. Imepokewa kutoka kwa Ummul Muuminina Aisha alisema kumwambia mtoto wa ami yake pindi alipomuuliza kuhusiana na Ally a.s akasema : "Unaniuliza juu ya mtu anayependwa mno na mjumbe wa Mwenyezi Mungu, bint yake aliye kipenzi kwake alikuwa chini yake (mke wa Ally). Hakika nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu akiwa amemwita Ally, Fatimah, Hassan na Hussein a.s akawafunika nguo yake na akasema :. Ewe Mola wangu, hawa ndio Ahlul Bayt wangu waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa. "Nilisogea kwao nikasema :. Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi si katika AhIi zako?" Mtukufu Mtume saww akasema : "Kaa kando Hakika uko katika Kheir.

Nasema :. Ama maneno ya Ummul Muuminina Aisha Aliposema :. Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi si katika AhIul Bayt wako? Mtukufu Mtume saww akasema : "Kaa kando hakik uko katika Kheir."

Hiyo ni dalili ya dhahiri kwamba wakeze Mtume saww hawahusiani kabisa na aya ya Utakaso, na hilo amekiri Ummul Muuminina Aisha, kwa hivyo tuwaelewaje wale wasiofahamu hilo.?

Fuatana nami sehemu ya kumi na moja ya Sunnah na Ahlul Bayt na ni nani hao? Hoja ya tatu.

REJEA:

  1. Jaamiul Bayan fi Taawilil Qur-an cha Tabariy, Jalada la kumi, Jz 22 UK 296 na kuendelea.
  2. Jaamiul Ahkaamul Qur-an cha Qurtubi Jz 14 UK 184.
  3. Tafsirul Qur-an Adhim cha Ibn Kathir Jz 3 UK 483 na kuendelea.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini