Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Imam Husein (A.S)

IMAMU HUSSEIN NI NEMBO YA HAKI

IMAMU HUSSEIN NI NEMBO YA HAKI

IMAMU HUSSEIN NI NEMBO YA HAKI KATIKA UISLAM Mara tu baada ya kifo cha Mtume Muhammad na kabla ya kukamilika kwa shughuli za mazishi, walijitokeza watu wengi waliokimbia mazishi hayo na badala yake kukimibilia katika ukumbi uliojulikana kwa jina la Saqifa Bani Saida. Lengo la kukimbilia katika ukumbi huo, ni kupitisha maazimio ya kutokubaliana na wasia aliouwacha Mtume na kuusisitiza kwa muda wa miaka yote 23 ya kipindi cha utume wake. Wasia huo ulikuwa ni kufuata uongozi wa watu wa nyumba ya Mtume (Ahlilbayt) ambao ni maimamu 12, kuanzia Imamu Aly Bin Abii Talib hadi kumalizia imamu Mahdi. Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Saqif Banii Saida, kiliibuka na mfumo mpya wa Utawala Haramu ambao ni kinyume na wasia wa Mtume. Katika mfumo huu wa utawala ulioanzia Sqifa Banii Saida historia ilishuhudia na kusajili watawala kama vile: Abuubakar, Omar Bin Khatab, Othman Bin Afan, Muawiya Bin Abi Sufiyan, Yazid Bin Muawiya na Wengineo.

Ufafanuzi

UJUMBE WA SIKU YA ASHURA

UJUMBE WA SIKU YA ASHURA UJUMBE WA SIKU YA ASHURA Katika Mji mtakatifu wa Qum, Irani; Ayatullah Al-Mirza Jawwad At -Tabrezi ameelezea rambirambi zake za dhati kwa wafuasi wa Aal-e-Muhammad (a.s.) kwa tukio hili linalowagusa la masaibu ya Karbala. Katika ujumbe wake kwenye tukio la siku ya Ashura, mtukufu Ayatullah At-Tabrezi alisema kifo cha Bwana wa Mashahidi Hazrat Aba Abdillah Al-Hussain (a.s.) ni njia inayong’ara na itoayo mwanga kwa Waumini, wapigania Uhuru, wanaonyanyaswa na kwa kila tabaka la jamii na pia kwa Dini na Imani zote. Ayatullah alisema kuwa fundisho linalopatikana katika tukio hili la huzuni ni kuwa ushindi kati ya Haki na Batili wakati wote upo pamoja na Haki (ukweli). UJUMBE WA SIKU YA ASHURA Siku ya Ashura hutonesha majeraha yetu, na hupelekea macho yetu kububujikwa na machozi kutokana na vipenzi vyetu kuuliwa mashahidi katika ardhi ya Karbala, na kutuweka katika usumbufu na majuto hadi siku ya Hisabu (Kiyama). Hivyo, huyu ni Husain (a.s.) ambaye watu wapaswa kumlilia (na kuomboleza) kwa kuuliwa shahidi.(Imam Ali Raza (a.s.)). Sisi na ndugu zetu wote tunakumbuka (mahali hapa) katika siku hizi maalumu za matukio ya Imam Husain (a.s.), pia Mapinduzi ya Kiislamu katika nyanja zote yakiongozwa na Imam Husain (a.s.), Ahlul Bayt wake, Mashaba, Wanamume, Wanawake, Wazee, Vijana na Watoto kwa upande mmoja na matendo ya kikatili yaliyotendwa na Madhalimu wa mauaji haya kwa upande mwingine.

Ufafanuzi

WAAFRIKA WALIOJITOA MUHANGA KARBALA

WAAFRIKA WALIOJITOA MUHANGA KARBALA WAAFRIKA WALIOJITOA MUHANGA KARBALA Ni mara nyingine tena imewadia Siku ya Ashura mwezi 10 Muharram, pia ni wakati mwingine Uislamu unapata nguvu kutokana na msukumo wa tukio la masaibu ya Karbala; na hii ni indhari na ni kumbukumbu kwa matendo ya kishujaa yaliyofanywa na Wana wa Afrika ambao waliandika ujumbe wa (Haki) kweli kwa damu yao katika ardhi ya Karbala. Uislamu, pamoja na Ujumbe wake kwa Walimwengu wote, tangu hapo awali ulimpa Uhuru mwanadamu kutoka katika himaya ya Wadhalimu. Ilikuwa suala lisilozuilika kwamba kilio cha “Hapana apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah” kingeunganisha watu wa Mataifa yote na wa Imani mbalimbali. Pamoja na ujumbe wake wa kujikomboa mwanadamu kiroho, Qur’an Tukufu imewalingania binadamu kuungana pamoja bila ya kujali rangi wala utaifa wao. “Hapana shaka mbora wenu mbele ya Allah (s.w.t.) ni yule mwenye kumcha Mwenyezi Mungu" (Qur’an, 49:13). Ni kwa aya hii Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu Haki ya Uhuru wake. Wenye kufuzu na kulipwa mema (Pepo) ni wale tu watakaotii amri zake bila kujali utaifa wao wala utukufu na ubora wa makabila yao.

Ufafanuzi

IMAM HUSEINI BIN 'ALI (A.S.)

IMAM HUSEINI BIN 'ALI (A.S.) IMAM HUSEINI BIN 'ALI (A.S.) Jina: Huseini. Kuniyah: Abu 'Abdillah. Lakabu: Sayyidu 'sh-Shuhad?. Baba: 'Ali bin Abi T?lib Mama: Fatimah bint wa Mtume. Kuzaliwa: 3 Shabani 4 A.H. Madina Kufariki: 10 Muharram 61 A.H. Karbala, Iraq. 1. Kuzaliwa na maisha yake ya mwanzo: Imamu Huseini (Sayyidu 'sh-Shuhad? / Bwana miongoni mwa mashahidi), mtoto wa pili wa'Ali na Fatimah, alizaliwa mwaka wa 4 A.H., na baada ya kaka yake Imamu Hasani kuuliwa shahidi akawa Imamu kwa amri ya Allah (kupitia kwa Mtukufu Mtume) na wosia wa kaka yake. Imamu Huseini siku zote alikuwa na kaka yake wakati wa uhai wa mtume na Imamu 'Ali; alichangia katika matukio muhimu zaidi ya kipindi hicho. Alikuwa bega kwa bega na kaka yake wakati wa kipindi kigumu cha Uimamu wa kaka yake. Uimamu wake mwenyewe ulikuwa wa kipindi cha miaka kumi 2. Utawala wa Mu'awiyah: Imamu Huseini aliishi chini ya masharti magumu ya uonevu na mateso. Hii ilitokana na ukweli kwamba awali ya yote sheria za dini na kanuni zimepoteza uzito na sifa zake nyingi na sheria za serekari ya Bani Umayya zimepata mamlaka kamili na uwezo. Pili, muawiyah na wasaidizi wake walitumia kila njia inyowezekana kuwaweka kando na kuwaondoa nje ya njia Ahlul Bayit wa Mtume na Shi'ah, na hivyo, kufutilia mbali jina la 'Ali na familia yake. Na juu ya yote, Mu'awiyah alitaka kuimarisha msingi wa ukhalifa wa mtoto wake, Yazidi, ambaye kwa sababu ya ukosefu wake wa kanuni na aibu alipingwa na kundi kubwa la Waislam. Kwahiyo, ili kuzima upinzani wote, Mu'awiyah alichukuwa njia mpya na kali zaidi, kwa nguvu na kulazimika, Imamu Huseini aliishi siku hizo na kuvumlia kila aina ya uchungu wa akili na kiroho na mateso kutoka kwa Mu'awiyah na wasaidizi wake - mpaka katikati ya mwaka wa 60 A.H. Mu'awiyah alifaliki na mtoto wake Yazidi akachukua nafasi yake.

Ufafanuzi

IMAMU HUSSEIN KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

IMAMU HUSSEIN KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI IMAMU HUSSEIN KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI  Edward G. Brown Sir Thomas Adams Profesa wa lugha ya kiarabu na masomo ya kimashariki katika chuo kikuu cha Cambridge: " "… ni kumbukumbu ya uwanja uliojaa damu wa Kerbala, ambapo mjukuu wa Mtume alianguka, akateswa na kiu na kuzungukwa na miili ya watu wake waliouwawa, kifo hicho wakati wowote chatosha kuchemsha hisia kali hata za asiyejali, na moyo ambao uchungu, hatari na kifo hupungua na kuwa mdogo mno." [A Literary History of Persia, London, 1919, p. 227] Ignaz Goldziher (1850-1921) Mhangari mashuhuri na msomi wa kimashariki: " "Tangu siku ile nyeusi ya Karbala, historia ya kizazi hiki…imekuwa ni mlolongo wa kutabika na mateso. Haya huelezwa kwenye mashairi na tungo fasihi za kuhusu kufa shahid - kwenye madhehebu ya Shia - na kufanya majilisi za Shia kuwapo katika mwanzo wa mwezi wa Muharram, ambapo siku ya kumi (a'shura) huwekwa kuwa ni siku maalum ya kumbukumbu ya msiba wa Karbala. Matukio ya janga hilo huwa yanaonyeshwa kwa njia ya ta'aziya. 'Sikukuu zetu ni siku za maombolezi', akitimiza mashairi haya ni amiri wa kuieleza hali ya Mashia akikumbusha mitihani mingi iliyokipata kizazi cha Mtume. Manung'uniko na maombolezo juu ya maovu na mateso waliyofanyiwa kizazi cha Ali, na maombolezo juu ya watu wake waliokufa mashahid: Haya ndiyo mambo ambayo wafuasi wao waaminifu hawawezi kuyaacha. Hata kuna methali isemayo: '..Yahuzunisha zaidi kuliko machozi ya Shia..' imekuwa ni methali itumikayo ya kiarabu." [Introduction to Islamic Theology and Law, Princeton, 1981, Uk. 179]

Ufafanuzi

NAFASI YA IMAMU HUSEIN

NAFASI YA IMAMU HUSEIN NAFASI YA IMAMU HUSEIN Kila mwaka unapowadia mwezi wa Muharram nyoyo za wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume wetu Muhammad saw na Ahlubaiti zake zinashikwa na hali ya huzuni na majonzi makubwa. Siku hizi zinakwenda sambamba na harakati na vikao vya kuhuisha mapambano makubwa ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein bin Ali (as) katika ardhi ya Karbala. Kwa mnasaba huo pia tunatuma sala na salamu zetu kwa mkombozi mkubwa wa mwanadamu Nabii Muhammad amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, Ali zake na Ahlubaiti wake waliotakaswa na dhambi na mambo machafu. Sala za salamu za Mwenyezi Mungu zikufikie wewe Abu Abdillah Hussein bin Ali na roho zilizouawa shahidi katika kupigania haki na dini ya Allah. Salamu zaAllah ziwafikie usiku na mchana hadi siku ya kufufuliwa viumbe kwa ajili ya hesabu. Risala na ujumbe mkubwa wa Manabii na mawalii wote wa Mwenyezi Mungu ilikuwa ni kupambana na dhulma na uonevu na kusimamisha haki na uadilifu. Mitume na mawalii wote walikuwa na jukumu la kusimamisha dini ya haki, uhuru na kumuonesha mwanadamu njia ya saada na uongofu.

Ufafanuzi

ALIYOYASEMA MTUME (S.A.W.W) KUHUSU IMAM HUSEIN (A.S)

ALIYOYASEMA MTUME (S.A.W.W) KUHUSU IMAM HUSEIN (A.S) Imam Hussein(as) ni mtoto wa Imam Ali bin Abi talib(as) bin Abdul Muthwalib bin Hashim. Mama yake ni Fatimatuz-zahra(sa), ambaye ni binti ya mtume Muhammad(saww). kwa hivyo ni mjuku wa mtume Muhammad(saw). Jambo hilo ni wazi kwa kila aliyesoma tarehe ya kiislamu,kwani

Ufafanuzi

RUHUSA YA KUOMBOLEZA

RUHUSA YA KUOMBOLEZA MAJLIS YA PILl YAH: RUHUSA YA KUOMBOLEZA; Hapana shaka kwamba ipo ruhusa ya kuomboleza vifo vya Waumini, na kwamba jambo hilo ni halali, na hapana dalili iliyo kinyume cha hivi.    

Ufafanuzi

ARUBAINI YA IMAM HUSEIN (A.S)

ARUBAINI YA IMAM HUSEIN (A.S) Arubaini ya Imam Hussein, Ukurasa Mwingine wa Mapambano ya Ashura

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini