Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 3

MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 3

MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 3 KUZALIWA MPAKA KUANZA KWA WAHYI MWENDELEZO WA MAKALA NO:2 MKATABA WA HUDAYBIA NA KUANGUKA KWA MAKKAH Katika mwaka wa sita wa wa hijiria, Mtume aliamua kwenda Makkah kuhiji. Watu wa Makkah waliwazuia Waislamu mahali panapoitwa Hudaybia na hawakuwaruhusu kuingia mjini hapo. Makabiliano haya yaliiishia kwenye mkataba wa amani baina ya Mtume na Makuraishi wa Makkah. Mkataba huu wa amani ulijenga mazingira salama kwa kiasi fulani, kwa Mtume kuanza kupanua ule wito wa Uislamu kwa makabila na watu walio mbali na bara Arabu. Kama matokeo ya shughuli za Mtume na jitihada zisizo na ubinafsi za Waislam katika kipindi kile, Uislam uliendea kote katika peninsula ya Arabia. Zilikuwepo pia barua zilizoandikwa kwa wafalme wa nchi zingine kama vile Persia, Byzantine na Abyssinia zikiwaalika wafalme hao kuukubali Uislamu. Wakati huu Mtume aliishi katika umasikini na ufukara na alikuwa na fahari nayo hali hiyo. Hakuwahi kutumia muda wake wowote bure bure tu. Bali muda wake wote uligawanywa katika sehemu tatu: moja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, katika kumuabudu na kumkumbuka Yeye; sehemu nyingine kwa ajili yake binafsi na watu wa nyumbani kwake na mahitaji ya nyumbani; na sehemu kwa ajili ya watu. Katika wakati wa sehemu hii ya muda wake alijishughulisha katika kueneza na kufundisha Uislamu na elimu zake, kusimamia mahitaji ya jamii ya Kiislamu, kuondoa maovu yoyote yaliyokuwepo, kuhudumia mahitaji ya Waislam, kuimarisha mafungamano ya ndani na nje, na mambo mengine kama hayo. Moja ya masharti ya mkataba huu wa amani lilikuwa ni kwamba Maquraishi wasingeweza kuwadhuru Waislamu au yoyote kati ya washirika wao walioungana nao. Sharti hili, hata hivyo lilikiukwa na Maquraishi pale walipolisaidia kabila la Bani Bakr dhidi ya kabila la Bani Khuza’a-hilo la kwanza ni washirika wa Maquraishi na hili jingine ni washirika wa Waislamu. Mtume aliwaomba Maquraishi kuheshimu mkataba huo, wavunje ushirikiano wao na kabila la Bani Bakr na kuwafidia wale waathirika wa uchokozi wao. Maquraishi walikataa kutii na kufuata masharti ya mkataba wao. Mtume, akiwa na jeshi lililoandaliwa vizuri lenye nidhamu ya hali ya juu, lenye takriban askari 10,000 liliingia Makkah katika mwaka wa nane baada ya hijiria na wakaiteka bila upinzani mkubwa. Mji huo, ambao ulikuwa umekataa ujumbe wake, na kupanga njama dhidi ya wafuasi wake na wakaungana katika njama ya kumuua yeye, sasa akawa chini ya huruma yake. Mtume aliwauliza watu wa Makkah: “Ni nini mnachoweza kutarajia kutoka kwangu?” Wao wakajibu: “Huruma! Ewe bwana mkarimu na mtukufu!” Kama angependa, angeweza kuwafanya wote kuwa watumwa wake. Lakini Muhammad – “rehma kwa ajili ya ulimwengu” akasema: “Nitaongea nanyi kama Yusuf alivyoongea na ndugu zake. Sitawasuteni leo; Mwenyezi Mungu atakusameheni, kwani Yeye ni Mwingi wa Huruma na Upendo. Nendeni, mko huru kabisa!” Kwa kuanguka kwa Makkah, kila kizuizi cha mwisho katika njia ya Uislamu kilikuwa kimeondolewa na watu wengi na makabila ya Waarabu katika peninsula ya Arabia yakaanza kuukubali ujumbe wa Uislam. Hivyo ule mwaka wa tisa wa hijiria unajulikana kama “Mwaka wa ujumbe” kwa sababu ya ile idadi ambayo siyo ya kawaida ya wajumbe waliokuwa wakija Madina kuja kutoa heshima zao kwa Mtume hapo Madina. HIJJA YA MWISHO NA KIFO Katika mwaka wa kumi wa hijiria, Mtume aliamua kwenda kufanya Hijja. Aliwaalika Waislamu kuungana naye na wajizoeshe kanuni za hija. Zaidi ya Waislam mia moja elfu waliungana naye katika hijja hii. Ingawa hii ni hijja ya mwanzo na ya mwisho ya Mtume, lakini inajulikana kama “al-Hijjatul’wida hija ya muago.” Aliichukua fursa hii ya ule mkusanyiko ambao haujawahi kutokea ili kuwakumbusha Waislamu juu ya mambo mengi muhimu na thamani ya Uislam. Akiwa njiani akirudi kwenda Madina, alisimama mahali panapoitwa Ghadir Khum na akatoa hotuba ndefu sana ambamo alifanya muhtasari wa yale mafundisho muhimu makuu ya Uislam, akawajulisha kuhusu kifo chake kilichokuwa kina karibia na akamteua Ali bin Abi Talib kuwa mrithi wake.

Ufafanuzi

MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 2

MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 2 MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 2 KUZALIWA MPAKA KUANZA KWA WAHYI MUENDELEZO WA MAKALA ILIYOPITA KUHAMA KWENDA MAKKAH Katika takriban mwaka wa kumi wa Utume wake, wakati Mtume alipoondoka kwenye “bonde la Shi’ab Abu Talib”, ami yake, Abu Talib, ambaye pia alikuwa ndiye mlinzi wake pekee, alifariki dunia, kama alivyofariki pia mke wake mpendwa Khadijah. Kuanzia hapo ikawa hakuna tena ulinzi wa maisha yake wala mahali pa kukimbilia. Hatimaye wale waabudu masanamu wa Makkah walibuni mpango wa siri wa kumuua Mtume. Wakati wa usiku wao waliizunguka nyumba yake kwa nia ya kuivamia nyumba yake mwishoni mwa usiku na kumkata kata vipande vipande wakati akiwa kitandani. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alimjulisha kuhusu mpango huo na kamuamuru kuondoka na kwenda Madina, wakati huo ikiitwa Yathrib. Mtume alimwambia ‘Ali alale kitandani mwake ili kwamba maadui wasigundue kutokuwepo kwake; bila kusita ‘Ali alikubali kutoa mhanga maisha yake kwa ajili ya Mtume na akalala katika kitanda cha Mtume. Kisha Mtume akaondoka hapo nyumbani chini ya ulinzi Mtukufu wa kimbinguni, akiwapita maadui zake katikati yao, na akichukua hifadhi ndani ya pango karibu na Makkah. Baada ya siku tatu, maadui zake, baada ya kutafuta kila mahali, walikata tama ya kumkamata yeye na wakarudi Makkah. Mtume naye akaondoka kuelekea Yathrib.

Ufafanuzi

MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 1

MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 1 MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 1 KIDOKEZO KIFUPI CHA WASIFA KUZALIWA MPAKA KUANZA KWA WAHYI Muhammad al-Mustafa, Mtume wa mwisho wa Allah, alizaliwa Makkah, Arabia mnamo mwezi 17 Rabi al-Awaal, mwaka wa kwanza wa tembo (Amul Fiil) 570 A.D. Mtume Muhammad (s.a.w.) alizaliwa katika ukoo wa Bani Hashim, wa kabila la Quraishi, ambao walikuwa ndio walioheshimiwa sana katika familia za Kiarabu. Bani Hashim walikuwa ni kizazi cha Ismail, mwana wa Nabii Ibrahim. Babu yake Mtukufu Mtume, Mzee Abdul Muttalib alikuwa ndiye Mkuu wa Bani Hashim na vile vile alikuwa ndio mlezi wa al- Kaaba. Baba yake yeye Mtume, alikuwa anaitwa Abdullah na mama yake aliitwa Amina. Baba yake alifariki miezi michache kabla ya kuzaliwa kwake. Akiwa na umri wa miaka sita, Mtume akampoteza mama yake pia na yeye akawekwa chini ya uangalizi wa babu yake, Abdul Muttalib. Lakini babu yake naye akafariki baada ya miaka minne; na safari hii, ami yake Mtume, Abu Talib alichukua dhima juu yake na akawa mlezi wake, akimchukua kuishi naye nyumbani kwake mwenyewe. Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.) kwa kiasi kikubwa alikulia nyumbani kwa ami yake na hata kabla ya kufikia umri wa balehe alikuwa akifuatana na ami yake kwenye safari za kibiashara kwa misafara. Mtukufu Mtume hakuenda shule yoyote, hata hivyo, baada ya kufikia umri wa utu uzima alikuwa maarufu kwa hekima zake, ushauri, uaminifu na ukweli wake. Mara akawa anajulikana kama “as-sadiq al-amin” – mkweli, mwaminifu. Ami yake, Abu Talib alikuwa kila mara akisema “Hatujasikia uwongo wowote kutoka kwa Muhammad, wala kuwa na tabia mbaya au kufanya uharibifu. Kamwe hacheki ovyo ovyo wala kuzungumza wakati usiofaa.

Ufafanuzi

HOJA ZA MAULIDI YA MTUME (S.A.W.W)

HOJA ZA MAULIDI YA MTUME (S.A.W.W) HOJA ZA MAULIDI YA MTUME (S.A.W.W) Maulidi ni Kiswahili cha neno la Kiarabu, mawlid. Neno hili lina maana ya "mazazi" au "kuzaliwa kwa…" (birthday). Kwa kawaida, linapotumiwa na Waislamu, huwa na maana ya siku aliyozaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), au hafla ya kuisherehekea siku hiyo. Waislamu wa ulimwengu mzima, ifikapo tarehe 12 ya Mfungo Sita (Rabiul Awwal), husoma maulidi na kuisherehekea siku hiyo kwa furaha kubwa. Sherehe hizo, kwa dasturi, haziishii tarehe hiyo tu, bali huendelea hata kwa miezi miwili mitatu baada ya hapo. Hili huwa ni kwa sababu ya Waislamu wa kila nyumba, kila mtaa, kila mji na kila nchi kutaka kushiriki katika sherehe hizo na kupata baraka zake. Vile vile huwapa Waislamu nafasi ya kutembeleana na kushirikiana katika sherehe hizo - jambo ambalo lisingewezekana lau watu wote wangeliamua kuzifanya sherehe hizo siku hiyo hiyo moja tu. Kwa nini kusoma maulidi? Waislamu husoma maulidi kwa sababu mbalimbali. Kati ya hizo ni: (i) kuikumbuka na kuitukuza siku aliyozaliwa mbora wa viumbe vyote, aliyetutoa vizani na kututia kwenye nuru; (ii) ni njia moja ya kutoa shukrani zetu kwa neema hiyo; (iii) katika sherehe hizo, hupatikana fursa ya kukumbushana maisha ya bwana mkubwa huyo na mafunzo yake; (iv) hupatikana fursa ya Waislamu wa madhihabi na mataifa mbalimbali kushirikiana na kuziweka kando hitilafu zao; na (v) mikusanyiko hiyo huleta athari kwa wasio Waislamu ya kuupenda Uislamu, na hata kusilimu.

Ufafanuzi

MTUME KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

MTUME KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI Washington Irving (1783-1859 )Anayejulikana kama "The first American man of letters": " "Alikuwa na tabia tulivu na mwenye nidhamu katika chakula, na akifuata sana utratibu wa kufunga. Hakuvama katika kupenda mavazi ya mapambo, namna wanavyojionyesha wenye mawazo finyu; pia kunyenyekea kwake katika mavazi kuliathiri pia kulionyesha matokeo ya kutopenda kwake kujitofautisha... alikuwa muadilifu katika muamala wake wa kibinafsi. Aliamiliana na watu wote kwa usawa: marafiki na wageni, matajiri na maskini, na wenye nguvu na wanyonge; na alipendwa na watu walala hoi kwa kuwa jinsi alivyokuwa akiwapokea kwa vizuri, na kusikiliza matatizo yao... Ushindi wake wa kijeshi vitani haukumfanya awe na ujuba au kibri, kama ambavyo wengine wangefanya hivyo kwa kuathiriwa na ubinafsi. Alipokuwa katika enzi za utawala wake wenye nguvu, aliendelea kujiweka kinyenyekevu kama alivyokuwa katika siku za shida. Alijiweka mbali na heshima kuu ya uongozi na hakuwa akifurahishwa iwapo ataingia mahali na apewe heshima kuu mno."

Ufafanuzi

HISTORIA YA MTUME (S.A.W.W).

HISTORIA YA MTUME (S.A.W.W). HISTORIA YA MTUME (S.A.W.W). Assalaam Alaikum Warahmatullah Taala Wabarakaatuh. Maisha ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) mwana wa Abdullah yako wazi zaidi kuliko yale ya Mitume (a.s) wengine waliomtangulia.Kwa nini? jawabu lake ni kwasababu: Kadiri wakati ulipokuwa ukizidi kupita ndivyo mabadiliko ya kihistoria,mabadiliko ya vitabu,mabadiliko ya sheria na hata shakhsia zao yalivyozidi kutokea, vyote hivyo vilipotoshwa na hivyo maisha yao kutojulikana vyema. Kwa hakika hakuna nyaraka zilizopo ispokuwa zile tunazozipata kutoka katika Kitabu Kitukufu cha Dini ya Kiislaam ambacho ni Qur'an Tukufu ambayo ni maneo ya Mwenyeezi Mungu (s.w) na Maneno ya Mtume (s.a.ww) na Watu wa nyumba yake waliotwaharishwa yaani Ahlul bayt wake (a.s). Kuna historia iliyokuwa wazi na safi kabisa inayozungumzia maisha ya Mtume (s.a.w) na kuzibainisha sifa za maisha yake kwa njia safi yenye kuridhisha kabisa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ni Mtume wa mwisho ambaye kachaguliwa na Mwenyeezi Mungu (s.w) kuwaongoza walimwengu wote.Hivi sasa ni karne kumi na nne (14) zimepita,katika kipindi hicho yaani karne 14 zilizopita wanadamu walikiishi katika hali ambayo hakuna athari yoyote ile ya Tawhid iliyokluwa ikionekana ispokuwa kutajwa jina tu.Watu walikuwa wameipuuza tawhid kikamilifu.Maadili na uadilifu vilikuwa vimetoweka kabisa katika jamii ya wanadamu.mwenye nguvu ndiye aliyekuwa akitamba na kuonekana dunia imeumbwa kwa ajili yake peke yake na wengine hawana haki katika dunia hii,ubabe ulitawala kila sehemu.Kaaba Tukufu ilikuwa imegeuzwa na kuwa sehemu ya kuabudia masanamu na Dini ya Nabii Ibrahim (a.s) ilikuwa imebadilishwa na kuwa ya kuiabudu miungu mbali mbali.

Ufafanuzi

MTUME (S.A.W.W)

MTUME (S.A.W.W) UTUME si jambo lisilojulikana katika dini za Kiyahudi na Kikristo. Katika Uislamu, utume umepewa hadhi na umuhimu mkubwa na wa kipekee kabisa. Kutokana na maelekezo ya Uislamu, Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu kwa lengo takatifu ambalo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu na kuishi kwa kufuata mafundisho na muongozo itokayo Kwake. Mwanadamu angewezaje kujua wajibu wake kwa Mwenyezi Mungu na lengo la kuumbwa na kuishi kwake hapa ulimwenguni bila ya kupata mwongozo sahihi na ulio wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu? HIVYO Mwenyezi Mungu alimchagua kutoka katika kila jamii, Mtume (mteule au nabii) ili apitishie ujumbe wake kwa watu au jamii kama alivyokusudia iwe. Mitume walichaguliwaje? Mtu anaweza kujiuliza ni vipi mitume walichaguliwa, na ni mitume wangapi walipewa kazi hiyo tukufu ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu? Utume au Unabii ni baraka au neema zitokazo kwa Mwenyezi Mungu na ni mapenzi yake anayomjaalia mja wake ampendaye. Lakini labda baada ya kupitia historia ya maisha ya Manabii kwa wanadamu, tunaweza kuelewa ni vigezo (mambo) gani muhimu vinavyomtofautisha Mtume na mtu au watu wengine.

Ufafanuzi

MUAMALA WA MTUME

MUAMALA WA MTUME MUAMALA WA MTUME Muamala wa Mtume na Jinsi ya kulingania Ukweli Makala hii iliyoko mbele yako inahusiana na tabia njema na muamala wa Mtume Mtukufu (SAW) katika kualika watu kwenye ukweli. Kwa kuitalii kwa makini utatambua kwamba, kinyume na inavyodaiwa na watu wenye chuki na maslahi binafsi ya siri, Uislamu ulienea kutokana na mantiki yake ya nguvu na sio jambo jingine lolote. Kwa maelezo hayo wale watu wanaodai kwamba Uislamu ulienea na kusambaa kwa ncha ya upanga na mabavu ni waongo wakubwa walio na agenda ya siri kuhusiana na suala hilo. Tunamualika sasa msomi mpenzi kusoma kwa makini yaliyomo humu kwa faida yake mwenyewe na faida ya Waislamu wenzake. Mwenyezi Mungu amemuarifisha Mtume mtukufu (SAW) kwa maneno na ibara maalumu kwa kusema: 'Ewe Mjumbe wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Kwa yakini Sisi tumekutuma, (tumekuleta uwe) shahidi na mtoaji wa habari nzuri na muonyaji. Na uwe muitaji (wa watu) kwa Mwenyezi Mungu, kwa idhini yake, na (uwe) taa itoayo nuru' (33:45-46). Kuhusiana na aya hii, moja ya majukumu muhimu ya Mtume Mtukufu wa Uislamu (SAW) lilikuwa ni kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu. Bila shaka jukumu hili zito lilihitajia kuwepo kwa mbinu na njia maalumu ya kufikiwa lengo hilo. Kuna njia tatu muhimu ambazo zimetajwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kufikiwa lengo hilo nazo ni hekima, ushauri mzuri na mawaidha au majadiliano mema: 'Waite (watu) katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora' 916:125). Kwa kutegemea ayah ii, njia ya kwanza ya kualika na kuita watu kwa Mwenyezi Mungu ni kutumia hekima na busara, mantiki na hoja zilizo thabiti na madhubuti.

Ufafanuzi

MTUME WA AMANI

MTUME WA AMANI MTUME WA AMANI   Qur'ani Tukufu inamuarifisha Mtume Muhammad (SAW) kuwa rehema kwa walimwengu wote. Inasema mtukufu huyo ana akhlaki, maadili na tabia adhimu, na kwamba watu walivutiwa na kukusanyika pembeni yake kutokana na tabia zake njema, maneno yake laini na ya unyenyekevu, kifua kipana na upole wake. Inaendelea kusema kuwa kama asingelikuwa hivyo na kuwa mkali, basi watu wangejiweka mbali naye na kutomkaribia kabisa. Alikuwa akishughulishwa na kutaabishwa mno na matatizo yaliyokuwa yakiwapata Waislamu na wafuasi wake. Katika aya nyingine, Qur'ani inasema kuwa Mtume alikuwa akishughulishwa mno na hali ya Waislamu kiasi kwamba alikaribia kutoa mhanga roho yake katika njia ya kutaka kuwaongoza Waislamu na kuwaepusha na madhara na upotovu. Tangu zama za kale, makundi maovu ya kijahili na yenye uadui dhidi ya Uislamu yamekuwa yakitumia hila na upotovu kama chombo cha kujinufaisha na kukariri upotovu huo ili kuudhihirisha kuonekana kuwa ni ukweli halisi. Karne nyingi kabla ya kuanza Vita vya Msalaba dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi, serikali na tawala za nchi hizo zilifanya juhudi kubwa za kupotosha sura halisi na nzuri ya mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW). Zilijaribu kumuonyesha Mtume Mtukufu (SAW) kuwa mtu aliyependa vita na kuwa mbali na misingi ya amani, njama na upotofu ambao hadi leo ungali unaenezwa ulimwenguni na nchi hizo zilizo na chuki kubwa dhidi ya Uislamu. Licha ya kuwa nchi hizo huzungumzia udharura wa eti kuzingatia usamehevu, kuheshimu imani, matukufu na fikra za upande wa pili, kuishi pamoja kwa amani na hata kuziarifisha serikali na nchi zao kuwa zisizo za kidini, lakini ukweli wa mambo ni kuwa misingi ya kiutamaduni na kifikra za watawala na serikali za nchi hizo, bado haijabadilika na ni ileile ya ubaguzi na uadui dhidi ya imani nyinginezo na hasa Uislamu. Licha ya kuwa hakuna tofauti yoyote ya kimsingi kati ya mitume wa Mwenyezi Mungu na kwamba wote walitumwa kwa ajili ya kufikia lengo moja la kurekebisha jamii na kumuongoza mwanadamu kwenye njia nyoofu, lakini nchi za Magharibi daima zimekuwa zikifanya juhudi za kuwatenganisha mitume hao na kudai kwamba baadhi yao walikuja kuleta amani na upendo hali ya kuwa wengine walikuja kuleta ghasia na machafuko.

Ufafanuzi

MUASISI WA USTAARABU

MUASISI WA USTAARABU MUASISI WA USTAARABU Ustaarabu wa Kiislamu umejadiliwa na kuchunguzwa na wanafikra katika pande mbalimbali na vitabu na makala nyingi na za aina mbalimbali zimeandikwa kujadili suala hilo. Hata hivyo suala lililopuuzwa na kufumbiwa macho kwa kiasi kikubwa katika medani hiyo ni nafasi ya kimsingi na isiyo na kifani ya Mtume Muhammad amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake na Ali zake katika kuweka jiwe na msingi na kuasisi ustaarabu huo adhimu. Mche wa mti huo mkubwa ulipandikizwa kwa mikono mitukufu ya Nabii Muhammad (saw) na misingi yake ikaimarishwa kwa hijra na kuhamia mtukufu huyo katika mji wa Yathrib. Makala hii inachunguza misingi muhimu ya ustaarabu katika mtazamo wa wasomi na nafasi ya Nabii Muhammad (saw) katika kuleta amani na utulivu, mshikamano wa kitaifa, ushirikiano na muawana, maadili bora, subira na ustahamilivu, umoja na mshikamano na hali bora ya wastani ya kimaisha ambavyo vyote ni miongoni mwa sababu za kujitokeza ustaarabu na kustawi kwake. Dibaji Ustaarabu wa Kiislamu umechunguzwa na kufanyiwa utafiti na wasomi mbalimbali katika pande mbalimbali. Ustaarabu huo wenyewe umebuni mbinu na utaratibu wa mfumo mkubwa zaidi wa kisayansi na kuitunuku dunia shakhsia kubwa za kielimu katika nyanja mbalimbali za sayansi. Kwa hakika maendeleo na ustawi wa haraka, adhama, ukamilifu na upana wa ustaarabu wa Kiislamu na vilevile kushiriki kwa matabaka mbalimbali ya mataifa na kaumu tofauti katika kujenga na kustawisha ustarabu huo ni miongoni mwa mambo yaliyowastaajabisha wengi. Mambo hayo yamewalazimisha wanafikra wengi hususan wa Kimagharibi kuinua juu mikono pale wanapozungumzia na kuchunguza historia ya ustaarabu wa Kiislamu.

Ufafanuzi

ARUBAINI YA IMAMU HUSEIN (A.S)

ARUBAINI YA IMAMU HUSEIN (A.S) ARUBAINI YA IMAMU HUSEIN (A.S) Kuwa na Kukumbuka ya Arubaini ya Imam Hussein (as) ni fursa nzuri ya kutafakari kuhusu malengo ya mapambano ya mtukufu huyo na masahaba zake. Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa mapambano ya Imam Hussein (as) ni miongoni mwa harakati ambazo zinakuwa na taathira kubwa zaidi kadiri siku na miaka inavyopita. Japokuwa zimepita karne nyingi sasa tangu baada ya tukio la Ashura lakini tukio hilo halikubakia katika jografia, eneo na zama zake, bali limeendelea kuwa nuru na tochi iliyoendelea kuangazia historia ya mwanadamu na kuwa na taathira kubwa kama jua. Kiongozi wa mapambano ya uhuru wa India Mahatma Gandhi aliwazindua watu wa taifa lake akiwaambia kwamba njia pekee ya kushinda wakoloni na dhulma ni kufuata nyayo za Hussein bin Ali (as). Akisema: "Sikuwaletea jambo jipya wananchi wa India. Nilichoiletea India ni matokeo ya uchunguzi na utafiti wangu kuhusu historia ya maisha ya mashujaa wa Karbala. Iwapo tunataka kuikomboa India tunapaswa kupita katika njia iliyotumiwa na Husssein bin Ali." Mwisho wa kunukuu.

Ufafanuzi

KUZALIWA KWA MTUME (S.A.W.W)

KUZALIWA KWA MTUME (S.A.W.W) KUZALIWA KWA MTUME (S.A.W.W) Kuzaliwa kwa Nabii Muhammad kuliandamana na miujiza mingi ikiwemo ya kusambaratika kwa nguzo za dhulma na kuzimika moto wa Fars. Nabii Muhammad ambaye jina lake lina maana ya aliyesifiwa, ni mtume wa mwisho kati ya mitume wote waliotumwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumuongoza mwanadamu katika njia nyoofu kuelekea ufanisi na saada ya milele. Tunawapongeza wapenda haki na Waislamu wote duniani dunia kwa mnasaba huu adhimu wa kuzaliwa Mtume Mhammad (SAW) pamoja na mjukuu wake Imam Swadiq (AS). Kuzaliwa kwa Nabii Muhammad kuliandamana na miujiza mingi ikiwemo ya kusambaratika kwa nguzo za dhulma na kuzimika moto wa Fars. Nabii Muhammad ambaye jina lake lina maana ya aliyesifiwa, ni mtume wa mwisho kati ya mitume wote waliotumwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumuongoza mwanadamu katika njia nyoofu kuelekea ufanisi na saada ya milele. Huyu ni Mtume ambaye alikuwa na siri zote za kuumbwa dunia kwenye kifua chake na kuziongoza nyoyo zilizojaa chuki kwenye njia ya haki na ukweli. Mwenyezi Mungu anasema hivi kuhusiana na Mtukufu huyo: "Amekufikieni Mtume aliye jinsi moja na nyiye, yanamhuzunisha yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni. (Na) kwa walioamini ni mpole na mrehemevu (kabisa) (Tauba 9-128)." Pia amesema: "(Alikuwa) mwenye kuzishukuru neema Zake (Mwenyezi Mungu zilizo juu yake), aka chagua na kumwongoza kwenye njia iliyonyooka (16-121)."

Ufafanuzi

SERIKALI YA MTUE (S.A.W.W)

SERIKALI YA MTUE (S.A.W.W) SERIKALI YA MTUE (S.A.W.W) Ushahidi na nyaraka za historia za kabla ya kudhihiri Uislamu zinaonyesha kuwa hakukuwepo utawala na serikali katika ardhi ya Hijaz na kwamba maisha ya Waarabu wa jangwani hayakutawaliwa na mfumo makhsusi wa kisiasa. Ni baada ya kudhihiri dini ya Uislamu huko Makka na kuhamia Mtume Muhammad katika mji wa Madina ndipo mtukufu huyo alipoanzisha serikali kuu na kubadili mfumo wa kikabila uliokuwa ukitawala kwa kuasisi mfumo mpya wa kisiasa na kijamii. Mbali na kutoa mafunzo na malezi kwa jamii ya watu wa Hijaz, Mtume Muhammad (saw) pia aliongoza yeye binafsi jamii changa ya Kiislamu na kushika hatamu za mfumo wa kijamii wa Waislamu katika nyanja mbalimbali za sheria, utamaduni, siasa, masuala ya kijeshi na kiuchumi.(2) Suala hilo linaonekana wazi zaidi katika mtazamo wa aya za Qur'ani na ushahidi wa kihistoria kiasi kwamba hata wataalamu wa masuala ya Mashariki (orientalist) wasiokuwa Waislamu wamelifafanua kwa uwazi zaidi. Msomi wa Kitaliano Fel Lino anasema: Mtume Muhammad (saw) aliasisi dini na dola kwa pamoja na masuala yote hayo mawili yalipanuka na kukuwa sambamba katika kipindi cha uhai wake.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini