Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAKALA MBALIMBALI

SIKU YA MUBAHALA

SIKU YA MUBAHALA

SIKU YA MUBAHALA MAANA YA MUBAHALA Mubahala Ni: Kuapizana Ujumbe wa Kikristo kutoka Najran ulifika kwa Mtume kujadili suala la Nabii Isa (a.s). Mtume aliwajulisha kuwa: إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ  خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٥٩﴾ "Hakika mfano wa Isa (a.s) mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliumbwa kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa naye akawa." 3:59. Kwakuwa Nabii Isa alizaliwa bila baba, Wakristo wamedhani kuwa baba yake ni Mwenyezi Mungu. Aya hii inaondoa dhana hiyo ambayo inapingana na utukufu wa Mwenyezi Mungu, na inawapigia mfano wa ajabu zaidi katika kuumbwa Adam bila ya baba wala mama. Aliumbwa kwa udongo kisha akaambiwa: kuwa naye akawa, na kwa neno hilo hilo Nabii Isa (a.s) ndivyo alivyoumbwa. Ujumbe huo ulipokuwa haukukubaliana na hoja hii, Mwenyezi Mungu akateremsha Aya: "Na atakayehojiana nawe (Muhammad) katika hili baada ya ujuzi uliokufikia, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafis zenu, kisha tuombe kwa kunyenyekea tuijaalie laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo." 3:61.

Ufafanuzi

VISA VYA KWELI NO.2

VISA VYA KWELI NO.2 VISA VYA KWELI Katika sehemu nyingi ndani ya Qur’ani, hadithi za mitume wafalme wa mataifa zimetajwa. Kwa kuongezea Mwenyezi Mungu amezungumzia masuala yanayohusiana na vita, amani, familia, dini, jamii na mada nyinginezo, katika muundo wa hadithi na masimulizi. Kwa kuvisoma visa hivi, watu wanaweza kuelewa na kutofautisha kati ya njia ya maendeleo na ile ya kuporomoka kwa maendeleo, na kupanda na kushuka katika kila kipengele, hususani maadili. Suratul Yusuf yote imetumika kusimulia kisa cha Yusuf, Yaqub, Zulekha na nduguze. Mwanzoni mwa sura Mwenyezi Mungu anasema: “Tunakusimulia (Ewe Mtume) masimulizi bora kabisa kwa (kupitia) yale tuliyokufunulia katika Qur’ani hii. (Suratul Yusuf; 12:13) Ambapo katika aya ya mwisho sura hii, anasema katika historia yao “kwa hakika kuna mazingatio kwa watu wenye akili.” (Suratul Yusuf 12: 111). Kwa hakika moja ya ustadi mkubwa kabisa wa Qur’ani ni hadithi hii ya Yusuf (as) iliyotajwa kuwa ni “simulizi bora kabisa” na mwisho (Qur’ani) inase- ma: “katika hadithi hizi kuna mazingatio kwa wale wanaotaka kuadilika na kufuata njia ya watu watimilifu. Juu ya hili Amirul Muuminina (as) katika Nahjul Balaghah, anamuambia mwanawe Imam Hasan (as): “Ingawa sijafikia umri ule uliofikiwa na wa kabla yangu, nimezitazama tabia zao na nimetafakari matukio ya maisha yao. Nilitembea katika maanguko yao mpaka nikawa miongoni mwao. Kwa kweli, kwa wema wa mambo yao niliyo (bahatika) kujua, ni kama nimeishi nao mwanzo hadi mwisho. Hivyo nimeweza kubaini kilicho kichafu na kisafi na chenye manufa na chenye madhara. Nimekuchagulia bora kabisa ya mambo hayo na nimekukusanyia nukta nzuri huku nikiyaacha yale yasiyo kuwa na manufaa.” Ili kufaidika zaidi ungana name katika Msururu wa Makala hizi zenye anuani ya: VISA VYA KWELI mpaka tamati.

Ufafanuzi

VISA VYA KWELI NO.1

VISA VYA KWELI NO.1 VISA VYA KWELI Katika sehemu nyingi ndani ya Qur’ani, hadithi za mitume wafalme wa mataifa zimetajwa. Kwa kuongezea Mwenyezi Mungu amezungumzia masuala yanayohusiana na vita, amani, familia, dini, jamii na mada nyinginezo, katika muundo wa hadithi na masimulizi. Kwa kuvisoma visa hivi, watu wanaweza kuelewa na kutofautisha kati ya njia ya maendeleo na ile ya kuporomoka kwa maendeleo, na kupanda na kushuka katika kila kipengele, hususani maadili. Suratul Yusuf yote imetumika kusimulia kisa cha Yusuf, Yaqub, Zulekha na nduguze. Mwanzoni mwa sura Mwenyezi Mungu anasema: “Tunakusimulia (Ewe Mtume) masimulizi bora kabisa kwa (kupitia) yale tuliyokufunulia katika Qur’ani hii. (Suratul Yusuf; 12:13) Ambapo katika aya ya mwisho sura hii, anasema katika historia yao “kwa hakika kuna mazingatio kwa watu wenye akili.” ( Suratul Yusuf 12: 111). Kwa hakika moja ya ustadi mkubwa kabisa wa Qur’ani ni hadithi hii ya Yusuf (as) iliyotajwa kuwa ni “simulizi bora kabisa” na mwisho (Qur’ani) inase- ma: “katika hadithi hizi kuna mazingatio kwa wale wanaotaka kuadilika na kufuata njia ya watu watimilifu. Juu ya hili Amirul Muuminina (as) katika Nahjul Balaghah , anamuambia mwanawe Imam Hasan (as): “Ingawa sijafikia umri ule uliofikiwa na wa kabla yangu, nimezitazama tabia zao na nimetafakari matukio ya maisha yao. Nilitembea katika maanguko yao mpaka nikawa miongoni mwao. Kwa kweli, kwa wema wa mambo yao niliyo (bahatika) kujua, ni kama nimeishi nao mwanzo hadi mwisho. Hivyo nimeweza kubaini kilicho kichafu na kisafi na chenye manufa na chenye madhara. Nimekuchagulia bora kabisa ya mambo hayo na nimekukusanyia nukta nzuri huku nikiyaacha yale yasiyo kuwa na manufaa.” Ili kufaidika zaidi ungana name katika Msururu wa Makala hizi zenye anuani ya: VISA VYA KWELI mpaka tamati.

Ufafanuzi

TAWASSULI (SEHEMU YA TATU)

TAWASSULI (SEHEMU YA TATU) TAWASSULI (SEHEMU YA TATU) UTANGULIZI Hakika Tawassul uhalisi wake umeelezwa na Qura’ni tukufu pindi Mwenyezi Mungu alipowaambia waumini: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {35} “Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na tafuteni njia ya kum- fikia. Na piganeni kwa ajili ya dini yake ili mpate kufaulu.” Al-Maida: 35. Hakika Aya hii tukufu imehesabu Uchamungu na Jihadi kuwa ni miongo- ni mwa njia za kisheria ambazo mwanadamu anaweza kuzifanya sababu ya kumfikia Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na je, kuna njia nyingine ambazo zimehimizwa na Sheria? Au jambo hili ameachiwa mwanadamu na kwa uwezo wake agundue njia nyingine za kumkurubisha kwa Mwenyezi Mungu? Ni wazi kuwa njia ambazo mja anaweza kujikurubisha kwazo kwa Mwenyezi Mungu hazitokani na Juhudi za kielimu, kwani kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na njia za kupatikana ukuruba huo zinahitaji mwongozo wa Mwenyezi Mungu. Na hapo ndipo Sheria ilipochukua jukumu la kuzibainisha, ikazitolea maelezo na kuziwekea mipaka ndani ya Kitabu na Sunna tukufu. Kila njia isiyokuwa ile iliyoelezwa na Sheria kwa namna ya pekee au ya mjumuisho, basi yenyewe ni aina moja ya bidaa na upotovu. Imam Ali bin Abu Twalib amegusia njia ambazo kwazo mja atajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, akasema: “Hakika njia bora ya kupita wenye kwenda kwa Mwenyezi Mungu ni: Kumwamini Yeye na Mtume wake na Jihadi katika njia yake, hakika yenyewe ndio heshima ya Uislamu. Na Tamko la dhati, hakika lenyewe ndio silika. Na kusimamisha Swala, haki- ka yenyewe ndio dini. Na kutoa Zaka, hakika yenyewe ni faradhi. Na Funga ya Ramadhani, hakika yenyewe ni ngome dhidi ya adhabu. Na Kuhiji Nyumba tukufu na kufanyia Umra, hakika hivyo viwili vinaondoa ufakiri na kuondoa dhambi. Na kuunga undugu wa damu, hakika kwenyewe ni ongezeko la utajiri katika mali. Na Sadaka ya wazi, hakika yenyewe inaepusha kifo kibaya. Na kutenda wema, hakika wenyewe unazuia kushindwa kwa udhalili.

Ufafanuzi

TAWASSULI (SEHEMU YA PILI)

TAWASSULI (SEHEMU YA PILI) TAWASSULI (SEHEMU YA PILI) UTANGULIZI Hakika Tawassul uhalisi wake umeelezwa na Qura’ni tukufu pindi Mwenyezi Mungu alipowaambia waumini: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {35} “Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na tafuteni njia ya kum- fikia. Na piganeni kwa ajili ya dini yake ili mpate kufaulu.” Al-Maida: 35. Hakika Aya hii tukufu imehesabu Uchamungu na Jihadi kuwa ni miongo- ni mwa njia za kisheria ambazo mwanadamu anaweza kuzifanya sababu ya kumfikia Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na je, kuna njia nyingine ambazo zimehimizwa na Sheria? Au jambo hili ameachiwa mwanadamu na kwa uwezo wake agundue njia nyingine za kumkurubisha kwa Mwenyezi Mungu? Ni wazi kuwa njia ambazo mja anaweza kujikurubisha kwazo kwa Mwenyezi Mungu hazitokani na Juhudi za kielimu, kwani kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na njia za kupatikana ukuruba huo zinahitaji mwongozo wa Mwenyezi Mungu. Na hapo ndipo Sheria ilipochukua jukumu la kuzibainisha, ikazitolea maelezo na kuziwekea mipaka ndani ya Kitabu na Sunna tukufu. Kila njia isiyokuwa ile iliyoelezwa na Sheria kwa namna ya pekee au ya mjumuisho, basi yenyewe ni aina moja ya bidaa na upotovu. Imam Ali bin Abu Twalib amegusia njia ambazo kwazo mja atajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, akasema: “Hakika njia bora ya kupita wenye kwenda kwa Mwenyezi Mungu ni: Kumwamini Yeye na Mtume wake na Jihadi katika njia yake, hakika yenyewe ndio heshima ya Uislamu. Na Tamko la dhati, hakika lenyewe ndio silika. Na kusimamisha Swala, haki- ka yenyewe ndio dini. Na kutoa Zaka, hakika yenyewe ni faradhi. Na Funga ya Ramadhani, hakika yenyewe ni ngome dhidi ya adhabu. Na Kuhiji Nyumba tukufu na kufanyia Umra, hakika hivyo viwili vinaondoa ufakiri na kuondoa dhambi. Na kuunga undugu wa damu, hakika kwenyewe ni ongezeko la utajiri katika mali. Na Sadaka ya wazi, hakika yenyewe inaepusha kifo kibaya. Na kutenda wema, hakika wenyewe unazuia kushindwa kwa udhalili.

Ufafanuzi

TAWASSULI (SEHEMU YA KWANZA)

TAWASSULI (SEHEMU YA KWANZA) TAWASSULI (SEHEMU YA KWANZA) UTANGULIZI Hakika Tawassul uhalisi wake umeelezwa na Qura’ni tukufu pindi Mwenyezi Mungu alipowaambia waumini: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {35} “Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na tafuteni njia ya kum- fikia. Na piganeni kwa ajili ya dini yake ili mpate kufaulu.” Al-Maida: 35. Hakika Aya hii tukufu imehesabu Uchamungu na Jihadi kuwa ni miongo- ni mwa njia za kisheria ambazo mwanadamu anaweza kuzifanya sababu ya kumfikia Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na je, kuna njia nyingine ambazo zimehimizwa na Sheria? Au jambo hili ameachiwa mwanadamu na kwa uwezo wake agundue njia nyingine za kumkurubisha kwa Mwenyezi Mungu? Ni wazi kuwa njia ambazo mja anaweza kujikurubisha kwazo kwa Mwenyezi Mungu hazitokani na Juhudi za kielimu, kwani kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na njia za kupatikana ukuruba huo zinahitaji mwongozo wa Mwenyezi Mungu. Na hapo ndipo Sheria ilipochukua jukumu la kuzibainisha, ikazitolea maelezo na kuziwekea mipaka ndani ya Kitabu na Sunna tukufu. Kila njia isiyokuwa ile iliyoelezwa na Sheria kwa namna ya pekee au ya mjumuisho, basi yenyewe ni aina moja ya bidaa na upotovu. Imam Ali bin Abu Twalib amegusia njia ambazo kwazo mja atajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, akasema: “Hakika njia bora ya kupita wenye kwenda kwa Mwenyezi Mungu ni: Kumwamini Yeye na Mtume wake na Jihadi katika njia yake, hakika yenyewe ndio heshima ya Uislamu. Na Tamko la dhati, hakika lenyewe ndio silika. Na kusimamisha Swala, haki- ka yenyewe ndio dini. Na kutoa Zaka, hakika yenyewe ni faradhi. Na Funga ya Ramadhani, hakika yenyewe ni ngome dhidi ya adhabu. Na Kuhiji Nyumba tukufu na kufanyia Umra, hakika hivyo viwili vinaondoa ufakiri na kuondoa dhambi. Na kuunga undugu wa damu, hakika kwenyewe ni ongezeko la utajiri katika mali. Na Sadaka ya wazi, hakika yenyewe inaepusha kifo kibaya. Na kutenda wema, hakika wenyewe unazuia kushindwa kwa udhalili.”1

Ufafanuzi

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 6

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 6 UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 6 AYA YA UDHU NI AYA MUHKAMAH Waislamu wameafikiana kwa mujibu wa na Kitabu kitukufu kuwa Swala haiwi sahihi isipokuwa kwa tohara, nayo ni: Wudhu, Josho, na Tayammum, na Allah (s.w.t.) amebainisha siri ya taklifu ni kwakuipata tohara kabla ya Swala kwa kauli yake: (Mwenyezi Mungu hataki kuwafanyiyeni ugumu, lakini anataka kuwatoharisheni). Udhu katika sheria ya kiislamu umepata umuhimu mkubwa kama ambavyo Qur’an na Sunna vimetamka. Amesema Mtume (s.a.w.w.): (Hapana Swala ila kwa tohara), na katika maneno yake mengine: (Wudhu ni sehemu ya imani) (Al’wasaailu, Juz.1, mlango wa kwanza miongoni mwa milango ya Wudhu). Ikiwa hii ndio nafasi ya Wudhu basi ni wajibu kwa Muislamu kuzitambua sehemu zake, na sharti zake, na vitanguzi vyake na vibatilisho vyake. Vitabu vya Fiq’h vimebainisha umuhimu huu. Ambalo twalitilia mkazo hapa ni kubainisha lile ambalo neno la wanavyuoni limehitilafiana kwalo.Naikusudia hukumu ya miguu upande wa kuosha au kupaka, hivi basi twasema: Mungu Mtukufu amesema ndani ya Kitabu chake kitukufu akibainisha wajibu wa wudhu na jinsi yake kwa kauli yake.

Ufafanuzi

UHURU WA KIJAMII WA MWANAMKE

UHURU WA KIJAMII WA MWANAMKE UHURU WA KIJAMII WA MWANAMKE UHURU WA KUJICHAGULIA MAJALIWA YAKE Katika kipindi cha kabla ya Uislamu, Uarabuni kulikuwa na aina ya ndoa iliyokuwa ikipendwa ikijulikana kama ndoa ya Shighar (kubadilishana mabinti) ambayo ilikuwa ni dhihirisho la mamlaka yasiyo na kikomo ya akina baba juu ya binti zao. Mwanaume alikuwa akimuoza binti yake kwa mwanaume mwingine kwa matarajio ya yeye pia kupewa binti wa huyo mwanaume kama mke. Katika ndoa za aina hii, hakuna mke yeyote katika hawa wawili aliyepata mahari. Uislamu ulipiga marufuku ndoa za aina hii. Inafaa kuzingatiwa kuwa Mtume (s.a.w.w.) alimpa uhuru kamili binti yake Fatimah Zahra (a.s) katika kuchagua mume. Aliwaoza pia binti zake wengine wengi, lakini hakuwanyima uhuru wao. Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alimwendea Mtume (s.a.w.w) na kueleza nia yake ya kumposa Fatima (a.s), Mtume alisema wanaume wengi walimwendea Mtume, na yeye akafikisha ujumbe kwa Fatimah, lakini aligeuza uso wake pembeni, kama ishara ya kukataa. Mtume alimhakikishia Ali kuwa angefikisha ujumbe wake pia. Mtume alikwenda kwa Fatimah na kumweleza binti yake mpendwa alichotaka Ali. Safari hii hakugeuza uso wake, lakini alinyamaza kimya na hivyo alielezea ridhaa yake. Mtume alipotoka nje, alikuwa na furaha, akasema, “Mungu ni Mkubwa!” HARAKATI ZA KIISLAMU JUU YA HAKI ZA WANAWAKE Uislamu umewafanyia wanawake mambo makubwa. Sio tu kwamba ulikomesha udhibiti usio na mipaka wa akina baba, lakini pia uliwapa wanawake uhuru, haiba na uhuru wa kufikiri na kutoa maoni. Uislamu kirasmi kabisa ulizitambua haki zake za asili. Hata hivyo, kuna tofauti mbili za msingi kati ya hatua zilizochukuliwa na Uislamu na kile kinachotokea katika nchi za Magharibi na zinazofuatwa na wengine. Tofauti ya kwanza inahusiana na saikolojia ya mwanaume na mwanamke. Uislamu umefanya na kufunua maajabu katika hili. Tutalijadili hili baadaye katika sura zinazofuatia. Tofauti ya pili ni kuwa, japo Uislamu uliwafanya wanawake wazijue haki zao na ukawapa utambulisho, haiba na uhuru, haukuwachochea kuasi na kuwafanyia uovu wanaume zao. Harakati za Kiislamu, za ukombozi wa wanawake zilikuwa nyeupe. Hazikuwa nyeusi wala nyekundu, hazikuwa bluu wala urujuani. Hazikukomesha heshima ya mabinti waliyokuwa nayo kwa baba zao wala ya wake kwa waume zao. Hazikuvuruga msingi wa maisha ya familia na hazikuwafanya wanawake wayatilie mashaka majukumu yao kwa baba zao na waume zao. Hazikutoa mwanga kwa wanaume ambao hawajaoa ambao mara zote huwa wanatafuta mwanya wa kuwalaghai wanawake.

Ufafanuzi

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 7)

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 7) DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 7) اللّهُمَّ رُدَّ كُلَّ غَرِيبٍ Ewe Mola Mrudishe Kila Alie Mgeni MAANA YA ‘GHARIIB’ Kutokana na ujuzi mdogo wa baadhi ya tamaduni na lugha, baadhi yetu tunadhani kwamba neno ‘Ghariib’ lina maana ya ‘maskini’. Kwa mfano neno hili kwa ki-Urdu lina tumiwa kuonyesha umasikini wa mtu, lakini linapo tumiwa kwa maana makhsusi, kama vile ‘Gharibul watan’ lina kuwa na maana nyingine. Kwa kiarabu ambayo ndio lugha ya asili ya neno lenyewe, ‘lina maana ya kitu kilicho mbali’. Kwa hivyo kitu chochote kilicho ghariib, kiko mbali. Seyyid Ali al-Madani al Husayni katika ufafanuzi wake wa Sahifatul Sajjādiyya anasema: الْغُرْبَةُ بالضمّ البَّعْدُ و الَنَّوَى “Ghurba (yenye irabu ya dhumma juu ya ghayn) ina maana ya ‘mbali’ na masafa”.1 Kwa hiyo, Ghariib ni kitu chochote ambacho kiko mbali [katika kuhusiana na kitu kingine cho chote]. Katika lugha ya kiarabu, maneno yasiyojulikana vile vile hujulikana kama ghariib. UFAFANUZI Uchungu unaompata mtu alie mgeni unajulikana vizuri kwa yule ambaye amepitia hali hii au yuko katika hali hii.Yeyote anayekwenda nchi ya kigeni ana matarajio ya kurejea nyumbani akiwa salama na mzima. Na bila ya shaka hangelipenda kutengana na watu wake wa karibu au kuviacha vitu vyake anavyo vihitajia katika maisha.Wale ambao wameacha miji yao na wakakumbwa na misukosuko wakiwa njiani au wamekwama katika nchi nyingine, wanafahamu shida iliyoko ya kuwa mbali na nyumbani. Historia ya miaka ya hivi karibuni imejaa mifano inayo vunja moyo ya kila msikilizaji mwenye kuhusika. Mazayuni kama walivyo kuwa katika miaka iliyoipita, wanaendelea kuzitesa sehemu mbali mbali za mataifa dhaifu ulimwenguni kwa kuzifanyia ugaidi na kuzihamisha, na hivyo basi kuwatoa wengi wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto katika miji yao, ili wapate uchungu wa mateso katika makambi ya wakimbizi. Watu kama hawa ambao hawana hatia, wanahitajia msaada wetu. Na kama tulivyo taja pale mwanzo, tuna wajibika kuziangalia sehemu ambazo tunaweza kutoa michango yetu ipasavyo kuhusiana na jambo hili na tuwasaidia kwa vyovyote vile iwezekanavyo. Kwa mfano, ikiwa kuna michango inayotolewa kupitia kwa vyama vya kutoa misaada vinavyo aminika, tujaribu tutoe michango yetu kwa wingi iwezakanvyo. Na ikiwa tunaweza tumsaidie ili aweze kuyazoea maisha mapya ambayo amelazimika kuwa ndani yake. Na ikiwa hatuna uwezo wa kuyafanya haya yote, basi tusisahau kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awasahilishie yanayo wakabili na awape utulivu.

Ufafanuzi

HESHIMA YA RAMADHANI

HESHIMA YA RAMADHANI HESHIMA YA RAMADHANI "Mwezi wa Ramadhani ni ambao imeteremshwa ndani yake Qur'ani kuwa mwongozo kwa watu..." (Qur'ani: 2:185) Waislamu kote ulimwenguni hufunga mwezi ambao ni mwema kuliko miezi yote, ulio na masiku bora kuliko masiku yote, wenye masaa ya baraka kuliko masaa yote na amali zifanyikazo katika mwezi huo ni makbuli kuliko baki ya maombi. Nao ni mwezi wa Ramadhani. Mwezi huu wa Ramadhani ambao ni mwezi wa tisa wa miezi wa Kiislamu, ni mwezi wa pekee wa aina yake kwa utukufu. Ni mwezi wa kusameheana, kuombeana heri na hata kufanya ibada kwa wingi na kwa usahali kabisa. Mwezi huu una matukio mbali mbali ya kihistoria ambayo hayatasahaulika, na ambayo vile vile hupambanua wazi utukufu wake. Imam Ja'far As-sadiq (a.s.) alisema kutoka kwa Babuye, (Mtume s.a.w.) "Taurati ilishuka na kumfikia Nabii Musa (a.s.) tarehe 6 Ramadhani, nayo Injili iIiteremshiwa Nabii Isa (a.s.) tarehe 12 za Ramadhani, kadhalika Zaburi ya Nabii Daud (a.s.) iliteremshwa mnamo tarehe 18 za Ramadhani, vile vile Qur'ani Takatifu iliteremka katika usiku wa Laylatul Qadri ambao kwa kawaida huwa katika mwezi huu wa Ramadhani."

Ufafanuzi

FAIDA ZA SAUMU

FAIDA ZA SAUMU FAIDA ZA SAUMU Limekuwa jambo jema kueleza faida za Saumu ili kila afungaye ajuwe hasa masumbuko yake ni kwa sababu gani? Kwani si vyema mtu kutaabika na hali hajui matokeo ya shughuli zake, na pengine huenda akaingia katika kundi la wale waliotajwa na mshairi mmoja kwamba: Mfisada mkubwa ni mjuzi mwenye kupotosha (bila kujua) na aliye muovu zaidi ni mjinga mwenye (kupenda) ibada. Hao watu wa aina mbili hizi ni fitina kubwa kwa watu na hasa kwa mtu aliyeshikamana na dini kwa kuwafuata. Jee, vipi utamfuata mtu ambaye hajui? Mshairi mwengine amenena: Ewe mtu (mjinga) unayemfundisha mwenzako, jee wewe nafsi yako unajua unachofundisha? Wampa dawa mtu aliyokonda na mwenye maradhi ili apone (kwa hizo dawa) na hali wewe ni mgonjwa?" Faida za kufunga ni nyingi sana tena mno, miongoni mwazo ni kutekeleza mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu Alizotufaradhia kwetu sisi na faida ya utekelezaji huu ni kuingia peponi. Faida ya pili ya Saumu ni kujizoeza subira, yaani katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, mtu anajifunza jinsi ya kuweza kuvumilia na kustahamilia njaa, kiu, na kila matamanio ya kimwili. Mtume (s.a.w) amenena: "Huo mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kusubiri, na hakika subira malipo yake ni pepo tu". Faida ya tatu ni kuwa na uadilifu na kujifundisha usawa baina ya tajiri na maskini. Imam Ja'far As-sadiq (a.s.) alisema: "Hakika si jingine, Mwenyezi Mungu amefaradhisha kufunga ili wapate kulingana tajiri na maskini (katika shida ya njaa na kiu) basi akapenda viumbe vyake wawe sawa, na Amwonjeshe tajiri maumivu ya kushikwa na njaa ili apate kumhurumia mnyonge, na apate kumsikitikia mwene njaa". Faida ya nne na ambayo ni muhimu zaidi ni kughufiriwa katika mwezi huu na kusamehewa madhambi yote ya mwaka ikiwa mwenye kufunga ameyafuata masharti yote na kufunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mtume (s.a.w) katika mojawapo ya hotuba alizozitoa kwa minajili ya mwezi huu akasema: "Enyi watu! Hakika umewaelekeni nyinyi, mwezi wa Mwenyezi Mungu (mwezi wa Ramadhani) kwa baraka, rehema na msamaha. Mwezi ambao ni bora mbele ya Mwenyezi mungu kuliko miezi yote, na siku zake ni bora kuliko siku zote, na masiku yake ni bora kuliko masiku mengine yote na masaa yake ni bora na muhimu kuliko masaa yote."

Ufafanuzi

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 6)

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 6) DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 6) اللّهُمَّ فَرِّجْ عَنْ كُلِّ مَكْرُوبٍ Ewe Mola Mfariji Kila Mwenye Huzuni MAANA YA ‘MAKRŪB’ Neno ‘Makrūb’ ni shamirisho ya jina ambalo asili yake ni kitenzi cha jina ‘karb’ lenye maana ya ‘huzuni nyingi’. Allāma Tabātabā’i katika kitabu chake ‘al-Mizān’, anamnukuu Sheikh Rāghib Isfahāni, Mtaalamu mashuhuri wa kuandika kamusi ya maneno ya Qur’an, akisema ya kwamba: الْكَرْبُ الغَمُّ الشَّدِيْدُ “Karb maana yake ni ‘huzuni kubwa”.1 Neno ‘karbala’ kwa mfano, limejengeka kutokana na neno (Karb) huzuni na majonzi na (balā) mtihani. Hivyo basi kwa ufupi, Makruub,’ ni mtu ambaye ana huzuni nyingi na majonzi. CHANZO CHA HUZUNI Katika sehemu hii ya dua, tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Kwa unyenyekevu awaondolee wote hali ya kuwa na ‘huzuni na majonzi’ wale wote walioko kwenye hali hii. Yeyote anayeomba kuondolewa kwa huzuni na majonzi anaomba pia kuondolewa kwa sababu ambazo pia husababisha huzuni. Hata hivyo ni lazima tuelewe kwamba, sababu za huzuni zinatafautiana kulingana na watu na mazingira tofauti. Kwa mfano, wale wenye ukaribu na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) japokuwa hawana huzuni kwa kuikosa dunia na starehe zake: أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ “Hakika marafiki (vipenzi) vya Allah hawaogopi wala hawahuzuniki” (Qur’an 10:62) Hupatwa na huzuni kwa yale yatakayo wafika makafiri katika siku za usoni (Allah anamwambia Mtume Wake): أَفَمَنْ زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ فَرَآهُ حَسَنًا ۖ فَإِنَّ اللَّهَ يُضِلُّ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ ۖ فَلَا تَذْهَبْ نَفْسُكَ عَلَيْهِمْ حَسَرَاتٍ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِمَا يَصْنَعُونَ “Basi roho yako isitoke kwa majonzi juu yao…”2 (Qur’an 35:8) Imam Khomeini (r.a.) katika kitabu chake maarufu kiitwacho ‘Hadithi al-Arbain’ anasema: “…Yeyote ambaye ameweza kutambua utukufu wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa kiwango kikubwa na akavijua vituo vitukufu vya Allah (s.w.t.) zaidi ya wengine, huwa anaumia zaidi na kuteseka kwa kiwango kikubwa sana kwa dhambi za viumbe na makosa yao dhidi ya utukufu wa Mwenye Mungu (s.w.t.). Vile vile, yule mwenye mapenzi na huruma kwa viumbe wa Mwenyezi Mungu huteseka kwa kiwango kikubwa mno kwa uhalifu wao na hali zao mbaya za kimaisha. Na bila ya shaka Mtume wa mwisho (s.a.w.w.) alikuwa amekamilika zaidi katika vituo vyote hivi na alikuwa juu kuwashinda Mitume wote na Mawalii kwa kiwango chake cha ukamilifu na ubora. Hivyo kuteseka kwake na kuhuzunika kwake kulikuwa kukubwa kuliko yeyote katika hao…” Wakati mwingine sababu ya huzuni huwa tofauti.

Ufafanuzi

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 5)

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 5) DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI (SEHEMU YA 5) اللّهُمَّ اقْضِ دَيْنَ كُلِّ مَدِينٍ Ewe Mola Mlipie Deni Kila Mwenye Kudaiwa MAANA PANA YA NENO ‘DENI’ Huenda wengi wakachukulia ya kwamba neno deni ni sawa na mkopo lakini katika sheria za kiislamu lina maana pana kushinda mkopo kwa kuwa mkopo ni sehemu ya deni. Āyatullāh Shirāzi katika kitabu chake cha ‘Tafsir-e-Nemūne’ amezungumzia jambo hili na akasema kwamba “Mkopo” hutumika mtu anapo lazimika kurudisha kilicho sawa na kilicho chukuliwa, kwa mfano kama atachukua pesa kwa njia ya mkopo atalazimika arejeshe kiasi hicho hicho na lau atachukua aina fulani ya chakula atalazimika arudishe aina hiyo hiyo. Hata hivyo dayn (deni) lina maana pana kwa kuwa linajumuisha aina yoyote ya shughuli, kama vile: kusuluhisha (sulh), mkataba wa kupangisha, (ijāra), kuuza na kununua na kadhalika.1 DENI WAKATI MWINGINE HUMZUIA MTU KUENDELEA KIROHO Deni wakati mwingine huwa ni kizuizi kikubwa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Sababu ya hili ni kwamba hushughulisha akili na moyo wa mtu, na kwamba ni kipengele cha wazi ambacho huzuia maendeleo. Tazama hadithi ifuatayo: 1. Imamu Zaynu’l ‘Abidin katika maombi yake ya kupendeza2 kwa ajili ya kuondokana na madeni anawajulisha wafuasi wake hali ngumu ambayo mdaiwa kwa kawaida huipata: Ewe Allah! Mbariki Muhammad na watu wa nyumbani kwake, na uniondolee deni ambalo huchusha uso wangu, huchanganya akili yangu, huvuruga mawazo yangu na hurefusha muda wangu kwa kulishughulikia! Naomba kinga Kwako, ewe Mola wangu, kutokana na wasiwasi na mawazo kuhusu deni, kutokana na uharibifu wa deni na kukosa usingizi; basi mbariki Muhammad na watu wa nyumbani kwake, na unipe kinga kutokana nalo! Naomba hifadhi Kwako, ewe Mola wangu, kutokana na udhalili wa deni katika maisha, na matokeo yake mabaya baada ya kufa…

Ufafanuzi

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 4

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 4 LENGO LA KUUMBWA MWANADAMU Msiba mkubwa wa maisha ya mwanadamu unatokana na kutofahamu madhumuni ya kuumbwa mwanadamu. Maadamu mwanadamu atakuwa hajui ‘lengo la maisha’ atakuwa daima kwenye matatizo. Kanuni hii inatumika kwa matajiri pia. Muulize kila tajiri iwapo pesa zake zinamfanya awe na furaha daima, bila shaka jawabu litakuwa ni la. Qur’an Tukufu na pia Ahlulbayt (a.s.) wametufahamisha kwamba makusudio ya lengo la kuumbwa kwa mwanadamu ni ili apate ujirani na ukaribu wa Mwenyezi Mungu. Na njia ya kumuongoza mtu kutambua hamu hii si nyingine bali ni ibada, kama ilivyoelezwa kwenya aya zifuatazo:- Katika sura ya 51 aya ya 56. Mwenyezi Mungu anasema ya kwamba: “Na sikuwaumba majini na wanaadamu ila waniabudu” Hapa lengo linaonyesha ya kuwa ni kumuabudu Mwenyezi Mungu. Lakini jee hili ndilo lengo la kipekee la kuumbwa kwa mwanadamu? Ili tuweze kulijibu swali hili, tunawajibika kuiangalia aya ya 99 katika sura ya 15, ya Qur’an, isemayo: “Na muabudu Mola wako mpaka ikufikie hiyo yakini” Kwa hivyo kitu cha mwisho ni kumjua Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na kila anapojikurubisha mtu kwa Mola wake ndivyo elimu kumhusu Muumba wake inavyoongezeka.

Ufafanuzi

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 3

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 3 DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 3 Moja ya falsafa za kufunga katika Mwezi wa Ramadhani ni kujizoesha njaa, na hivyo kufahamu hali ya wale ambao wana njaa na hawana uwezo wa kujitosheleza ipasavyo. Hadithi ifuatayo iliyonukuliwa na Faidh Maulā Kāshāni kutoka kwenye kitabu ‘Man lā yahdhuru’l Faqih’, inazungumzia jambo hili hili. Imām al-Sadiq (a.s.) katika hadithi iliyo sahihi, wakati anapoelezea falsafa ya kufunga anasema: “[Allah (s.w.t.) alitaka kufanya usawa baina ya viumbe vyake kwa kumuonjesha tajiri njaa na uchungu ili amuonee huruma alie dhaifu na amhurumie mwenye njaa.]”1 yanayo sababisha njaa Njaa ni tatizo lililo enea katika ulimwengu wa leo na kuna sababu mbalimbali ambazo zaweza kuainishwa katika (sababu) aina mbili: aina ya kwanza (ya sababu) zinamhusu mtu binafsi na aina ya pili (ya sababu) zinatokana na mambo ya nje. Chanzo cha sababu zinazomhumsu mtu mwenyewe, hutokana na muathiriwa mwenyewe, ambapo sababu za nje huanzia kwenye jamii na matukio asilia mengineyo. Aina hizi mbili za sababu hatuwezi kuzijadili kwa sasa kwa kuwa zitatutoa nje ya eneo la ufafanuzi huu mfupi. Hata hivyo ni muhimu kujifunza mipaka ya sababu hizi ili tujitahidi kujiepusha nazo au kuziondolea mbali kwa urahisi. Suala hili ambalo liko chini ya mjadala, kama linavyoweza kuonekana kwa uwazi, vile vile linauhusiano wa karibu na umaskini. Mwanzoni tulionyesha ukweli kwamba, kitu kinacho jitegemea husimama kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo ikiwa Mwenyezi Mungu hakutaka mtu apatwe au aathiriwe na msiba hakuna kitakacho mpata. Kanuni hii kama ilivyotajwa mwanzoni, sio tu inatajwa na ufunuo (wahyi), bali pia huthibitishwa na akili.

Ufafanuzi

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 2

DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 2 DU’A YA MWEZI WA RAMADHANI 2 Tunapomwomba Mwenyezi Mungu Awatajirishe maskini tunatakiwa kivitendo pia tuchukue hatua katika kuwatajirisha wengine kwa kiasi cha uwezo wetu. Jambo hili ni kwamba ndilo linalo tarajiwa kutoka kwetu kama tulivyo elezea hapo mwanzo. Tunapoangalia sehemu hii ya du’a kwa makini tunafahamu ya kwamba mwenye kuisoma hawaombei wanaohitajia waondolewe haja zao kwa mda mfupi, kama tufanyavyo wengi wetu tunapowasaidia wanaohitajia kwa kipindi kifupi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuwanunulia mahitaji yao ya nyumbani. Na tukafurahi kwa kuwa tumemfurahisha Mwenyezi Mungu kwa kitendo chetu hiki. Bila ya shaka ni kitendo kizuri, na kina thawabu nyingi, lakini ni tafauti na yale tunayo muomba Mwenyezi Mungu kwenye sehemu hii ya du’a kwa kuwa lengo letu siyo maskini watoshelezewe haja zao muda mfupi, bali tunamuomba Mwenyezi Mungu awasaidie kwa kuwapa njia ya kudumu ya mapato, yaani, “Ewe Mola mtajirishe kila aliye maskini.” Baada ya kuifahamu du’a hii, basi mwenye kusoma dua hii anatakiwa afikirie namna ya kutoa mchango wake katika kuwatajirisha maskini. Kwa mfano, yule mwenye mali anatakiwa angelifikiria namna ya kuwasaidia maskini ili wajianzishie biashara ndogondogo na kujitajirisha mwenyewe. Na yule mwenye biashara ndogo na anahitaji wafanyikazi angeliwaajiri maskini na awatajirishe kwa kiwango fulani. Na yule ambaye ni mwajiriwa, kutokana na kufahamiana kwake na matajiri angeliwaombea masikini kazi kwao. Wasomaji, linalohitajika hapa ni kufahamu mambo mbali mbali yanayo husiana na jambo hili tukufu. Na lililo muhimu hapa ni kwamba kila mtu achukue hatua kuhusiana na jambo hili.

Ufafanuzi

UTUKUFU WA RAMADHANI

UTUKUFU WA RAMADHANI  UTUKUFU WA RAMADHANI  “Enyi Mlioamini mmefaradhishiwa Saumu kama walivyofaradhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu”. (TMQ 2:183) Tunaweza kuugawa Utukufu wa Ramadhani katika sehemu mbili kubwa: 1.Utukufu wa ibada ya funga kwa ujumla  ndani  ya  Ramadhani au nje ya  Ramadhani. Na kwa kuwa ndani ya mwezi wa Ramadhani imo ibada ya funga, mfungaji  hana budi kufaidika na utukufu huo. 2.Utukufu  maalum  (khasa) wa funga ya Ramadhani na yote yaliyomo ndani yake UTUKUFU  JUMLA WA KUFUNGA SAUMU Amesema Mtume (SAAW):   akipokea  kutoka kwa  mola  wake “Kila Amali ya mwanadamu ni yake, isipokuwa Saumu, hiyo ni Yangu, na Mimi ndie Nitakayelipa”  (Bukhar) Amesema pia SAAW:  “Watu Watatu dua zao hazirejeshwi    Kiongozi muadilifu, aliyefunga mpaka kufuturu na dua ya mwenye kudhulumiwa” (Ibn Majah) Pia kasema SAAW: “Hakika katika pepo kuna mlango unaitwa Rayyan wataingia  mlango huo wafungaji na hatoingia mwengine yoyote kinyume na wao” (Bukhar) UTUKUFU  MALUMU (KHASA) WA RAMADHANI “Na mkifunga ni kheri kwenu ikiwa mnajua” (TMQ 2:184)  Kwa Aya hii Muumba wa kila kitu Anatangaza kwamba kufunga Ramadhani kuna kheri kwetu. Jee kuna kubwa kuliko kauli ya Allah Taala? Amesema Mtume SAAW: “Swala tano, ijumaa mpaka ijumaa  Ramadhani mpaka Ramadhani ni kafara (kifutio) cha madhambi atakapojiepusha mtu na madhambi makubwa/al-kabair” (Bukhari) Anasema (s.a.w.w) : “Amekula hasara mtu nitakapotajwa asiniswalie, na amekula hasara itakapoingia Ramadhani na ikaondoka hakusamehewa madhambi yake. Amesema tena SAAW: “Itakapoingia Ramadhani milango ya moto hufungwa, na hufunguliwa milango ya pepo, na hufungwa mashetani  (Bukhar) Amesema tena SAAW: “Atakaefunga kwa imani thabit na matarajio ya malipo  husamehewa  madhambi yaliyotangulia  (Bukhar) Kasema SAAW: Hakika imekufikieni funga ya Ramadhani, basi atakaefanya sunna ya kisimamo chake, atakaefunga na kusimama kwa ibada kwa  imani na matarajio ya malipo atafutiwa madhambi yake kama  siku alipozaliwa kutoka katika tumbo la mama yake (Nassai) Pia kasema SAAW: “Hakika  umekudhihirikieni mwezi wa Ramadhani ndani yake umo usiku mtukufu wa laylat-ul-qadr ambao ni bora kuliko miezi alfu.

Ufafanuzi

FADHILA ZA MWEZI WA RAMADHANI

FADHILA ZA MWEZI WA RAMADHANI FADHILA ZA MWEZI WA RAMADHANI Sifa njema zote Anastahiki Allaah Mola wa viumbe vyote na Swalah na salamu zimfikie Mtume wetu na kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na aali zake watoharifu. Ama kwa hakika katika mwezi wa Ramadhwaan kuna fadhila nyingi ambazo mimi nitazitaja kwa uchache, namuomba Allaah Aniwafiqishe 'asaa yawe na manufaa katika Duniya na Akhera. 1) MWEZI WA QUR-AAN Kama Alivyosema Allaah Mtukufu: "Mwezi wa Ramadhwaan ni mwezi ambao imeteremshwa Qur-aan ili iwe uongozi kwa watu na hoja na upambanuzi (Baina ya haki na batil)” [Qur-aan 2:185] Vilevile kama ilivyopokewa na Ibn 'Abbaas (radhiya Allaahu 'anhu) kuwa  makusudiyo yake   kwa hakika kuteremshiwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Qur-aan mwanzo ni katika mwezi wa Ramadhwaan na vilevile Qur-aan mwanzo wa kuteremka ni usiku wa Laylatul-Qadir na Laylatul-Qadir iko katika mwezi wa Ramadhwaan. Hivyo basi ni juu yetu kufanya juhudi katika mwezi huu kukithirisha sana kusoma Qur-aan.  Walikua Salafus-Swaalih (Wema Waliotangulia) wakikilinda kitabu cha Allaah kwa kukisoma na kuyafanyia kazi yaliyokuwemo kwa mazingatiyo. Pia Tunaambiwa kuwa Sayyidnaa Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) akimfundisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Qur-aan katika mwezi wa Ramadhwaan, na alikuwa 'Uthmaan bin 'Afaan (Radhiya Allaahu 'anhu)  kila siku akisoma Qur-aan yote yaani anakhitimisha mara moja kwa siku,  kwa maana,  msahafu mzima anausoma kwa siku moja. Na walikuwa baadhi yao katika wema wakisoma Qur-aan yote kwa siku tatu, wengine kwa wiki moja na wengine kwa siku kumi. Walikuwa wakisoma Qur-aan ndani ya Swalah na nje ya Swalah. Allaah Atuwafiqishe mimi na wewe tuisome Qur-aan na kwa mazingatio khasa katika mwezi huu tufanye juhudi sana ili tuweze kupata fadhila za mwezi huu mtukufu.

Ufafanuzi

RAMADHANI NA UTULIVU WA MOYO

RAMADHANI NA UTULIVU WA MOYO RAMADHANI NA UTULIVU WA MOYO Wataalamu wa masuala ya nafsi au wanasaikolojia wanasema: "Sisi wanaadamu katika uwepo wetu,  tuna uwezo mkubwa wa kupokea mapenzi na mahaba na iwapo moja ya hilo litatoweka, tutahisi tumekosa kitu na hivyo kuingiwa na wasiwasi. Nukta muhimu zaidi ya uwezo huu wa mahaba ni mapenzi kwa Mwenyezi Mungu ambayo hutupatia hisia chanya na utulivu. Kwa hakika utulivu ni nukta muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwa kadiri kwamba tunaweza kusema kuwa, sababu kuu ya jitihada za mwanadamu ni kufikia utulivu. Wengi hutafuta mali na utajiri ili wapate utulivu. Kwa mfano kununua nyumba au ardhi hufanyika kwa ajili ya kufikia utulivu. Wengi hutafuta maisha ya kifahari ili wapate utulivu na pia kuna wengi ambao humuabudu Mwenyezi Mungu ili waweze kupata utulivu. Lakini kati ya yote hayo tuliyoyataja ni lipi lenye kumletea mwanadamu utulivu wa kudumu?" Erich Seligmann Fromm, mwanasaikolojia wa Ujeurmani anaandika hivi : "Tujaalie kuwa, maisha ya kimaada na kuishi maisha bora ni mambo ambayo huandamana na furaha na utulivu.  Uzalisahji usio na mipaka , uhuru usio na mipaka na ustawi wa kustaajibisha ni mambo yanayoweza kuifanya dunia iwe ni pepo na kuifanya ichukue sehemu ya pepo iliyoahidiwa. Lakini ukweli ni kuwa, katika zama zetu hizi za kiviwanda, mwanadamu amegonga mwamba katika kufikia malengo yake makubwa, Mwanadamu ametambua kuwa, kupata anasa kupita kiasi hakuwezi kumdhaminia utulivu na furaha." Naye Albert Schweitze, tabibu Mjerumani ambaye mwaka 1952 alipata Tuzo ya Amani ya Nobel wakati alipokuwa akipokea zawadi hiyo aliwahutubu walimwengu kwa kusema: "Mwanadamu amekuwa mtu mwenye uwezo wa kupita kiasi. Lakini mtu huyu mwenye uwezo wa kupita kiasi hajaweza kufikia hekima na fikra ya juu. Kadiri ambavyo uwezo wa mwanadamu unavyozidi kuongozeka, anazidi kudhoofika na kudhoofika zaidi na hili ni jambo linalopaswa kututikisa nafsi zetu."

Ufafanuzi

MWALIKO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

MWALIKO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI MWALIKO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI Tuko katika siku tukufu za ibada ya funga ya mwezi wa Ramadhani na sote tumealikwa kuwa wageni wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mtu anapoalikwa kwenye karamu au shughuli yoyote ya ugeni, hali hiyo humsisimua na kumfanya awe ni mwenye furaha wakati wote hadi wakati wa kushiriki karamu au ugeni huo. Sote tunajua ya kwamba jambo linalomfanya mwalikwa kuwa na furaha hiyo ni ile hamu ya kutaka kukutana na mwenyeji wake pamoja na wageni wengine walioalikwa kwenye karamu hiyo ambapo mazingira mapya ya kuonana na kujuliana hali wageni hujitokeza, mapenzi na upendo kudhihirishwa na wakati mwingine zawadi kutolewa na mwenyeji wao. Kabla ya kushiriki kwenye mwaliko, jambo la kwanza ambalo mwalikwa hukabiliana nalo ni jinsi atakavyovalia vizuri, kutembea vizuri na kuzungumza vizuri. Tunapofahamu kuwa mwenyeji wetu atakuwa anatusubiri mlangoni kwa ajili ya kutulaki, hapo kasi ya hatua hatua zetu kumuelekea huongezeka. Mwanzo wa kila mwaliko huwa ni kuzingatia na kufungamana kimawazo na mwenyeji, ambapo kila mara mfungamano huo unapokuwa ni wa kirafiki zaidi, ugeni nao hunoga na kuvutia zaidi. Hivi sasa na kwa mara nyingine tumealikwa na mwenyeji ambaye ni rafiki mwema wa kuvutia, mwenye huruma na anayesamehe zaidi kati ya wenyeji wengine wote tunaowajua sisi wanadamu. Mwenyezi Mungu ni Muumba wa pekee na Mwenye Hekima ambaye jina lake hutuliza nyoyo zinazosononeka na kutaabika.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini