Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAKALA MBALIMBALI

UZAYUNI MELE YA WAYAHUDI

UZAYUNI MELE YA WAYAHUDI

UZAYUNI MELE YA WAYAHUDI Watu wengi ulimwenguni huenda wakadhani kwamba maneno “Uzayuni” na “Uyahudi” au “Uyuda” yana maana moja lakini ukweli wa mambo ni kuwa si hivyo hata kidogo. Wasomi na wataalamu wa Kizayuhudi ambao wanaelewa vyema mafundisho ya kitabu kitakatifu cha Mayahudi yaani Taurati au Torati wanasema kuwa, dhana na fikra kwamba maneno hayo yana maana moja haionekani kuwa ni sawa. Pamoja na kuwa Wazayuni hujihesabu kuwa ni miongoni mwa Mayahudi, lakini Mayahudi wengi hujiweka mbali na fikra za Uzayuni. Katika makala hii, tatajaribu kudurusu na kuchunguza maaoni na mitazamo ya wasomi wa Kiyahudi kutoka pembe tofauti za dunia kuhusiana na suala hili. Wakati huohuo, tutajaribu kuona ni jinsi gani utawala ghasibu wa Israel hutoa radiamali yake kuhusiana na maoni hayo na pia ni jinsi gani mitazamo hiyo iliyo dhidi ya Uzayuni huakisiwa katika vyombo vya habari vya kimataifa. Hata kama baadhi ya wasomi wa Kiyahudi wanaamini kwamba kuna uwezekano wa kiasisiwa dola la Kiyahudi, lakini wanasisitiza kwamba dola hilo lililoahidiwa si hili la hivi sasa la utawala ghasibu wa Israel lililoasisiwa kinyume cha sheria katika ardhi za Wapalestina. Shughuli za taasisi nyingi za Mayahudi zinaendeshwa kwa imani kwamba, taifa la Mayahudi halina haki yoyote ya kubuni dola hadi atakapokuja mwokozi wa dunia.

Ufafanuzi

HUDUMA ZA HOLLYWOOD

HUDUMA ZA HOLLYWOOD HUDUMA ZA HOLLYWOOD Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo amukutana na Mwendeshaji filamu na wasanii walioshiriki katika kutengeneza filamu ya Nabii Yusuf (as) akiwashukuru kwa kazi kubwa ya kisanii ya kutengeneza filamu hiyo. Ayatullah Khamenei amesema kuwa filamu hiyo kwa hakika ni mwanzo wa kazi za ubunifu wa kisanii kwa kutumia visa katika majmui ya sanaa za kimapinduzi. Amesisitiza kuwa Wizara ya Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu, Shirika la Utangazaji la Iran (IRIB) na wasanii wanapaswa kuwekeza zaidi katika medani hiyo. Amesema utumiaji wa sanaa katika kueleza kisa katika filamu ya Nabii Yusuf (as) ni moja ya sifa makhsusi za filamu hiyo ya televisheni. Ameongeza kuwa kwa kawaida katika dunia ya sasa, sanaa ya filamu inatumia baadhi ya masuala kama ngono kwa ajili ya kuwavutia watazamaji, lakini katika filamu hii ya mfululizo ambayo imewavutia watu wengi hapa nchini na katika nchi nyingine, kinyume na aghlabu ya filamu na michezo mingine, maudhui kuu ya kisa chake ilikuwa ni kujiepusha na dhambi na utakasifu wa nafsi.

Ufafanuzi

MCHANGO WA HIJA KATIKA SUALA LA UMOJA

MCHANGO WA HIJA KATIKA SUALA LA UMOJA MCHANGO WA HIJA KATIKA SUALA LA UMOJA Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa moja ya haja za dharura za kipindi cha sasa ni kutilia maanani umoja na mshikamano wa Kiislamu. Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo katika hadhara ya wafanyakazi wa sekta ya utamaduni na wasimamizi wa misafara ya hija ya mwaka huu ya Iran. Amesisitiza kuwa ibada ya hija inapaswa kuwa dhihirisho la azma kubwa ya umma wa Kiislamu mkabala wa hatua zozote za kuzusha mfarakano na zinazopinga umoja na maendeleo ya dunia ya Kiislamu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa hija ni fursa adhimu na yenye thamani kubwa na akaongeza kuwa fursa ya kuwa kando ya msikiti mtakatifu wa Makka, msikiti wa Mtume, haram za Maimamu watoharifu na masahaba wa Mtume inapaswa kutumiwa kwa ajili ya kuzidisha rasilimali ya imani, masuala ya kiroho na unyenyekevu mbele ya Mola Mlezi. Amesema kuwa mahujaji wanapaswa kuwa macho ili fursa hiyo ya thamani isitumike katika kazi zisizokuwa na thamani za kidunia.

Ufafanuzi

ATHARI YA UISLAMU NDANI YA UINGEREZA

ATHARI YA UISLAMU NDANI YA UINGEREZA ATHARI YA UISLAMU NDANI YA UINGEREZA Waziri wa Sheria wa Uingereza amesema kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamekuwa na athari kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba athari hizo pia zinaonekana miongoni mwa Waislamu wa Uingereza. Akizungumza katika mazungumzo ya meza duara yaliyokuwa yakijadili mchango wa Waislamu katika jamii ya Uingereza, Jack Straw amesema kuwa athari za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwishoni mwa muongo wa sabini zilihisika pia nchini Uingereza ambapo Waislamu wa nchi hiyo pia walijihisi kuwa na nguvu. Katika sehemu nyingine, Straw amesema kuwa Waislamu, Wakristo na Mayahudi wanapasa kuimarisha uhusiano wao na kwamba serikali ya London inapasa kusisitiza umuhimu wa suala hilo kupitia vyombo vya habari. Hata hivyo Straw amedai kwamba Uislamu umekuwa ukitumiwa vibaya na baadhi ya makundi ya kisiasa katika miongo ya hivi karibuni.

Ufafanuzi

SHEREHE ZA KRISMAS

SHEREHE ZA KRISMAS SHEREHE ZA KRISMAS Katika moja ya hotuba zake za swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Omar bin Khattab huko Doha nchini Qatar, Sheikh Yusuf Qardhawi amezungumzia masuala matatu muhimu yanayowahusu Waislamu. Ameanza kwa kuzungumzia kuenea kwa madhihirisho ya sherehe za Kikristo za Krismasi nchini Qatar na kukosoa vikali tabia ya Waislamu ya kujishughulisha na sherehe hizo zisizoambatana na utamaduni wa Kiislamu. Sheikh huyo amesikitishwa mno na tabia hiyo na kuuliza maswali mengi kwa kusema; Je, sisi tunaishi katika jamii ya Kiislamu au Kikristo? Ni sherehe gani hizi zinazofanyika katika mitaa na maduka kwa jina la sikukuu ya Kikristo au Krismasi, ni kana kwamba sisi tunaishi katika mojawapo ya nchi za Ulaya zinazofuata mafundisho ya Kikristo? Huku akiashiria kumalizika hivi karibuni tu kwa idi kubwa ya Waislamu ya Adh'ha, na kutofanyika sherehe kubwa kama hizo zinazoonekana hivi sasa za Krismasi nchini Qatar, Sheikh Yusuf Qardhawi ameashiria kuwepo hitilafu kubwa miongoni mwa Wakristo wenyewe kuhusiana na iwapo kweli Nabii Isah (as) au kwa jina jingine, Yesu, alizaliwa tarehe 25 Disemba au tarehe 7 Januari. Alisema hitilafu hizo pia zinahusiana na iwapo Yesu alizaliwa katika msimu wa joto au wa baridi. Hata hivyo ameashiria aya ya Qur'ani Tukufu kuhusiana na uzawa wa Isah Masih (as) na kusema kuwa kwa mujibu wa aya hiyo, mtukufu huyo alizaliwa katika msimu wa joto ambapo tende zilikuwa zikivunwa.

Ufafanuzi

KUYAHUDISHWA KWA AQSA

KUYAHUDISHWA KWA AQSA KUYAHUDISHWA KWA AQSA Viongozi wa Palestina wametahadharisha juu ya njama zinazofanywa na Wazayuni za kubomoa na kuharibu nyumba za Wapalestina katika mji unaoukaliwa kwa mabavu wa Quds kwa ajili ya kuufanya mji huo kuwa wa Kiyahudi. Kwa mujibu wa ripoti ya televisheni ya al-Alaam viongozi wa Palestina wanasema kuwa kitendo hicho ni sawa na kutangazwa vita, mauaji ya kizazi na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina. Wanasisitiza kwamba, siasa hizo za Wazayuni zinahatarisha kizazi kizima cha Wapalestina katika mji huo mtakatifu. Kuhusiana na suala hilo, Maad az-Zatari, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya al-Maqdis ameiambia televisheni ya al-Alaam kwamba, utawala wa Israel unatekeleza siasa za kubomoa na kuharibu nyumba za Wapalestina wanaoishi katika mji wa Quds ili kuwalazimisha kuondoka katika mji huo na hivyo kutoa fursa ya kufanywa kuwa wa Kiyahudi.

Ufafanuzi

UCHOCHEZI NA FITINA

UCHOCHEZI NA FITINA UCHOCHEZI NA FITINA Licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufanya juhudi za pande zote na pia wasomi na wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu kuchukua hatua muhimu za kuleta umoja miongoni mwa Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia, kwa bahati mbaya bado inasikika sauti ya fitina na mifarakano kutoka kwa baadhi ya watu na nchi zisizopenda kuona umoja na utulivu ukidumishwa katika umma wa Kiislamu. Bila shaka sauti hii haitakuwa na manufaa ila kwa maadui wa Uislamu. Ni wazi kuwa sauti hii ni hatari kubwa inayopasa kuleta muamko miongoni mwa Waislamu na kuwafanya waepuke kutumbukia kwenye shimo la fitina na mifarakano. Je, ni kwa hoja gani juhudi za miaka mingi za kuleta umoja na mshikamano kati ya Waislamu, zilizofanywa na wasomi pamoja na wanafikra wakubwa wa Kiislamu wakiwemo Sayyid Jamal, Sheikh Shaltut na Imam Khomeini zimechukuliwa kuwa mchezo na baadhi ya watu ambao wanajichukulia kuwa ndio walio kwenye njia ya haki na kuwatuhumu waumini kwa mambo yasiyo na msingi, bila ya kuwa na hoja yoyote ya maana? Ni wazi kuwa Mawahabi wa Saudi Arabia wameazimia kuwahudumia kwa nguvu zao zote maadui wa umoja wa Uislamu, na hakuna njia nyingine yoyote ya kufikia lengo hilo isipokuwa kuchochea fitina na mifarakano katika jamii ya Kiislamu.

Ufafanuzi

WAISLAMU NA UMOJA WAO

WAISLAMU NA UMOJA WAO WAISLAMU NA UMOJA WAO Kikao cha 23 cha kimataifa cha Umoja wa Kiislamu ambacho kinawashirikisha wasomi, wanafikra na wanazuoni wa Kiislamu wapatao 500 kutoka pembe mbalimbali za dunia kilicho anza Machi Pili mjini Tehran Iran na kuendelea hadi Alkhamisi Machi Nne, ikiwa ni katika siku za kuadhimisha Wiki ya Umoja wa Kiislamu. Kikao hicho kilifunguliwa rasmi kwa hotuba ya Ayatullah Hashimi Rafsanjani, Mkuu wa Majlisi ya Kumchagua Kiongozi Mkuu wa mfumo wa Kiislamu wa Iran ambaye pia ni Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu nchini Iran. Kikao hicho cha siku tatu ambacho kinawajumuisha wanafikra na wasomi wa Kiislamu kutoka humu nchini na pembe nyinginezo za dunia kitajadili masuala na changamoto mbalimbali zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu na hasa kuhusiana na suala la kuimarisha umoja na mshikamano kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu chini ya anwani isemayo: "Umma wa Kiislamu, Tokea Madhehebu Tofauti hadi Mielekeo ya Kimakundi."

Ufafanuzi

SABABU YA KUCHUKIWA UISLAMU NI UJAHILI

SABABU YA KUCHUKIWA UISLAMU NI UJAHILI SABABU YA KUCHUKIWA UISLAMU NI UJAHILI Rita De Milo, mhadhiri wa masuala ya utafiti wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Rome, mji mkuu wa Italia amesema kuwa ujahili wa wasiokuwa Waislamu na raia wengi wa nchi za Magharibi kuhusiana na Uislamu ni sababu kuu ya kuenea chuki yao dhidi ya Uislamu na hivyo kuwapelekea kuiogopa dini hii. Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharqul Ausat, Rida De Milo amesema kuwa Uislamu umebainisha vyema na kwa kina masuala mbalimbali yanayomuhusu mwanadamu, likiwemo suala la haki za binadamu na hasa haki za mwanamke. Amesisitiza kuwa hakuna taasisi wala dini nyingine ilivyobainisha vyema na kutetea haki za mwanamke kama ulivyofanya Uislamu. Amesema sheria za Kiislamu ni nguzo muhimu inayopasa kupewa umuhimu mkubwa katika sheria za kimataifa kwa kutilia maananni kwamba zinabainisha vyema umuhimu wa kulindwa haki za binadamu bila ya kujali dini, rangi, ukabila wala utaifa wao. De Milo ameendelea kusema kuwa kuenea kwa dini tukufu ya Kiislamu katika nchi za Magharibi ni dalili ya wazi kuwa mafundisho ya dini hii yanawahusu wanadamu wote. Amesema kuwa hata kama kuna hujuma ya makusudi inayoenezwa na makundi fulani dhidi ya dini hii lakini ni wazi kuwa hujuma hiyo haitadumu kwa muda mrefu kwa sababu Waislamu nao wameanzisha mbinu za kujitetea na kulinda thamani za dini yao dhidi ya hujuma hiyo.

Ufafanuzi

MBINU ZA MAADUI KUZUSHA FITINA

MBINU ZA MAADUI KUZUSHA FITINA MBINU ZA MAADUI KUZUSHA FITINA Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo amehutubia umati mkubwa wa maelfu ya wanafunzi wa vyuo vya kidini, maulamaa, walimu na maimamu wa swala za jamaa wa misikiti ya Tehran kwa mnasaba wa kukaribia mwezi wa Muharram akisema kuwa ulinganiaji sahihi ni kuwazindua wananchi na kuwawezesha kumaizi mambo katika jamii hususan katika kipindi cha fitina. Ayatullah Khamenei ameashiria matukio ya baada ya uchaguzi wa Rais hapa nchini hususan hatua ya hivi karibuni ya maadui wa taifa la Iran ya kumvunjia heshima Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu na akawashukuru wananchi kwa kuwa macho na kujitokeza kwa wingi kupinga kitendo hicho. Vilevile amewataka wananchi wote kuwa watulivu hususan tabala la wanafunzi wa vyuo vikuu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa jengo hili imara ambalo uhandisi wake ni wa Mwenyezi Mungu, umetayarishwa na rijali wa Mwenyezi Mungu na litabakia kwa himaya ya taifa linalomwamini Mwenyezi Mungu, litabakia imara daima na maadui hawatafikia malengo yao. Ayatullah Ali Khamenei ameashiria matukio ya baada ya uchaguzi wa Rais hapa nchini na akasema inasikitisha kwamba baada ya uchaguzi huo baadhi ya watu walivunja sheria na kuanzisha ghasia na kutayarisha uwanja uliowapa matumaini maadui waliokuwa wamekata tamaa kiasi cha kuthubutu kumvunjia heshima Imam Khomeini mbele ya macho ya wanafunzi wa vyuo vikuu wafuasi wa Imam, Mapinduzi na mfumo wa Kiislamu hapa nchini. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa kitendo hicho cha kumuvunjia heshima Imam ni matokeo ya ukiukaji huo wa sheria na kuridhishwa na uungaji mkono wa vyombo vya habari vya wageni, na baada ya makosa hayo kutukia zinafanyika jitihada za kuyaficha kwa kutoa visingizio mbalimbali.

Ufafanuzi

GHADIR NA SUALA LA UMOJA

GHADIR NA SUALA LA UMOJA GHADIR NA SUALA LA UMOJA Kitabu cha 'al-Ghadir' kilizusha wimbi kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Kitabu hicho kimewapelekea wasomi na wanafikra wa Kiislamu kukichambua katika mitazamo mbalimbali ya fasihi, historia, itikadi, hadithi, tafsiri na jamii. Jambo linaloweza kuzingatiwa kwa uwazi zaidi katika mtazamo wa kijamii kuhusiana na kitabu hicho ni uzito wa umoja wa Kiislamu unaotiliwa mkazo na kitabu hicho muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu. Wahubiri, wasuluhishi, wanafikra na wasomi wa Kiislamu, kwa karne nyingi sasa wamekuwa wakichambua na kuzungumzia umuhimu wa kuwepo umoja na mshikamano kati ya mataifa, jamii na makabila mbalimbali ya Kiislamu na hasa katika zama hizi ambapo maadui wa Waislamu wanawahujumu kutokea kila upande na kwa kutumia zana na silaha mbalimbali hatari. Kwa kuendesha hujuma hiyo, maadui wana lengo la kuwatawanya na kuwasambaratisha Waislamu kupitia uchochezi wa hitilafu kongwe na nyingine zinazozushwa katika zama hizi. Kwa kuzingatia ukweli huo, wanafikra wa Kiislamu wanaamini kuwa kuna udharura mkubwa wa kuimarishwa umoja na mshikamano kati ya Waislamu hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote ule.

Ufafanuzi

GHADIR IZINGATIWE

GHADIR IZINGATIWE GHADIR IZINGATIWE Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alipokutana na maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali waliokwenda kuonana naye kwa mnasaba wa sikukuu ya Ghadiri Khum (siku Imam Ali bin Abi Twalib alipotawazwa rasmi na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa Imam na kiongozi wa umma wa Kiislamu baadaye yake) alisema kuwa suala la Ghadir ni kigezo cha milele cha Mwenyezi Mungu kinachoainisha njia sahihi ya umma wa Kiislamu. Ayatullah Khamenei ameashiria urongo mkubwa unaoenezwa na Wazayuni na nchi za kigeni kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran kwa shabaha ya kupotosha fikra za walimwengu na akasema kuwa urongo huo utawafedhehesha zaidi maadui wa taifa la Iran baada ya kudhihiri ukweli wa mambo. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amewapongeza wananchi wa Iran na Waislamu wote ulimwenguni kwa mnasaba wa sikukuu ya Ghadir. Akifafanua sababu ya sikukuu hiyo kuitwa sikukuu kubwa zaidi ya Mwenyezi Mungu (Idullahil Akbar), Ayatullah Khamenei amesema, tukio la Ghadiri Khum lilikuwa na maana kubwa zaidi kuliko idi na sikukuu nyingine za Kiislamu, kwani kwa mujibu wa vigezo vya Mwenyezi Mungu, wajibu wa Waislamu kuhusu uongozi na serikali uliainishwa katika siku hiyo.

Ufafanuzi

CHINI YA KIVULI CHA MTUME

CHINI YA KIVULI CHA MTUME CHINI YA KIVULI CHA MTUME Kila tunapoifikia siku ya kuadhmisha kuzaliwa Bw. Mtume Mohammad al Mustafa (S.A.W.W), tunatakiwa tufahamu kuwa: Yeye ni shaksia aliyekuwa ni chanzo na chimbuko la umoja katika vipindi vyote vya historia ya Uislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW ndiye dira ya hisia na itikadi za umma wa Kiislamu. Kwa hakika Mtume SAW ni nukta ya kukurubiana Waislamu na madhehebu ya Kiislamu. Hakuna shaka kuwa siku kuu yenye baraka ya kuadhimisha kuzaliwa Mtume SAW ndio wakati muhimu zaidi wa kuchukua hatua zenye athari katika kuleta umoja wa Kiislamu. Tunachukua fursa hii kuwapongeza Waislamu wote duniani kwa mnasaba huu muhimu wa Milad Un Nabii na Wiki ya Umoja wa Kiislamu. Umoja ndio msingi muhimu zaidi ambao unawezesha taifa au umma wowote ule kufikia malengo yake. Ni kwa sababu hii ndio maana moja ya ahadi na mapatano ya Mwenyezi Mungu na Mitume Wake ikawa ni kuleta Umoja na mshikamano katika jamii. Quran Tukufu inakumbusha kuwa wanaadamu wote wameumbwa kwa udongo na wametokana na baba na mama mmoja. Quran Tukufu katika aya yake iliyo wazi kabisa inawataka Waumini wote wajiepushe na mifarakano. Katika aya ya 103 ya Surat Aali Imran, Mwenyezi Mungu anasema: "Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyokuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu…"

Ufafanuzi

CHANGAMOTO ZA UMOJA

CHANGAMOTO ZA UMOJA CHANGAMOTO ZA UMOJA Umoja ni mojawapo ya maamrisho matakatifu ya Mwenyezi Mungu yanayotuliza zaidi moyo na ambayo harufu yake nzuri bila shaka huhisika na kila mtu ambaye moyo wake umezama katika dini takatifu ya Uislamu. Maisha ya Waislamu na jamii za Kiislamu zinapasa kujengeka juu ya msingi wa mafundisho na maana ya kuvutia ya neno umoja. Sauti tamu na ya kuvutia ya aya: 'Na shikamaneni kwa kamba (dini) ya Mwenyezi Mungu nyote, wala msiachane' (3:103), 'Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake wala msizozane (msigombane), msije mkaharibikiwa na kupoteza nguvu' (8:46), 'Na kwa yakini huu umma wenu ni umma mmoja' (23:52) na aya nyinginezo ambazo huashiria moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, umuhimu wa kuimarishwa umoja na kuepukwa mifarakano kama zile zinazoanza na ibara, 'Enyi mlioamini' na 'Enyi watu', zote hizi zinaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu na mawalii wake wema wanataka kufikiwa kwa jambo hili muhimu kwa upande mmoja na kwa upande mwingine kuonyesha kwamba ndio ufunguo wa kufanikiwa Waislamu maishani mwao. Ushauri na maamrisho ya Mtume Mtukufu (SAW) na maimamu watoharifu (AS) kuhusiana na umuhimu pamoja na udharura wa kuimarishwa umoja miongoni mwa Waislamu ni jambo ambalo linadhihiri wazi katika mafundisho ya Kiislamu. Kwa msingi huo, jaribio lolote la Muislamu kutaka kuudhuru umoja wa Waislamu kwa kisingizio choche kile ni suala lisilosameheka hata kidogo. Ni wazi kwamba tabia na vitendo vya mtu kama huyo huwa havitofautiana kabisa na vile vinavyotekelezwa na maadui ima kwa siri au kwa uwazi kwa shabaha ya kukabiliana moja kwa moja na mafundisho ya dini kwa visingizio mbalimbali.

Ufafanuzi

TUSIKUBALI KULAZIMISHWA

TUSIKUBALI KULAZIMISHWA TUSIKUBALI KULAZIMISHWA Magharibi wasitulazimishie 'demokrasia' yao yenye utata. Nchi zote za Magharibi, kwa kutaja chache tu; Marekani, Uingereza, Ufaransa, Japan na nyingine zina demokrasia. Lakini je, zote zina aina moja ya mfumo wa demokrasia? Mfumo upi kati ya hiyo ni wa kidemokrasia zaidi? 'Demokrasia' za Magharibi zenyewe zina tofauti kubwa katika aina ya tawala za kisiasa zinazolenga kupata matokeo yale yale katika jamii yenye demokrasia. Ikiwa matokeo ya kujenga taifa la kidemokrasia ni kanuni ya thamani au faida inayotumiwa, basi swali linaloletwa hapa kwa hakika ni la balagha, yaani lisilohitaji jibu, kwa sababu patakuwapo mifumo mingi yenye ufanisi ya demokrasia kwa kadiri ya idadi za mataifa na nchi zilizopo duniani. Ikiwa tunu za demokrasia ni aina moja kwa wanadamu wote, na zinapendwa na wote, nini hiki kinachodaiwa kuwa ni 'Magharibi' kumiliki demokrasia kwa sababu tu, katika historia, wao (mataifa ya Magharibi) yalianza zamani safari yao kuuendea uhuru wakati wengine waliachwa nyuma kwa sababu mbalimbali, ukiwamo ukoloni (sema 'unyimi wa haki za kidemokrasia') na nchi hizo hizo za Magharibi? Ikiwa, kwa ajili ya hoja au ubishani, jibu la swali lililoulizwa hapo ni 'NDIO', na marejeo kwa aina ya demokrasia ya Magharibi yanamaanisha kiukweli kupendekeza kwamba aina pekee za demokrasia za Magharibi ndizo zinatakiwa kunakiliwa au kufuatwa na mataifa mengine, bila kujali historia za jadi ya sehemu husika na taasisi zake, basi ni muhimu kabisa kutabiri kwamba patakuwapo na asilimia 100 ya pingamizi au upinzani wa kutoa na kulazimishia matumizi ya 'mfumo wa demokrasia ya Magharibi', tena kutoka maeneo mawili tofauti katika nchi zinazoitaka demokrasia.

Ufafanuzi

MTAZAMO WA HIZBU TAHRIIR

MTAZAMO WA HIZBU TAHRIIR MTAZAMO WA HIZBU TAHRIIR WAJIBU WA SHERIA KATIKA JAMII Ushahidi wa Faradhi ya Khilafah Uisilam umerejeshwa kuwa ni dini tu ya nchi na usekula umefanywa kuwa ndio itikadi ya kuendeshea maisha. Makafiri wamefanikisha katika kuitenganisha dini na dunia na kutenganisha mfumo wa utawala wa Ukhalifah katika maisha na akili za Waisilamu.. "Lazima tuufishe chochote amabcho kitajaribu kuujenga tena Ummoja Kiisilam kwa kizazi cha Waisilam. Kama tulivyofanikisha kuumaliza utawala wa Khilafah, hivyo ni lazima tuhakikishe kuwa ummoja wa Waisilam haufufuki tena, ikiwa ni kifikra au kielimu." Maneno ya Waziri wa Nje wa Uingereza akimwambia hayo kwa Waziri Mkuu wake kabla ya vita vya pili vya dunia. "Hali halisi sasa ni kuwa Uturuki imekufa na haitofufuka tena, kwa sababu tumeiangamiza nguvu yake, Khilafah na Uisilam". Maneno ya Lord Curzon, Waziri wa Nje wa Uingereza aliyoyanukuu mbele ya baraza la Wakilishi baada ya mkataba wa Lausanne wa tarehe 24/07/1924. Hivi kweli ni ajabu leo hii kuwa Waisilam hawajui chochote kuhusiana na mfumo wao wa kweli wa utawala? Kuwa hawajawahi kabisa kusikia neno hilo hata kutajwa katika mazungumzo na harakati za kuufufua ummah? Waingereza kweli wamefanikiwa kutuelimisha hadi kufikia kuwa tunaukimbilia mfumo wao wa utawala na kuutupa mbali mfumo wetu wa haki uliotokana na dini yetu hii ya Uisilam. Hivyo basi, ni nini hii Khilafah? Na kwa nini ni muhimu katika Uislam?

Ufafanuzi

MAMBO YASIYO FAA

MAMBO YASIYO FAA MAMBO YASIYO FAA Asalaam alaikum warahmatullahi wabarakatuh. Shukran zote anastahiki Allah (S.W.T) na rehema na amani zimshukie bwana wetu Muhammad (S.A.W). HUU NI UJUMBE, NA ANAESOMA UJUMBE HUU AMFIKISHIE MWENZIWE KWA NJIA YOYOTE ILE ILI TUSIWE NA DHIMA MBELE YA ALLAH. Allah (S.W.T) anasema katika Qur-aan suratul Al Imran aya 31: 31. Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. *** 32. Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakigeuka basi Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri. *** Na hadithi ya Mtume wetu (S.A.W) inaeleza hivi: Watu wote wataingia peponi ila asietaka,masahaba wakaumuuliza ewe mjumbe wa Allah, nani hao wasiotaka? Rasuul (S.A.W) akasema atakae nitii ataingia peponi na atakae niasi ataingia motoni. Hoja ninayoitaka kuieleza ina umuhimu katika maisha yetu na ambayo kila kukicha mambo yanazidi kugeuka na kubadilika sura.Na kama tukiachia hali hii iendelee tutafika mbali.

Ufafanuzi

ARDHI ILIYOSAHAULIKA

ARDHI ILIYOSAHAULIKA ARDHI ILIYOSAHAULIKA UTANGULIZI Ardhi hii iliyosahaulika ilikuwa na migongano mingi sana baina ya staarabu tofauti, baina ya Uislamu na Ukafiri, baina ya haki na batili na baina ya at-Tawheed na shirki. Migongano hii ilikuwa ya kutumia silaha au baridi kwa kuelezea, kujadiliana na kulingania. Mgomgano wa mwisho ni ule ulioletwa na maandishi ya Mkataba wa Sykes - Picot ulioandikwa 1916 baina ya Uingereza na Ufaransa.Ardhi hii inatajwa ana lakini haipo kwenye ramani na imesahaulika sana na hususan sisi Waislamu. Allah, Mtume Wake na historia imetupatia sifa tofauti ya ardhi hii. Sifa hizi zimefanya kila taifa kuigombea.

Ufafanuzi

UMASKINI

UMASKINI CHANZO KIKUU CHA UMASKINI WA TANZANIA Miaka nenda miaka rudi, taifa la Tanzania limeeendelea kuhesabika miongoni mwa nchi maskini kabisa duniani. Sio tu kuhesabika uko kwa taifa hili kuko katika takwimu za wataalamu wa uchumi, bali pia kiwango cha maisha ya watanzania wengi ni cha chini sana. Watanzania tumeeendelea kuishi maisha ya dhiki sana, mulo kwa wengi kuupata imekuwa taabu, nyumba wanamoishi watu ni hohehahe, elimu ya wengi wetu ni duni, kusafiri toka sehemu moja hadi nyingine shida tupu (vijijini na mijini), huduma za afya licha ya kutopatikana kwa urahisi, zilizopo wanaomudu gharama zake ni wachache na hata hivyo hazilidhishi, vipato vya wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara viko hoi, ili mradi tu ni dhiki juu ya nyingine. Wakati walio wengi taabu zetu kwa kutaja chache ndio hizo, wapo wenzetu wachache nchini ambao maisha yao ni ya neema, tena neema tele. Watanzania tumeendelea kujiuliza, kulikoni bila majibu. Baadhi yetu tu, mfano wasomi na wengine,wamejaribu kutafuta majibu na ufumbuzi wa umaskini huu lakini hadi sasa bila suluhisho. Kwa kutumia nadharia kwa mfano, wapo wanaosema chanzo na kiendelezo cha umaskini wetu, ni tabia ya watanzania wengi kutojiwekea akiba, yaani baada ya kuzalisha kidogo, kidogo hicho chote kinawekwa katika matumizi, hivyo hakuna akiba na kwahiyo hakuna uwekezaji katika mradi wowote mpya wa uzalishaji au kupanua uliopo, na matokeo yake uzalishaji unaendelea kuwa kidogo kama sio kupungua, ilimradi unakuwa ni mduara tatizi usiokoma wa ufukara. Kwa kusimamia kwenye nadharia hii, wapo wanaotuhubiria watanzania kwamba tujenge tabia ya kuweka akiba jamani. Ni mahubiri mazuri sana, lakini swali la kujiuliza hapo ni je, kweli kuna mtanzania asiyetaka kuweka akiba? Kwa maoni yangu, mtanzania wa hivyo hajazaliwa, bali sisi tunaoishi roho zetu zi radhi kuweka akiba lakini hali halisi inakataa. Wengi watakubaliana nami kwamba, mfanyakazi wa Tanzania ya leo ambaye mara nyingi mshahara wake wa mwezi huisha siku kumi au kumi na tano baada ya kuupokea, kumwambia aweke akiba ni kumkejeli mchana kweupe!

Ufafanuzi

TABIA NJEMA NA ATHARI ZAKE KLATIKA UISLAMU

TABIA NJEMA NA ATHARI ZAKE KLATIKA UISLAMU NAFASI YA TABIA KATIKA MWENENDO WA MTUME Mamboi matatu yajulikanayo kuwa ndio sababu ya kuendelea na kuhuyika dini. ama ni yapi mambo hayo? ili kuyajua mambo hayo, ungana nami katika makala hii mapaka mwisho.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini