Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Imam Baaqir (a.s)

MAISHA YA IMAMU BAAQIR (A.S)

MAISHA YA IMAMU BAAQIR (A.S)

MAISHA YA IMAMU BAAQIR (A.S) Tarehe saba mwezi wa Dhihijja inasadifiana na siku ya kukumbuka siku aliyoaga dunia mmoja wa wajukuu watoharifu wa Mtume Muhammad (saw). Tonakupeni mkono wa pole enyi wapenzi Waislamu kwa mnasaba huu mchungu na tunakukaribisheni kusikilza machache kuhusu maisha ya mtukufu huyo. Siku ambayo habari za kuaga dunia Imam Muhammad Baqir (as) zilienea katika mji mtakatiu wa Madina, mji huo ulighubikwa na huzuni kubwa ya wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw). Hii ni kwa sababu hawakuwa wakiuona tena uso wenye nuru wa mjukuu huyo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu wala kusikia sauti yake changamfu na yenye kutuliza nyoyo katika Msikiti wa Mtume (saw). Hali hiyo ya huzuni iliwaathiri zaidi wafuasi wa karibu wa Imam Baqir na hasa Jabir bin Yazid Ju'fi. Siku na wakati ulikuwa ukimpitia kwa tabu kubwa Jabir. Alikuwa na kumbukumbu nzuri na ya kuvutia kutoka kwa Imam Baqir (as). Alipomwona Imam kwa mara ya kwanza, alikuwa kwenye Msikiti wa Mtume (saw) ambapo alikuwa amezungukwa na watu walioonekana kuwa na hamu kubwa na kusikiliza kwa makini maneno ya hekima aliyokuwa akiyasema. Imam alikuwa akizungumzia utafutaji elimu na umuhimu wake. Alipomkaribia, alimsikia Imam akisema: "Tafuteni elimu, kwa sababu utafutaji elimu ni jambo zuri. Elumu ni mwongozi wako kwenye giza, msaidizi wako katika mazingira magumu na rafiki mwema wa mwanadamu."

Ufafanuzi

FADHILA ZA MWALIMU

FADHILA ZA MWALIMU FADHILA ZA MWALIMU "Imam Baaqir (a.s) amesema:Mwenye kufundisha (jambo lolote la) kheri,wanyama wa ardhini humuombea maghfira (au msamaha kwa Mwenyeezi Mungu -s.w-),na wanyama wa baharini,na chochote kile kinachopatikana katika ardhi ya Mwenyeezi Mungu au katika mbingu yake,sawa sawa kile kidogo sana au kikubwa,humuombea maghfira na msamaha." Ufafanuzi wa hadithi hii: Hadithi hii,inaonyesha umuhimu wa Mwalimu na fadhila kubwa alizonazo mbele ya Mwenyeezi Mungu (s.w),hadithi inasema kwamba: viumbe wote wa Mwenyeezi Mungu (s.w) wanaopatikana ardhini na mbinguni,humuombea msamaha na maghfira Mwalimu huyu.Lakini si kila mwalimu hufanyiwa hivyo!,bali yule tu mwenye kufundisha na kuelimisha jambo lolote lile la kheri,ama yule mwenye kupotosha akidai kwamba anafundisha au anaelimisha,kumbe anawapeleka watu njia isiyokuwa yenyewe na hatimaye kuwapoteza,huyo hapati uombezi huu wa maghfira kutoka kwa kila kiumbe cha Mwenyeezi Mungu (s.w) bali hupata kinyumbe chake.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini