Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Kusoma Qurani

ATHARI YA DINI TAKATIFU

ATHARI YA DINI TAKATIFU

ATHARI YA TAWHIYD KATIKA KUKAMILIKA MWANAADAMU KIELIMU Itikadi ya kuamini Mola mmoja ni alama inayoonesha ukamilifu wa mwanaadamu kielimu, na ubora wa mwanaadamu kuliko malaika. Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:- شَهِدَ اللّهُ اَنَّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ وَالْمَلاَئِكَةُ وَاُوْلُواْ الْعِلْمِ قَآئِمَاً بِالْقِسْطِ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ[1] Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. Basi iwapo mtu atauona utukufu wa Mwenyeenzi Mungu na uumbaji wa ulimwengu, na akazishuhudia aya za Mwenyeezi Mungu, lakini asiamini Mola mmoja huyo, basi mtu huyo atakuwa ni miongoni mwa majahili, na ni alama moja wapo inayoonesha ujahili wa mtu huyo.

Ufafanuzi

DINI ZA MOLA MTAKATIFU

DINI ZA MOLA MTAKATIFU UHAKIKI WA DINI KUPITIA MSINGI WA IJTIHADI. Hatua ya kwanza: Umuhimu wa maudhui (mada). 1. Kila haki imebeba maumbile mawili, umbile la ndani na umbile la nje, maumbile hayo huthibitishwa na kusadikishwa kutokana na ukweli wa haki hiyo, kwa ufafanuzi zaidi tunaweza kusema hivi:- Haki ni kama kombe na lulu, lulu ambayo hupatikana katika kombe hiyo, kombe ni umbile la nje na lulu ni umbile la ndani, hivyo kuna uwiano baina ya vitu hivyo viwili, bila ya kuonekana kombe hatuwezi kuthibitisha kuwa katika kombe hiyo mna (lulu) ndani yake au mna kitu chengine. Kwa hiyo kadiri itakavyoonesha kuwa umbile la nje lina thamani na muhimu, basi umbile la ndani pia litakuwa ni muhimu na lenye thamani zaidi.

Ufafanuzi

HISTORIA YA QUR_ANI

HISTORIA YA QUR_ANI HISTORIA KUHUSIANA NA MAUDHUI YA MIUJIZA Ijapokuwa haieleweki ya kwamba maudhui kuhusu miujiza yalianza kipindi gani, lakini muujiza wa qur-ani ndio maudhui ya mwanzo yaliyokuja yanayohusiana na Qur-ani. Na Qur-ani tukufu kwa kuthibitisha madai yake hayo – yaani kuwepo kwa muujiza kuhusiana na kitabu hicho – imetumia neno muujiza, katika kipindi chote hicho kilichopita Qur-ani inapoelezea kuhusu miujiza ya Mitume hutumia neno (ايه na  بينه) kwa kuthibitisha kuwepo kwa miujiza, na kwa sababu hiyo basi neno (istilaha) muujiza (معجزه)  kutokana na riwaya au hadithi zilizokuja ndio neno la mwanzo lililotumika kuthibitishia madai yake hayo1. na baadae ndio zikatumika istilaha (maneno) nyengine, na istilaha hizo ziliendelea kuenea siku hadi siku2.

Ufafanuzi

KUKAMILIKA KWA MWANAADAMU

KUKAMILIKA KWA MWANAADAMU SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU Katika makala iliyopita tulielezea sharti na vizuizi vinavyomfanya mwanaadamu asifikie katika ukamilifu, na hii ni kwa sababu hakuweza kumfahamu Mola wake, katika makala hii tutaendelea kuelezea masharti na vizuizi vinavyomfanya mwanaadamu asiweze kufikia katika ukamilifu. 2) Maisha salama na viongozi waaminifu. Ijapokuwa kumfahamu Mwenyeezi Mungu ni mahitajio ya nafsi yaliyomo ndani ya nyoyo za wanaadamu, na fitra hiyo inawiana na akili na dalili, lakini kukua kwa fitra hiyo na kudhihirika matumaini ya akili na ya kimoyo mwanaadamu anahitajia mazingira yaliyo salama ili aishi katika mfumo wa maisha ambao utamuongoza yeye kufikia katika njia ya saada.

Ufafanuzi

MAYAHUDI WAIPINGA QUR_ANI TAKATIFU

MAYAHUDI WAIPINGA QUR_ANI TAKATIFU MAYAHUDI HAWAISADIKI QUR_ANI TAKATIFU WALA HAWAMSADIKI MTUME (S.A.W.W). Katika makala iliyopita tulielezea vipi Mayahudi walimkanusha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kitabu chake, katika makala hii basi tutaendelea na mada yetu hiyo na kutupilia macho mitihani ambayo Mwenyeezi Mungu anawapa waja wake. Suleimani aliyetajwa hapa ni Nabii suleimani. Mayahudi wanamwitakidi nabii Suleimani kuwa ni Mfalme aliyepata ufalme wa uchawi, si Mtume,basi na hawa wachawi wa kiislamu humnasibisha nabii Suleimani hizo elimu zao za uchawi, basi Mwenyeezi Mungu anamkanushia haya.

Ufafanuzi

MAYAHUDI WAZIKADHIBISHA DINI ZA ALLAH

MAYAHUDI WAZIKADHIBISHA DINI ZA ALLAH MAKAFIRI WANAMKADHIBISHA NA KUMTUKANA MTUME (S.A.W.W) Katika makala iliyopita kuhusiana na kauli ya Mwenyeezi Mungu juu ya makafiri tulielezea kwa muhtasari jinsi Makafiri walivyokuwa wakimkadhibisha na kumtukana Mtume muhammad (s.a.w.w.). Na vile vile hawakukiamini kitabu chake Kitukufu – Qur_ani - . Katika makala hii basi tutaendelea kuielezea mada hiyo kwa kuzingatia Aya za Qur-ani za Mwenyeezi Mungu. hivyo endelea kuwa nami mpaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

SHARTI ZA KUKAMILIKA KWA MWANAADAMU

SHARTI ZA KUKAMILIKA KWA MWANAADAMU SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU NO.3 Tukiendelea na mada yetu inayohusiana na masharti na vizuizi vinavyompelekea mwanaadamu asiweze kufikia katika ukamilifu, katika makala hii tutaelezea masharti sharti jengine linalomfanya mwanaadamu asifikie katika ukamilifu. Sharti hilo ni:- Kunufaika na muongozo wa Mitume na Maimamu (a.s).Ili tumfahamu Mwenyeezi Mungu zaidi ni lazima tujiepushe na yale aliyotukataza, ili tunufaike na uongofu na uwalii wa Mitume na Maimamu (a.s), kwa sababu Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndio kiumbe bora aliye karibu na Mwenyeezi Mungu.

Ufafanuzi

SHARTI ZA KUKAMILIKA KWA MWANAADAMU NO.2

SHARTI ZA KUKAMILIKA KWA MWANAADAMU NO.2 SHARTI ZA KUFIKIA MJA KATIKA UKAMILIFU NO.2 Tukiendelea na mada yetu inayohusiana na masharti na vizuizi vinavyompelekea mwanaadamu asiweze kufikia katika ukamilifu, katika makala hii tutaelezea masharti sharti jengine linalomfanya mwanaadamu asifikie katika ukamilifu. Sharti hilo ni:- 3) Chuki na kukalidi matendo ya wengine. Sharti ya tatu miongoni mwa masharti yanayomfanya mwanaadamu amfahamu Mola wake ni kujiepusha na chuki, kukalidi au kuiga matendo ya wengine bila ya kuwa na dalili au elimu nayo.

Ufafanuzi

UMUHIMU WA HIJABU KATIKA JAMII

UMUHIMU WA HIJABU KATIKA JAMII

Ufafanuzi

UTUKUFU WAKE MOLA MTAKATIFU

UTUKUFU WAKE MOLA MTAKATIFU SIFA TUKUFU ZA MWENYEEZI MUNGU. Qur-ani kariym amemsifu na kumuelezea Mwenyeezi Mungu kwa sifa zilizo bora na kamili kabisa, na imejiepusha na kumuelezea kwa sifa mbaya. Katika Suratul-Hashri Aya ya 22-24 tunasoma:- هُوَ اللهُ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ[1] Yeye ndiye Mwenyeezi Mungu ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye tu. Anayejuwa yaliyofichikana na yaliyo dhahiri. Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.  هُوَ اللهُ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلاَمُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ سُبْحَانَ اللهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ[2] Yeye ndiye Mwenyeezi Mungu ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye tu; Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye shani, Anayefanya analolitaka, Mkubwa. Mwenyeezi Mungu Yu mbali na hao wanaomshirikisha naye.

Ufafanuzi

BAADHI YA TABIA NJEMA ZA MTUME S.A.W.W

BAADHI YA TABIA NJEMA ZA MTUME S.A.W.W BAADHI YA TABIA ZAKE NABII MUHAMMAD (S.A.W.W) Miongoni mwa tabia njema nyengine za Mtume (s.a.w.w) ni kuwa Yeye alikuwa ni mwenye upendo na huruma, na alifanya jitihada zake zote katika kuwaongoza watu katika njia njema yenye saada, kama anavyosema Allah (s.w):- وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ اَن تَبْتَغِيَ نَفَقاً فِى الاَرْضِ اَوْ سُلَّماً فِى السَّمَاء فَتَاْتِيَهُم بِآيَةٍ وَلَوْ شَاء اللّهُ لَجَمَعَهُمْ عَلـٰي الْهُدَي فَلاَ تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ[1] Na ikiwa ni makubwa kwako huku kukataa kwao, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara -- Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa angeli wakusanya kwenye uwongofu. Basi usiwe miongoni mwa wasio jua.

Ufafanuzi

DARAJA BORA YA NABII MUHAMMAD (S.A.W.W)

DARAJA BORA YA NABII MUHAMMAD (S.A.W.W) DARAJA ILIYO BORA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W). Mitume yote ya Mwenyeezi Mungu imeshirikiana katika sifa ya daraja ya utume, - yaani Mitume yote imepewa sifa hii tufu na Mola wao – na vile vile Mitume hiyo wana nuru ya elimu waliyopewa na Mola wao, na kwa elimu hiyo ni kwa ajili ya kuwaongowa wanaadamu na kuwaongoza katika njia njema, vile vile kwa elimu hiyo huweza kuwajibu watu masuala yao. Sifa nyengine waliyonayo Mitume ni kuwa wao ni maasumu, na wameepukana na kila machafu, na sifa hii huwafanya wanaadamu wawe na imani na Mitume hiyo na kuwa na uhakika na yale ambayo Mitume hiyo inawalingania. Sifa nyengine waliyonayo Mitume ni kuwa wote walikuwa wakifanya jitihada katika kuufikisha ujumbe waliopewa na Mola wao, na vile vile walikuwa na huruma na watu wao.

Ufafanuzi

FADHILA ZA MTUME (S.A.W.W) KATIKA QUR_ANI

FADHILA ZA MTUME (S.A.W.W) KATIKA QUR_ANI 2. HUKUMU NA FADHILA ZA QUR_ANI, NI ALAMA BORA INAYOONESHA UBORA WAKE (S.A.W.W). Vitabu vyote vya Mwenyeezi Mungu alivyoviteremsha kwa Mitume yake ni vyenye nuru na vinavyowaongoza watu katika njia ya uongofu,Kwa hiyo vitabu vyote vya Mwenyeezi Mungu vinatuonesha nuru na uongofu lakini kitabu cha qur-ani ndani yake kimekusanya hukumu zote zilizomo ndani ya vitabu hivyo, yaani kitabu cha Qur-ani ni kiongozi wa vitabu vyote hivyo vya Mwenyeezi Mungu. Mitme wote wamekuja na hukumu moja katika Itikadi ya Mungu, Mitume, Malaika, Kiama, Tabia njema na kama haya. Lakini katika mambo ya baadhi ya Hukumu wakikhitilafiana kidogo katika Sharia zao kwa mujibu wa nyakati zao hizo ambao ukikhitilafiana sana umbali wa nyakati wa baadhi ya Mitume na Mitume wengine, na mambo lazima yakhitalifu, na kila anayoyafanya Mwenyeezi Mungu,anayafanya kwa hikima.

Ufafanuzi

HEKIMA YA KUENDELEZWA NJIA ZA MITUME

HEKIMA YA KUENDELEZWA NJIA ZA MITUME HEKIMA YA KUENDELEZWA NJIA ZA MITUME Malengo na madhumuni waliyokuja nayo Mitume ni kuwaongoza watu katika njia ya Mwenyeezi Mungu, Mitume huwaongowa watu na kuwaongoza katika njia ya saada iliyo kamilifu. Kwa sababu hiyo basi ili kufikia katika malengo yao hayo, hawakuegemea na mawaidha au ujumbe waliopewa na Mola wao tu, bali walistahamili tabu na mashaka za makafiri na wale waliowapinga. Vile vile walifanya jitihada na kuwa viongozi wema na walio bora ili kuondoa serikali za za kitaghuti,na kupinga suna za kijahilia.

Ufafanuzi

MAKHALIFA WATAKAOENDELEZA NJIA ZA MITUME

MAKHALIFA WATAKAOENDELEZA NJIA ZA MITUME MAKHALIFA WANAOENDELEZA NJIA ZA MITUME. Malengo na madhumuni waliyokuja nayo Mitume ni kuwaongoza watu katika njia ya Mwenyeezi Mungu, Mitume huwaongowa watu na kuwaongoza katika njia ya saada iliyo kamilifu. Kwa sababu hiyo basi ili kufikia katika malengo yao hayo, hawakuegemea na mawaidha au ujumbe waliopewa na Mola wao tu, bali walistahamili tabu na mashaka za makafiri na wale waliowapinga. Vile vile walifanya jitihada na kuwa viongozi wema na walio bora ili kuondoa serikali za za kitaghuti,na kupinga suna za kijahilia.

Ufafanuzi

MTAZAMO WA ALLAH (S.W) KWA WAJA WAKE

MTAZAMO WA ALLAH (S.W) KWA WAJA WAKE MTAZAMO WA ALLAH (S.W) KWA WAJA WAKE *Mayahudi kwa kujitapa kuwa ni watukufu, kwa kule kunasibikana kwao na Mitume, walikuwa wakidai kuwa hawataadhibiwa ila siku arobaini tu ambazo wazee wao waliabudu ndama, Mwenyeezi Mungu anawakadhibisha kwa Aya hizi kwamba, yoyote atakayefanya maovu ataadhibiwa kwa maovu yake, na hapana litakalomnusuru mtu ila imani na amali njema.Basi wananasihiwa wale wanaojigamba kwa sababu na kuona kuwa nasabu zao zitawatosha mbele ya Mwenyeezi Mungu. Mungu ameyakataa haya katika mahala pengi katika Qur-ani, pamoja katika humo ni Aya ya 101 ya suratul-Muuminuun, na Mtume ameyakataa katika hadithi nyingi.

Ufafanuzi

MUHAMMAD (S.A.W.W) MTUME WA MWISHO

MUHAMMAD (S.A.W.W) MTUME WA MWISHO MTUME MUHAMAD (S.A.W.W) NI MTUME WA MWISHO. *Khaataman Nabiyyiin, maana yake mwisho wa Mitume. Na inaonesha ukamilifu wa Mtume huyo, na Mtume wa mwisho ni yule ambaye anabakia kuwa mkamilifu hadi siku ya Kiama, na hakuna Mtume mwengine yoyote atakayekuja baada yake. Na hii ni kwa sababu akili inakubali kufuata kile kilicho bora na kikamilifu zaidi. Na vile vile Mtume wa mwisho ni yule ambaye ni m-bora zaidi kuliko wengine, kwa sababu Yeye ni mwenye kuchukua ujumbe wa dini iliyo kamilifu, na natija ya hayo ni kwamba dini ya kiislamu ni dini kamilifu zaidi, na Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni m-bora wa Mitume yote ya Mwenyeezi Mungu.

Ufafanuzi

MUISLAMU WA MWANZO

MUISLAMU WA MWANZO 1. MUISLAMU WA MWANZO. Katika kamusi ya Qur-ani Mjiyd (Muslim) ni mtu ambaye amesalimu katika kutii amri za Mola wake, kama alivyosema Mfalme (Malkia)Sabaa:- قِيلَ لَهَا ادْخُلِى الصَّرْحَ فَلَمَّا رَاَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّةً وَكَشَفَتْ عَن سَاقَيْهَا قَالَ إِنَّهُ صَرْحٌ مُّمَرَّدٌ مِّن قَوَارِيرَ قَالَتْ رَبِّ إِنِّى ظَلَمْتُ نَفْسِى وَاَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَانَ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ[1] Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema:Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Kwa maana hiyo basi, Mitume na wajumbe wote wa Mwenyeezi Mungu walikuwa ni Waislamu, yaani hawakuwa washirikina wala walikuwa hawafuati dini zilizoharifiwa, kama tunavyosoma kuhusiana na Nabii Ibrahimu (a.s).

Ufafanuzi

NI WATU GANI WASIOPASWA KUTIIWA

NI WATU GANI WASIOPASWA KUTIIWA NI WATU WA AINA GANI AMBAO HAWAPASWI KUTIIWA? Mwenyeezi Mungu Mtukufu ili kuzuia dhulma na kuleta uadilifu katika jamii ametukataza kuwatii baadhi ya watu, na vile vile ametukataza tusiwachague watu madhalimu kutuongoza. Miongoni mwa watu hao ni kama hawa wafuatao:- 1- Watu wanaofanya israfu na kuleta ufisadi katika jamii. Yaani ni wale watu ambao hufanya kila wawezalo kuleta ufidasi katika jamii,  na hutumia mali za baytul-mali katika mahitajio yao binafsi au kwa wale walio karibu nao. Na hufanya israfu katika mali za baytul-mali kuwanyima watu haki zao.

Ufafanuzi

TABIA NJEMA ZA MTUME (S.A.W.W)

TABIA NJEMA ZA MTUME (S.A.W.W) TABIA NJEMA ZA MTUME (S.A.W.W). Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na uso wenye bashasha na furaha, maneno mazuri, na moyo wenye upendo na wakati wote alionekana na tabasamu usoni mwake. Na alikuwa ni mwenye jitihada katika kuwalingania watu na kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu. kama anavyosema Allah (s.w):- وَإِنَّ لَكَ لاَجْراً غَيْرَ مَمْنُونٍ. وَإِنَّكَ لَعَلى خُلُقٍ عَظِيمٍ[1] Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini