Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Kusoma Qurani

AINA TOFAUTI ZA AMANA

AINA TOFAUTI ZA AMANA

KUTOA AMANA. kutoa amana ni:- Mwanaadamu kuipeleka haki ambayo  aliweka ahadi ya kuitoa amana hiyo, na kinyume chake ni khiyana. Kuna aina tofauti za amana, miongoni mwa hizo ni:- 1. Baadhi ya amana ni haki za Mwenyeezi Mungu kwa wanaadamu, kwa mfano:- Hukumu za kisheria na ibada. 2. Na baadhi ya amana ni haki za Mitume ya Mwenyeezi Mungu kwa wanaadamu. kwa mfano:- Hukumu za Serikali, na sunna za Mitume. 3. Baadhi ya amana, ni haki za watu miongoni mwa watu wengine, kwa mfano:- mali, na vyenginevyo.

Ufafanuzi

IMAMU ALI (A.S) ANAPASWA KUTIIWA

IMAMU ALI (A.S) ANAPASWA KUTIIWA IMAMU ALI (A.S) NDIYE KHALIFA ANAYEPASWA KUTIIWA Imamu Ali (salamu ziwe juu yake) tangu utotoni mwake alikuwa ni mfuasi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), na katika kipindi chote cha uhai wake hakumlaumu Mtume, au kwenda kinyume na Amri zake (s.a.w.w). Imamu Ali (a.s) anasema:- ولقد کنت أتبعه اتباع الفصیل اثر امه[1] Mimi nilikuwa namtafuta Mtume (s.a.w.w), na nilikuwa pamoja naye kila anapokwenda, mfano wa mtoto wa ngamia anayemtafuta mama yake.

Ufafanuzi

MAKHALIFA WASIOPASWA KUTIIWA

MAKHALIFA WASIOPASWA KUTIIWA MAKHALIFA WASIOPASWA KUTIIWA Katika makala zilizopita tulielezea kuhusiana na wale makhalifa wanaopaswa kutiiwa. katika makala hii tutaendelea na mada yetu inayohusiana na maudhui hayo hayo. 5- Wale madhalimu. ni wale ambao hawaji matawi ya chini katika kuhifadhi serikali zao na vyeo vyao, na huwa tayari kufanya dhulma yoyote waitakayo ili kufikia katika mahitajio yao.

Ufafanuzi

MALIPO YA KUFIKISHA UJUMBE WA ALLAH (S.W)

MALIPO YA KUFIKISHA UJUMBE WA ALLAH (S.W) MALIPO YA KUFIKISHA UJUMBE WA ALLAH (S.W) Malipo ya kufikisha ujumbe na amana ya Mwenyeezi Mungu. Mitume ya  Mwenyeezi Mungu,walistahamili tabu na mashaka mengi ili kuwaongoza watu katika njia iliyo sahihi. Na walifanya jitihada zao zote ili kuwaokoa watu na maisha ya kidhulma. na hawakuhitaji malipo wala ujira  kutokana na tabu ambazo walizipata. Mitume ya Mwenyeezi Mungu, ijapokuwa hawakutaka ujira kutoka kwa watu, lakini  wana ujira mkubwa kutoka kwa Mola wao. kama tunavyosoma kuhusiana na Nabii Muhammad (s.a.w.w).:-  وَإِنَّ لَكَ لاَجْراً غَيْرَ مَمْنُونٍ

Ufafanuzi

MWANAMKE NDANI YA QUR_ANI

MWANAMKE NDANI YA QUR_ANI MISINGI NA KANUNI ZA MAANDALIZI ZISIZOEPUKIKA Kabla ya kuingia katika uchambuzi wa mambo yanayomuhusu mwanamke, na kujibu masuali na mishikeli hatuna budi kwanza tutaje misingi na kanunu ambazo ni muhimu katika kila utafiti unaomuhusu mwanamke kisheria. Msingi wa kwanza: Ubinadamu kwa mwanamme na mwanamke, hakika ya wawili hao wameumbwa kwa asili.

Ufafanuzi

QUR_ANI INATOSHA

QUR_ANI INATOSHA QUR_ANI INATOSHA Kuna kauli inayosemwa na baadhi ya Waislamu kuwa Qur-ani inatosha  kuhukumu mambo ya Waislamu  yanayohusiana na dini. Hivi kweli kauli hiyo ni sahihi? wafuasi wakweli wa Mwenyeezi Mungu, ni wale wenye kuyafanyia amali maagizo ya Mola wao, watu hao hutii yale yaliyomo ndani ya Qur-ani, na vile vile hutii amri za Mwenyeezi Mungu na Mitume yake. Watu ambao husema :- حسبنا کتاب الله. "Kitabu cha Mwenyeezi Mungu kinatosha, kwa hakika wameipinga kauli ya Mwenyeezi Mungu, na hawakuzifanyia amali Aya za Mwenyeezi Mungu.

Ufafanuzi

SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO NO.3

SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO NO.3 SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO NO.3 5. ushujaa. Katika makala zilizopita tulielezea kuhusiana na sifa wanazotakiwa makhalifa kuwa nazo. katika makala hii tutaendelea na mada yetu inayohusiana na maudhui hayo hayo.katika maelezo yaliyopita tulielezea sifa ya pili wanayotakiwa Mitume kuwa nayo, nayo ni uadilifu, tukiendelea na mada yetu katika kipengele hiki tutaelezea sifa ya tatu, nayo ni kutafakari katika kuiongoza jamii, miongoni mwa nyadhifa anazotakiwa kiongozi wa jamii ya Kiislamu, au  hata isiyo ya kiislamu kuwa nazo ni kuwa yeye anatakiwa azingatie maslahi na manufaa ya watu wa jamii hiyo anayoiongoza, na yeye ndiye anayeweza kutoa amri ya kuwa watu wapigane vita, au wakubali suluhu,na katika hatua ya mwanzo, yeye ndiye mwenye hiyari na anayeweza kuitumia mali ya Baytul mali kutokana na maslahi ya jamii, basi wadhifa huo mkubwa ni lazima apewe mtu anayestahiki kuwa khalifa baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). kwa faida zaidi ungana nami mpaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO NO.2

SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO NO.2 SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO No2 3. kufikiri na kutafakari katika kuiongoza jamii. katika maelezo yaliyopita tulielezea sifa ya pili wanayotakiwa Mitume kuwa nayo, nayo ni uadilifu, tukiendelea na mada yetu katika kipengele hiki tutaelezea sifa ya tatu, nayo ni kutafakari katika kuiongoza jamii, miongoni mwa nyadhifa anazotakiwa kiongozi wa jamii ya Kiislamu, au  hata isiyo ya kiislamu kuwa nazo ni kuwa yeye anatakiwa azingatie maslahi na manufaa ya watu wa jamii hiyo anayoiongoza, na yeye ndiye anayeweza kutoa amri ya kuwa watu wapigane vita, au wakubali suluhu,na katika hatua ya mwanzo, yeye ndiye mwenye hiyari na anayeweza kuitumia mali ya Baytul mali kutokana na maslahi ya jamii, basi wadhifa huo mkubwa ni lazima apewe mtu anayestahiki kuwa khalifa baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). kwa faida zaidi ungana nami mpaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO

SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO 2- UADILIFU katika maelezo yaliyopita tulielezea kuhusu sifa wanazotakiwa Mitume kuwa nazo, na tukaelewa kuwa moja katika sifa hizo ni elimu, tukiendelea kuelezea sifa nyengine, sifa ya pili wanayotakiwa Mitume kuwa nayo ni uadilifu, Mitume wanatakiwa pindi wanapotoa hukumu za kiislamu, au wanapomhukumu mtu wasihukumu kutokana na yale wanayoyapenda katika nafsi zao, yaani wasihukumu kutokana na matamanio yao ya kibinafsi, bali wahukumu kutokana na yale ambayo Mola wao amewaamrisha, na wala wasihukumu kwa kutegemea vyeo vyao binafsi au kutokana na sehemu waliyonayo katika jamii, bali wahukumu kwa kutegemea ridhaa ya Mola wao. kwa faidi zaidi ungana nami mpaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

UWIANO ULIOPO BAINA YA QUR_ANI NA AHLULBAYT (A.S)

UWIANO ULIOPO BAINA YA QUR_ANI NA AHLULBAYT (A.S) UWIANO ULIOPO BAINA YA QUR_ANI NA AHLULBYT (A.S) Natija inayopatikana katika somo hilo ni kuwa,ikiwa kuna mtu au kundi lolote lile lenye madai ya kuwa kitabu cha Qur-ani kinatosha, au kupinga amri za Mitume ya Mwenyeezi Mungu,kundi hilo au mtu huyo atakuwa amepinga maamrisho ya Mola wake. na kwa hakika atakuwa hakufanya amali ya yale yaliyomo ndani ya Qur-ani. Basi mtu huyo yuko mbali na Mwenyeezi Mungu. ili kufadikka zaidi juu ya somo hili,ungana nami katika makala hii mpaka tamati.  

Ufafanuzi

ALLAH (S.W) HAJAFANANA NA KITU

ALLAH (S.W) HAJAFANANA NA KITU  ALLAH (S.W) HAJAFANANA NA KITU Miongoni mwa sifa nyengine za Allah (s.w) ni:- MWENYEEZI MUNGU SI KIUMBE, HANA KIWILIWILI NA KATU HAONEKANI. Sisi tuna imani ya kuwa; Mwenyeezi Mungu haonekani kwa macho katu, kwa sababu kuona kwa macho kunamaanisha kuwa Mwenyeezi Mungu ni kiumbe aliye na kiwiliwili, aliye katika sehemu maalumu, au umbo maalumu, hali ya kwamba sifa hizoo ni sifa za viumbe vilivyoumbwa na Mwenyeezi Mungu, hali ya kwamba ubora na utukfu wa sifa za Mwenyeezi Mungu uko juu zaidi, kiasi ya kwamba haiwezekani kumfananisha Yeye na sifa za viumbe, kwa hivyo hatuwezi kumsifu Mwenyeezi Mungu kwa sifa za viumbe vyake, kwa hiyo kuwa na itikadi ya kumuona Mwenyeezi Mungu sio sahihi, na itikadi hiyo ni miongoni mwa aina fulani za shirki, na huko ndio kumshirikisha Mwenyeezi Mungu.

Ufafanuzi

DHATI YAKE ALLAH (S.W)

DHATI YAKE ALLAH (S.W)   DHATI YAKE ALLAH (S.W)  DHATI YA ALLAH (S.W) IMETAKASIKA NA ISIYOKUWA NA MWISHO. Sisi tunaamini kuwa dhati  ya Mwenyeezi Mungu imeenea sehemu zote, naye hana mwanzo wala mwisho, dhati hiyo inaonekana katika elimu yake, qudra ya utukufu wake, kubakia kwake milele katika sehemu zote na zama zote, na kwa sababu hiyo basi ndio tukasema kuwa Mwenyeezi Mungu hana sehemu maalumu wala kipindi maalumu, kwa sababu sehemu au nafasi na zama zina kiwango maalumu, ijapokuwa Mwenyeezi Mungu hana sehemu maalumu wala zama maalumu lakini Yeye yuko katika sehemu na zama zote, kwa sababu dhati ya utukufu wake iko juu zaidi kuliko sehemu na zama.

Ufafanuzi

FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA

FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO 1. Kauli muhimu za Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni kuwalingania watu kuamini Mola mmoja na kuwakumbusha maisha baada ya mauti. Jitihada kubwa walizozifanya Mitume baada ya kuwalingania watu kuabudu Mola mmoja ni kuihuisha Siku ya Kiama katika nyoyo za watu. katika makala iliyopita tulielezea kuhusiana na umuhimu wa siku ya kiama katika makala hii tutaendelea na kuelezea faida za kuikumbuka siku hiyo takatifu. hivyo endelea kuwa sambama ba nami mpaka tamati mwa makala hihi.

Ufafanuzi

FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO.2

FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO.2 FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO. 2. Kauli muhimu za Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni kuwalingania watu kuamini Mola mmoja na kuwakumbusha maisha baada ya mauti. Jitihada kubwa walizozifanya Mitume baada ya kuwalingania watu kuabudu Mola mmoja ni kuihuisha Siku ya Kiama katika nyoyo za watu. katika makala iliyopita tulielezea baadhi ya faida za kuikumbuka siku ya Kiama katika makala hii tutaendelea kuelezea faida nyengine.

Ufafanuzi

FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO.3

FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO.3 FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO.3. Kauli muhimu za Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni kuwalingania watu kuamini Mola mmoja na kuwakumbusha maisha baada ya mauti. Jitihada kubwa walizozifanya Mitume baada ya kuwalingania watu kuabudu Mola mmoja ni kuihuisha Siku ya Kiama katika nyoyo za watu. katika makala iliyopita tulielezea kuhusu baadhi ya faida za kuikumbuka siku ya Kiama, katika makala hii tutaendelea kuelezea faida nyengine. hivyo endelkea kuwa sambamba nami mpaka tamati mwa makala hii.,

Ufafanuzi

KIAMA NA WATENDAO MATENDO YA KHERI

KIAMA NA WATENDAO MATENDO YA KHERI KIAMA NA WATENDAO MATENDO YA KHERI Kauli muhimu za Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni kuwalingania watu kuamini Mola mmoja na kuwakumbusha maisha baada ya mauti. Jitihada kubwa walizozifanya Mitume baada ya kuwalingania watu kuabudu Mola mmoja ni kuihuisha Siku ya Kiama katika nyoyo za watu. Katika makala iliyopita tulimalizia kwa mada ya faida za kuikumbuka siku ya Kiama. katika makala hii tutazungumzia kuhusiana na matendo ya kheri wanayoyatenda wale walio na imani na siku hiyo. hivyo endelea kuwa sambamba nami mpaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

KUWEPO KWA MOLA MTAKATIFU

KUWEPO KWA MOLA MTAKATIFU  KUWEPO KWA MOLA MTAKATIFU Sisi tunaamini kuwa Mwenyeezi Mungu ndiye muumbaji wa vitu vyote, na athari ya utukufu na elimu yake inaonekana kwa uwazi kabisa katika kila kiumbe ulimwenguni, katika umbile la mwanaadamu, wanyama, mimea, katika nyota ziliopo mbinguni, na katika kila kitu ulimwenguni. Sisi tuna itikadi ya kuwa; kila tukifikiri na kutafakuri zaidi kuhusiana na siri ya viumbe vyote duniani, tutafahamu utukufu wa elimu na qudra ya dhati ya Mola Mtakatifu, na kwa kuonekana maendeleo ya elimu na taaluma ya wanaadamu ya kila siku kunapatikana na kufunguka elimu mpya kutokana na elimu na hekima zake Allah (s.w), na tafakuri za wanaadamu zinazidi kukua na kuenea kwa wingi zaidi, na tafakuri hizo ndio chanzo cha kuwa karibu naye Mola mtakatifu na kunufaika na upeo wa nuru ya utukufu wake.

Ufafanuzi

MATAWI YA TAWHIYD

MATAWI YA TAWHIYD MATAWI YA TAWHIDI NO.1 Sisi tuna itikadi ya kuwa tawhiyd ina matawi mbali mbali, kama vile: A: TAWHIYD KATIKA DHATI YAKE ALLAH (S.W). Yaani dhati ya Allah (s.w) ni moja, naye ni mmoja tu, asiyefanana na kitu chochote ulimwenguni. B: TAWHIYD KATIKA SIFA ZAKE ALLAH (S.W). Tawhiyd katika sifa za Mwenyeezi Mungu, yaani sifa zote za Mwenyeezi Mungu, mfano elimu, Qudra na uwezo, ubakiaji wa milele wa Allah (s.w), na sifa nyengine nyingi zote ziko katika dhati yake Allah (s.w), sio kama sifa za viumbe, kwani sifa za viumbe haziko ndani ya udhati wa viumbe bali ziko nje ya viumbe, ama ni lazima tuzingatie kuwa; dhati hiyo ya sifa za Mwenyeezi Mungu inahitajia tafakuri na mazingatio ya kifikra. nk..

Ufafanuzi

SIKU YA KIAMA

SIKU YA KIAMA SIKU YA KIAMA. Kauli muhimu za Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni kuwalingania watu kuamini Mola mmoja na kuwakumbusha maisha baada ya mauti. Jitihada kubwa walizozifanya Mitume baada ya kuwalingania watu kuabudu Mola mmoja ni kuihuisha Siku ya Kiama katika nyoyo za watu. Na Allah (s.w) ameielezea siku hiyo ya Kiama kuwa ndio madhumuni muhimu ya kuwapa Mitume wake Utume. Pale aliposema:- رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِى الرُّوحَ مِنْ اَمْرِهِ عَلـٰي مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنذِرَ يَوْمَ التَّلاَقِ[1] Yeye ndiye Mwenye vyeo vya juu, Mwenye A'rshi. Hupeleka Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake, ili kuonya kwa Siku ya Mkutano.

Ufafanuzi

TAWHIDI NI KIINI CHA ELIMU

TAWHIDI NI KIINI CHA ELIMU TAWHIYD NI KIINI CHA ELIMU NA MAFUNZO YOTE YA UISLAMU Sisi tuna itakidi ya kuwa; mambo muhimu yanayohusiana na elimu na taaluma bora ya Mwenyeezi Mungu ni Tawhiyd, na kuwa na imani ya kuwepo Mola mmoja aliyetakasika, kwa hakika Tawhiyd sio msingi miongoni mwa misingi ya dini tu, bali, mbali ya kuwa Tawhiyd ni msingi wa dini vile vile ni kiini cha itikadi zote za Kiislamu, na tunaweza kusema kuwa; Misingi na matawi ya Kiislamu  yamejikusanya katika misingi ya Tawhiydi, kila kipengele miongoni mwa vipengele vya Islamu kumezungumzwa masuala ya Tawhid, na kuwa na imani na Mola mmoja, tawhiydi katika sifa na matendo ya Mwenyeezi Mungu, Tawhiyd katika malengo mamoja walikuja nayo Mitume walipokuwa wakilingania nyumati zao, Tawhiyd katika dini moja miongoni mwa dini za Mwenyeezi Mungu, Tawhiydi katika kibla na vitabu vya mwenyeezi Mungu, Tawhitdi katika hukumu na sheria za Mwenyeezi Mungu kwa wanaadamu wote, na hatimae Tawhiyd kwa Waislamu wote na tawhiyd kwa siku ya Kiama, na kwa sababu hiyo basi, Qur-ani takatifu inabainisha kuwa upotoshaji wowote ule utakaofanywa katika tawhiyd ya Mwenyezi Mungu ni uovu usiosamehewa na ni shirki kubwa.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini