Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Familia na watoto

YENYE KUHATARISHA NYUMBA ( 3 )

YENYE KUHATARISHA NYUMBA   ( 3 )

YENYE KUHATARISHA NYUMBA ( 3 ) MUZIKI NA NYIMBO Miongoni mwa yenye kuzoeleka katika majumba yetu ni mziki. Kwa kweli mziki umeenea kila pembe ya dunia kiasi ambacho unawaumiza Waislamu wengi kimwili na kiakili bila ya kujijua. Kila mtu amekabiliana na hali ambayo humuingiza kusikiliza muziki ama kwa hiari au kwa lazima. Kuongezeka umaarufu wa muziki kunahatarisha sana majumba ya Waislamu na hatimae kutumbukia katika balaa hilo usiku na mchana. Ukweli ni kuwa muziki unaathiri sana mioyo ya Waislamu na kuishughulisha akili kwa mambo ya kipuuzi. Tunatumia muda na pesa nyingi katika kununulia CD za majimbo yasiyo na faida, zana za miziki, na hata kuwatumbukiza watoto wetu kwa vifaa (toys) mbali mbali vilivyojaa miziki; Tunajitia makosani na kuuporomoa itikadi sahihi ya Muislamu. Kuna dalili tosha katika Quraan na Sunnah zenye kuonyesha uharamu wa muziki.

Ufafanuzi

YENYE KUHATARISHA NYUMBA ( 2 )

YENYE KUHATARISHA NYUMBA   ( 2 ) YENYE KUHATARISHA NYUMBA  ( 2 ) UVUTAJI SIGARA Uvutaji wa sigara umeenea na kushamiri dunia nzima licha ya kuwa madhara yake yapo wazi.  Baadhi ya Waislamu wametumbukia katika balaa hili na kuziathiri nyumba zao bila ya kujijua. Kuna sababu tosha zenye kuonyesha uharamu wa jambo hili kwa Muislamu.  Sigara ina athari sana katika dini, afya, mazingira, familia, rasilimali na mengineyo. i. MADHARA KATIKA DINI Sigara inaathiri  ibada ya mja na inapunguza malipo ya ibada hiyo.  Kwa mfano ibada ya sala ambayo ni nguzo muhimu ya Muislamu;   Kutokana na hadithi iliyosimuliwa na wengi; Amesema Mtume Swalla Llahu Alayhi wa Ssalam  “Mwenye kula Kitungu maji au thawm, basi asiukaribie Msikiti wetu na akae nyumbani” [Bukhari na Muslim] Tunaona makatazo yamekuja kutokana na harufu mbaya inayotokana na vitu hivyo amabayo huwakirihisha watu pamoja na Malaika katika nyumba za Allaah (Misikitini).    Bila ya shaka mdomo wa mvutaji sigara una harufu mbaya zaidi  kuliko vitunguu, ima huwakera watu na Malaika kwa harufu hiyo au kukosa fadhila za sala ya jamaa msikitini kwa mwanamme.

Ufafanuzi

YENYE KUHATARISHA NYUMBA

YENYE KUHATARISHA NYUMBA MAMBO YA KUZINGATIA HASA KWA KINA MAMA Miongoni mwa mambo yenye kuporomoa Uislamu katika majumba ya Waislamu ni udhaifu wa baadhi ya kinamama kuupuuza au kutoyatambua mafunzo muhimu yanayowahusu ambayo dini yetu yameyaweka wazi. Miongoni mwa hayo ni haya yafuatayo: i. Kudhihirisha Mapambo: Kawaida, wanawake huwa na mvuto wa kimaumbile. Hivyo Uislamu umeweka sheria maalum juu ya kuhifadhi maumbile hayo, heshima, staha pamoja na hadhi zao. Suurat Al-Ahzab: 59 Allaah Subhaanahu Wata'ala Anatueleza: Ewe Mtume! Waambie wake zako na binti zako na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri shungi zao, kufanya hivyo kutapelekea wepesi wajuulikane (kuwa ni watu wa heshima) ili wasiudhiwe. Ni mazoea ya wanawake wengi wanapotaka kutoka au kupata wageni majumbani mwao hudhihirisha mapambo yao yakiwemo maumbile yao kwa nguo za wazi au za kubana, manukato pamoja na mapambo mengine. Hali hii inaweza kusababisha vishawishi vingi, fitina na mtafaruku katika familia. Ni lazima tuwe waangalifu ni nani waliotuzunguka hasa wale wasiotakikana kuona mapambo hayo (wasiokuwa mahrim). Suuratu Nnuur: 31 Allaah Subhaanahu Wata'ala Anatuhimiza: Na waambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika. Kujistiri kwa hijabu ya ki shari'ah kunapelekea kupata ridhaa ya Allaah Subhaanahu Wata'ala na kutii amri Yake, kujitakasa pamoja na kuheshimika na wengine.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini