Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Hadithi na elimu zake

MAKHALIFA KUMI NA MBILI KATIKA VITABU VYA PANDE MBILI

MAKHALIFA KUMI NA MBILI KATIKA VITABU VYA PANDE MBILI

BAADHI YA WANAZUONI WA AHLISUNA WA KISASA AMBAO HAWAJISHUGHULISHI NA KUFANYA UTAFITI WANADHANI HADITHI HII IPO KWA SHI'AH TU. NA WANABWETEKA NA KUNG'ANG'ANA NA HADITHI YA KHULAFAU RASHIDUNA WANNE, AMBAYO HAIPO HATA KWENYE VITABU VYA AHLISUNA Kuna hadithi inasema: Katika ummah wangu kutakuwa na Maamiri kumi na mbili. Kuna kauli nyingine inasema: Kuna Makhalifa waongofu kumi na mbili. Kuna kauli nyingine inasema: Kutakuwa na Maimamu kumi na mbili. Kuna kauli nyingine inasema: kutakuwa na watawala kumi na mbili. Kwa hiyo, Mtukufu Mtume saww anaposema: Makhalifa kumi na mbili wa kwanza wao ni Ally Bin Abi Twalib as na wa mwisho ni Imamu Muhammad Bin Hassani Al Mahdy as. Mtukufu Mtume saww akisema: Kutakuwa na Maamiri kumi na mbili, wa kwanza wao ni Ally Bin Abi Twalib as na wa mwisho wa Muhammad bin Hassani Al Mahdy as. Akisema: Maimamu watakatifu baada yangu ni kumi na mbili, wa kwanza wao ni Ally Bin Abi Twalib as na wa mwisho wao ni Muhammad Bin Hassani Al Mahdy as

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini