Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Tarehe

WATU WA TEMBO ( AS-HAB-I-FIIL )

WATU WA TEMBO ( AS-HAB-I-FIIL )

WATU WA TEMBO ( AS-HAB-I-FIIL ) Najjashi (Negus), alikuwa ni Mfalme wa Abisynnia ambaye alijichukulia jukumu la kueneza Ukristo na alifanya kila jitihada alizoziweza ili aweze kuirudisha vile ilivyo kuwa miongoni mwa watu wake na ikafuatwa na wingi wa raia zake. Alipopata habari kuwa watu kutoka sehemu mbalimbali za Ulimwenguni walikuwa wakienda Makka kuhiji huko Al Ka’abah Tukufu, basi naye aliamua kuvumbua jambo ambalo litawavutia watu kutokwenda Makkah kuizuru Al Ka’abah Tukufu na badala yake waende nchini mwake. Hivyo, basi yeye alijenga Kanisa moja kubwa katika Sana’, mji uliopo Yemen na kuipamba vizuri kwa kila kitu cha kuvutia zikiwemo mazulia, mapazia n.k. Kwa hakika lilikuwa ni jambo la kuvutia sana kwa mtu yeyote aliye angalia kwa kuona ufundi wa kistadi uliotumika katika ujenzi wake. Najjashi alifikiria kuwa baada ya kuona maajabu ya ujenzi huo wa Kanisa watu hawatakwenda tena Makkah kuzuru Al-Ka’abah Tukufu na badala yake watakwenda Sana’ kuzuru hilo Kanisa, na vile vile watu wa Makkah pia watakuja kuhiji hapo Sana’, Yemen. Pamoja na hayo yote watu wa Makkah hawakujali chochote. Vile vile sio kwamba ni watu wa Yemen na Abisynnia tu walioisahau Makkah, laa, wao kama kawaida yao waliendelea na safari zao za kwenda mji mtukufu wa Makkah na kuzuru Al Ka’abah Tukufu.

Ufafanuzi

PEPO ( JANNAT ) YA SHADDAD

PEPO ( JANNAT ) YA SHADDAD PEPO ( JANNAT ) YA SHADDAD JE SHADDAD NI NANI … Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokwenda katika Mi’raj alikutana na Malakul Mauti. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza : “Je ni wakatigani ambapo wewe kwa hakika ulisikitika katika kutoa roho ya wanaadamu ?” Kwa hayo Malakul Maut akajibu : “Ewe Mtume wa Allah swt ! Zipo nyakati mbili tu ambapo mimi kwa hakika nilisikitika mno wakati wa kutoa Roho nazo ni, kwanza kulikuwa na jahazi moja iliyokuwa baharini ikiwa na wasafiri walikuwamo humo, na Allah swt aliniamrisha kuipindua jahazi hiyo na kuzitoa roho zote za wasafiri waliokuwamo isipokuwa mwanamke mmoja aliyekuwa ana mimba. Nami nikafanya hivyo hivyo nilivyoamrishwa. Mwanamke huyo aliweza kuelea kwa msaada wa ubao alioupata wakati wa kuzama. Wakati mwanamke huyo anaelea, alimzaa mtoto, ndiye aliyeitwa Shaddad. Alipomzaa mtoto huyo, mama huyo akafa( hapa niliposikitika wakati wa kuitoa roho ya mama huyu) na mtoto akabakia peke yake majini juu ya ubao, ambapo kwa amri za Allah swt aliweza kufika salama u salimini hadi nchi kavu (kisiwa kilichokuwapo karibu).Hapo Allah swt alimwamrisha Swala mmoja kumnyonyehsa maziwa mtoto huyo kwa muda usipungua miaka miwili. Ulifika wakati ambapo kulitokezea wasafiri kisiwani hapo na walipomwona mtoto huyo na alivyokuwa mzuri, walishauriana kumpelekea mfalme kwani alikuwa hana mtoto. Na walifanya hivyo, na Mfalme alimpenda mtoto huyo na kumchukua kama mtoto wake ….. Mtume Adam a.s. tangu aje duniani humu ilipofika miaka 2647 ndipo Mtume Hud a.s. alipozaliwa na kulipofika miaka 2700 ndipo Shaddad bin ‘Aad alipokuwa Mfalme na ni Mfalme huyu ambaye ametengeneza mfano wa Jannat (Peponi) yenye bustani za kupendeza humu duniani. Humu yeye alijenga majumba ya kuvutia na kupendeza, na aliweka wajakazi warembo:wasichana kwa wavulana kutoka sehemu mbalimbali humu duniani ambao kwa hakika waliifanya pepo yake ipendeze na kuvutia. JE KUNA MTU ALIYEBAHATIKA KUIONA PEPO HIYO? Katika zama za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuna mtu mmoja aitwaye ‘Bwana ‘Abdullah bin Kalaba ndiye aliyebahatika kuiona. Na hapa tunaelezea vile inavyopatikana katika vitabu vya historia. WASEMAVYO WANAHISTORIA “Katika Bara la Uarabuni kulikuwa na Shakhsiyyah moja aliyekuwa akiitwa ‘Bwana ‘Abdullah bin Kalaba ambaye alikuwa na Ngamia wake aliyekuwa ametoroka na kupotelea katika majangwa ya ‘Aden na katika kumtafuta huyo ngamia wake alifika katika majangwa ambapo aliuona mji mmoja ukivutia. Mji huo ulikuwa umezungukwa na ngome. Ndani ya mji huo kulikuwa na majumba ya kupendeza na yenye kuvutia sana. Na juu ya kila jengo kulikuwa na bendera zilizokuwa zikipepea. Yeye anasema kuwa alifanikiwa kuingia ndani ya mji huo. ‘BWANA ‘ABDULLAH ANAELEZEA ALIVYIONA PEPO YA SAHADDAD “Mimi niliteremka chini kutokea ngamia wangu na nikamfunga katika nguzo mojawapo. Nikauchukua upanga wangu nikawa ndani ya ngome hiyo. Milango yake ilikuwa ni madhubuti na ya kupendeza sana kiasi kwamba kamwe nilikuwa sijawahi kuona kabla ya hapo. Milango ilikuwa imetengenezwa kwa ubao mzuri sana na manukato mazuri sana na ufundi uliotumika ulikuwa ni wa utalaamu wa hali ya juu sana na juu ya mbao zake kulikuwa kumepachikwa Yaqut za rangi mbalimbali. Ukiangalia chumba kimoja utakisahau chumba cha pili katika ngome hiyo. Madirisha yake yalikuwa yametengenezwa kwa dhahabu na shaba, ukiona milango , kuta na sakafu yake ilivyokuwa iking’ara na kwa hakika kila kitu humo utakachokiona utastaajabika mno.” ‘Bwana ‘Abdullah alipoyaangalia majengo hayo yaliyokuwa mazuri na yenye kuvutia alishangazwa kuona kuwa hapakuwapo na mtu yeyote, na alijaribu kusonga mbele akaona miti ambayo imejaa maua ikiwa inapeperushwa na upepo mzuri sana. Na chini mwake kulikuwa na mito iliyokuwa ikitiririsha maji. Kwa hakika hii ndiyo ile Jannat ambayo Allah swt ametupa habari zake. Basi mimi kwa hayo nilimshukuru Allah swt kwa kunijaalia bahati hiyo. Mimi niliokota vipande vidogo vidogo vyenye harufu nzuri mno ya Mishk na Ambar. Na hapo nikawaza kuwa sasa itabidi nitoke zangu nje kwa haraka. Nilipofika katika mji wa Yemen huko niliwasimulia watu kuhusu Jannat hii. Kwa hakika nilishangazwa kuona kuwa habari zangu hizi zilienea kila mahali kama upepo.

Ufafanuzi

MALAIKA: HARUT NA MARUT

MALAIKA: HARUT NA MARUT MALAIKA: HARUT NA MARUT Imepokelewa riwaya kutoka kwa Imam Muhammad al-Baquir a.s. kuwa: Baada ya kifo cha Mtume Sulayman bin Daud a.s., Ibilisi alitengeneza uchawi na kuuviringa na nyuma yake aliandika kuwa mzigo huu umetengenezwa na Asif bin Barkhiyyah kwa ajili ya ufalme wa Mtume Suleyman, na kwamba imetolewa kutoka hazina ya ilimu. Na kwa nguvu zake kila jambo linawezekana. Na baada ya hapo aliifukia chini ya kiti cha Mtume Sulayman a.s. Na baadaye aliifukua chini ya kiti hicho na kuidhihirisha mbele ya watu wa zama hizo. Kwa kuyaona hayo, wale waliokuwa Makafiri walianza kusema kuwa Mtume Suleyman a.s. aliweza kuwatawala kwa uchawi lakini wale waliokuwa Mumin walikuwa wakisema kuwa Mtume Sulayman a.s. alikuwa ni Mtume wa Allah swt na mwenye taqwa. Allah swt anatuambia kuwa ni Sheitani ndiye asemaye kuwa Mtume Suleyman a.s. alikuwa ni mchawi. Na jambo hilo ndilo walilolifuata na kuliamini Mayahudi. Lakini Mtume Suleyman a.s. kamwe hakufanya tendo lolote la kukufuru au la ushirikina hivyo kamwe hawezi kuwa mchawi. Wale wanaohalalisha uchawi ni makafiri kwa sababu Masheitani walikuwa wakifanya uchawi na kuwafundisha watu uchawi na ushirikina. Baada ya kupita zama za Mtune Nuh a.s., kulikuja zama moja ambamo wakazi wake walikuwa wakijishughulisha mno na mambo ya uchawi na ushirikina, kwa sababu ya kufuata imani hizo zilizopotofu, kulikuwa kukitendeka matendo maovu kabisa. Hivyo wakazi walikuwa wameupuuzia Uislamu, na kwa hayo Allah swt aliwatuma malaika wawili waliokuwa wakiitwa Harut na Marut, ambao walitumwa katika mji uitwao Babul, katika maumbile ya mwanadamu ili waweze kuwazuia wanadamu wasiendelee na uchawi na ushirikina uliokuwa umepindukia kiasi. Malaika hao walitii amri ya Allah swt na walimwelezea Mtume wa zama hizo kuwa uwafundishe mambo fulani fulani wakazi wako ili waweze kujiepusha na uchawi na ushirikina huo uliokuwa umewapotosha kabisa. Basi Mtume huyo aliwaambia watu wake kuwa wajifunze mafunzo hayo makhsusi ili waweze kujiepushe na uchawi na kamwe wasiwatendee chochote wenzao. Allah swt anatuambia kuwa katika mji huo wa Babul kulikuwapo na Mayahudi ambao wao kwa hakika walikuwa wakitenda kinyume na kile walichokuwa wakiambiwa na Mtume huyo, yaani wao badala ya kuutokomeza uchawi, wao ndio wakawa waabudu wa uchawi na wakawa wakifanya uchawi. Malaika wakawaambia sisi tunawafundisheni haya kwa ajili ya kutaka kuwajaribu na kuwajua wale waliona imani ya kurudi kwa Allah swt na hivyo kujiepusha na uchawi. Na kutaka kuwatambua wale walioasi na kutumia ilimu hii kwa ajili ya kuwadhuru wengine.

Ufafanuzi

MAISHA YA MTUME SALEH

MAISHA YA MTUME SALEH MAISHA YA MTUME SALEH Mtume Saleh a.s. aliitwa: Mtume Saleh a.s. bin Abud bin Asif bin Nasikh bin Abud bin Hadir bin Thamud bin Amir bin Sam bin Nuh. Kabila lake lilikuwa likiishi mipaka ya Kusini ya Syria katika milki iliyokuwa ikijulikana kama Al-hijr au Al-Hajar na ilijulikana kama Wadiul-Qura. Mtume Saleh a.s. alikuja baada ya Mtume Hud a.s. na alitokana na kizazi cha tisa cha Mtume Nuh a.s. URITHI Baada ya kuangamiza Allah swt Qaumu A'ad ambao hawakuyasikiliza maneno ya Mtume wao Hud a.s. na baada ya kufa hao wote ikabaki ardhi yao bila majumba wala wakazi wala mimea hata wanyama na baada ya haya yote Allah swt aliirithisha ardhi yao kwa Qaum nyingine nao ni Qaum Thamud. Wakaja Qaumu Thamud mahali pakawa Qaum-u-‘Aad Allah swt aliwaneemesha neema nyingi kuliko Qaum ‘Aad. Walijenga Qaum Thamud majumba kati ya majabali na wakalima mabustani na makonde na wakatoboa mito lakini pamoja na masikitiko makubwa hazikuwa akili zoa zina maendeleo kuliko Qaum iliyotangulia. Ni hao hao ambao waliabudu masanamu na mawe na wakadhani kwamba neema yao haitoondoka na wala haitatoweka. UJUMBE Na mbele ya utakafiri huu na ujinga Allah swt alimtuma kwao mwanamme miongoni mwao anayeitwa Mtume Saleh a.s. na yeye miongoni mwa watukufu wao na mwenye akili katika wao ambaye alimuamini Allah swt wake na Allah swt alimchagua yeye ili awaongoe hawa Majahili waliopotea akawalingania wao kwenye ibada ya Allah swt na akatilia mkazo na akawaimiza wao juu ya Tawhid yaani kumpwekesha Allah swt na kuacha kumshirikisha Yeye ni Yeye ambaye aliwaumba wao na akawaumbia wao ardhi na akawapa wao miongoni mwa fadhila Zake na neema Zake kisha akawakataza wao kuabudia masanamu ambayo wameyatengeneza wao wenyewe. Kwani hayo masanamu hayadhuru wala hayanufaishi chochote na wala hayamtoshelezi mtu kutoka kwa Allah swt chochote kisha akawakumbusha wao kwamba yeye ni miongoni mwa wao na yeye anapenda kuwanufaisha wao na wanapojipatia maslaha yao na akawaamrisha wao wamtake msamaha Allah swt na watubu kwake Yeye kwani yeye ni mwenye kusikia na mwenye kujibu na anakubali toba kwa yule mwenye kutaka msamaha kwake.

Ufafanuzi

MAISHA YA MTUME LUT

MAISHA YA MTUME LUT MAISHA YA MTUME LUT Mtume Lut a.s. alikuwa ni ndugu wa kijamaa wa Mtume Ibrahim a.s. yaani mtoto wa mamake mdogo na dada yake Mtume Lut a.s. aliolewa na Mtume Ibrahim a.s. Tendo ovu kabisa lililokuwa katika ukoo wa Mtume Lut a.s. ni tendo la Ulawiti 1 TABIA MBAYA Ulizidi ufisadi katika mji mmoja miongoni mwa miji ya zamani kiasi kwamba atakapoona mtu ufisadi unatendwa na mmoja kati yao basi hakatazwi na mtu mwingine atakapo shuhudia heri inafanywa na ndugu yake basi humkemea mpaka aache heri anayoifanya. Kila mtu katika kijiji hicho alikuwa katika upotevu na uovu na ujinga, hawasikii wala hawasikilizi ilikuwa ni mamoja kwao apatikane mtu wa kuwapa mawaidha wao au mtu wa kuwanasihi wao kulikuwa hakuna tofauti yoyote. Walikuwa ni watu waovu na wabaya zaidi na wenye tabia mbaya miongoni mwa watu, uhai wao (ulikuwa ni khiana na tabia mbaya) na wote hao wakati huo walikuwa ni wenye tabia mbaya sana na nia mbaya. Lakini unaonaje ewe msomaji je walijizuia na maovu yao haya au walizidi katika upotevu na ufijari na madhambi ? KUENEA MAMBO YA HARAMU Ilikuwa kama kwamba nafsi zao hazikutosheka na kule kusema uongo na kuwa na tabia mbaya na ghadr na mengineyo mengi, wakasababisha na kuleta mambo ya unyama ambayo hakutangulia kufanya yeyote kabla yao. Je ni mambo gani hayo? Hakika waliacha mambo aliyoyahalalisha Allah swt kwao kwa wanawake na wakawa hawaoi wanawake ! Wakawaacha wake zao na kuanza maovu ya kuingiliana na wanaume wenzao. Jambo ambalo Allah swt aliliharamisha kabisa. Na laiti wao wangesitiri haya maovu au wakajaribu kujiepusha kutoka katika maovu haya au kujiweka mbali nayo ingelikuwa afadhali lakini wao walijitumbukiza katika mambo hayo na wakawa wanayatangaza wazi wazi mpaka ukaenea ufisadi na kukaenea mambo ya haramu na zikawa tabia zao mbaya ni rahisi kiasi kwamba zikawa zimefikia daraja kubwa sana na yote hayo yalikuwa ni madhambi na ufisadi wala hawezi mtu yeyote kuyafanya wala kufikiria binaadamu au kupiga picha ya binaadamu katika akili yake.

Ufafanuzi

URITHI WA IMAM ALI (A.S.)

URITHI WA IMAM ALI (A.S.) URITHI WA IMAM ALI (A.S.) MUHTSARI Qur’ani imetilia umuhimu mambo yote yanayohusu maisha na mus- takabali wa mwanadamu, hivyo Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake nao wakafuata njia hiyo ya Qur’ani, wakisimama imara kutafsiri makusudio ya Qur’ani na kubainisha ishara na alama zake. Suala la wema na uovu ni suala la mwanzo kabisa walilotilia umuhimu na kuliashiria, hivyo wakafafanua kipimo cha wema na uovu huku wakifafanua alama na mwonekano wa mtu mwema na mtu mwovu. Waligusia vinavyosababisha wema na uovu, hivyo kwa maelezo hayo wakatoa mfumo kamili wa ukamilifu wa mwanadamu katika maisha.

Ufafanuzi

SIFA ZA IMAM ALI (A.S.) NA MWONEKANO WAKE

SIFA ZA IMAM ALI (A.S.) NA MWONEKANO WAKE SIFA ZA IMAM ALI (A.S.) NA MWONEKANO WAKE URAFIKI MUHTASARI Huruma ya kutekeleza ahadi ni huruma ya kina kwa Imam Ali (a.s.), huruma ambayo ilikuwa imejenga moyo wake huku ikidhihirika katika matendo na mienendo yake, hiyo ni hata mbele ya adui yake. Akitarajia kuwaongoza waliopotea na kuwarudisha katika njia sahihi wale waliokengeuka. Ama kuhusu uadilifu ni kuwa laiti kama ungejitokeza kwa mtu basi angekuwa ni Ali bin Abu Talib (a.s.) na wala si mwingine, kwani alikuwa ni nguvu kali ya kutekeleza uadilifu kwa watu wote. Alikuwa ni mjuzi anayemjua mwanadamu, jamii na kanuni za Mwenyezi Mungu, hivyo kidole chake hakikuacha haki na uadilifu kwa maana yote ya uadilifu na vipengele vyake vyote katika maisha. Kila kitu katika utu wa Imam Ali (a.s.) kimekamilika na chenye muundo mmoja, kwani hatupati tofauti yoyote katika sifa zake na mwonekano halisi wa utu wake, hivyo akastahiki kuwa alama kati ya alama za utukufu wa Mwenyezi Mungu na mfano bora kwa wanadamu wote katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kujenga imani ya Mwenyezi Mungu, kifikira, kimwenendo na kihuruma, hivyo yeye ni mfano mwema wa mtawala shupavu na mtawaliwa mwaminifu mtiifu, na yeye ni sura halisi ya nia njema, utiifu, ibada na nguvu ya haki. Imam Ali (a.s.) alikuwa mkarimu sana kuliko watu wote huku akiwa na mkono mkunjufu. Alikuwa na ukarimu wa hali ya juu huku akijitofautisha kwa kuwa na moyo salama usiokuwa na chuki hata kwa maadui zake, hivyo hakuridhia jambo mbadala lichukue nafasi ya ukweli, kikauli au kivitendo. Sifa zote hizi ziliungana na sifa ya kujiamini mbele ya haki kwa kiwango cha juu. Mwana wa Abu Talib alijitofautisha na wengine kwa jihadi iliyoende lea katika vipindi vyote vya maisha yake yote huku akiwa na maadili bora na mtazamo wa ndani wa makini uliyonyooka, akiwa na ubainifu safi na utambuzi wa haraka na nguvu za kupambana, hivyo akawa ni kiongozi bora na mfano wa juu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika kila sifa bora.

Ufafanuzi

MWONEKANO WA UTU WA IMAM ALI BIN ABU TALIB (A.S.)

MWONEKANO WA UTU WA IMAM ALI BIN ABU TALIB (A.S.) MWONEKANO WA UTU WA IMAM ALI BIN ABU TALIB (A.S.) MUHTASARI Imam Ali (a.s.) alijitenga kwa kuwa na sifa mahsusi ambazo zilimtofautisha na maswahaba wengine, zikamwajibisha awashinde wote waliotaka kulingana nae miongoni mwa maswahaba na wasiokuwa maswahaba. Aya za Qur’ani zimejaa fadhila hizi za pekee huku maelezo ya Mtume (s.a.w.w.) yakiashiria sifa hizi zilizomtofautisha Ali (a.s.) na wengine. Ushahidi wa maswahaba na waliokuja baada ya maswahaba unaashiria undani wa fadhila za Ali (a.s.) ndani ya umma huu japokuwa watu wengi hawakufuata uimamu wa mtu huyu mtukufu.

Ufafanuzi

DONDOO ZA MAISHA YA MBORA WA MAWASII

DONDOO ZA MAISHA YA MBORA WA MAWASII DONDOO ZA MAISHA YA MBORA WA MAWASII KIONGOZI WA WAUMINI ALI BIN ABU TALIB MUHTASARI Ali bin Abu Talib (a.s.) alitokana na asili ile ile aliyotokana nayo Mtume (s.a.w.w.) hivyo nasaba yake na nasaba ya Mtume (s.a.w.w.) ni moja. Ali (a.s.) alitofautiana na maswahaba wengine kwani hakuna shirki yoyote iliyomuingia. Kisha akawa ni mtu mahsusi kwa Mtume (s.a.w.w.) hivyo akawa akimfunza mafunzo yatokanayo na hekima za Mwenyezi Mungu na elimu ya Mola Wake, jambo ambalo hakulipata swahaba mwingine yeyote. Ali (a.s.) alidhihirisha utiifu na ufuataji kamilifu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.), akajipamba kwa maadili mazuri, akajitolea nafsi na kila lenye thamani kwa ajili ya itikadi ya Uislamu. Mwenyezi Mungu alimteua awe wasii wa Mtume Wake (s.a.w.w.) hivyo akasimamia jukumu la uwasii kwa ukamilifu mpaka adui akakiri hilo kabla ya rafiki. Imam Ali (a.s.) alibeba majina na lakabu nzuri ambazo zinaonyesha jinsi alivyoshikamana sana na Mwenyezi Mungu na alivyokuwa na itikadi salama ya Mwenyezi Mungu na maadili bora mazuri.

Ufafanuzi

URITHI WA MBORA WA MITUME

URITHI WA MBORA WA MITUME URITHI WA MBORA WA MITUME AKILI NA UKAMILIFU WA MWANADAMU MUHTASARI Mtume (s.a.w.w.) ni mfano hai wa ukamilifu wa mwanadamu. Pia urithi wake ndio wenye thamani baada ya Qur’ani. Hakika yeye alikunywa toka chemchemu ya ufunuo mpaka akabubujisha ukamili- fu wake kwa wanadamu kwa kiwango kinachotosheleza kuwapeleka wanadamu mbele upande wa ukamilifu na kuwafikisha kileleni mwa ukamilifu. Tumechagua mifano ya ufasaha wake na semi zake fasihi kuhusu akili, elimu na njia ya kufikia wema na ukamilifu. Tumechagua kwa kiwango ambacho kitawaangazia wenye kufuata njia yake, hivyo wale watafuta ukweli hawatojizuia kutumia madhumuni ya semi hizo.

Ufafanuzi

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 3

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 3 TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 3 UKARIMU MUHTASARI Hakika Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mkarimu sana, hivyo alikuwa akieneza upendo, ukarimu, wema na mali kwa watu wote, huku akitoa msamaha, huruma na ulaini kwao. Ili awaokoe toka kwenye ujinga wao na apate kuwaunganisha pamoja wawe kitu kimoja. Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anaishi na waislam kama mmoja wao huku haya zikimtukuza kwa kumpa haiba na heshima, huku unyenyekevu ukimzidishia heshima na utukufu. Hivyo alikuwa akiwahurumia wadogo na kuwaheshimu wakubwa. Alikuwa akisikia ushauri wa mnasihi ilihali yeye ni mwenye akili zitokazo mbinguni kwa njia ya ufunuo.

Ufafanuzi

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 2

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 2 TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 2 MSOMI ASIYEWAHI KUSOMA WALA KUANDIKA Muhtasari Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad bin Abdullah hakujifunza mikononi mwa mwanadamu yeyote, lakini alikuja na Kitabu cha kie- limu na kimaarifa cha kimataifa ambacho kimewataka wanadamu wote katika zama zote walete mfano wake. Kupitia Kitabu hicho Mtume (s.a.w.w.) aliweza kumtoa mwanadamu toka jamii ya kijinga mpaka jamii ya kielimu iliyokamilika yenye kustaarabika, huku akihimiza usiku na mchana juu ya utafutaji wa elimu na maarifa mbalimbali. Hivyo kupitia Kitabu hicho aliasisi dola kubwa na kujenga ustaarabu wa pekee ambao mfano wake hau- jashuhudiwa na mwanadamu. Mtume (s.a.w.w.) alibeba maana kamili ya ibada kwa Mwenyezi Mungu Muumba, hivyo alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Mola Wake Mtukufu, mahusiano ambayo yalitokana na ujuzi, mapenzi, utashi, na moyo mkunjufu, hivyo akawa ni kiigizo chema katika swala yake, funga, dua na uombaji msamaha, kiigizo ambacho kinamchorea mwanadamu njia ya ukamilifu kuelekea kwa Muumba, Mjuzi. Mtume (s.a.w.w.) alianza harakati akiwa amebeba jukumu kubwa huku akimtegemea Mwenyezi Mungu katika kila harakati na kila jambo, hivyo akawa ni shujaa, jasiri na mkakamavu katika kulingania njia ya Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.w.) aliishi mbali na ladha za dunia na starehe zake, hivyo alikuwa ni sehemu ya mafakiri na masikini, akishirikiana nao katika taabu zao huku akitarajia rehema za Mola Wake, mnyenyekevu Kwake, mwenye kujitenga na kila ujeuri utokanao na starehe za dunia na furaha za mapambo yake.

Ufafanuzi

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 1

TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 1 TABIA NA MWONEKANO WA HITIMISHO LA MANABII 1 MUHTASARI Mwenyezi Mungu katoa wasifu wa Mtume Wake Muhammad (s.a.w.w.) kwa kueleza sifa zake za ukamilifu wa kibinadamu, hivyo akamfanya mbora wa mitume, hitimisho lao, na kigezo chema amba- cho watakiiga wanadamu ili wanadamu hao wafikie kilele cha ukamilifu. Mwenyezi Mungu kawafafanulia waigaji sifa zake na maadili yake mazuri mema. Kizazi chake ambacho ndio kijuacho zaidi yale yaliyomo nyumbani kimetoa wasifu wa mbora wao na mjumbe mwaminifu kupitia maneno yaliyo timilifu yaliyokusanya sifa zote. Huku maneno hayo yakitoa taswira ya ukamilifu na sifa ambazo zimemfanya awe ni kiigizo chema kwa wanaomfuata na bendera kwa wenye kuongoka. Maelezo hayo yaliyonukuliwa kutoka kwa kizazi chake yametoa taswira ya adabu ya hali ya juu ya Mtume (s.a.w.w.) na sera yake binafsi na ya kijamii ya hali ya juu.

Ufafanuzi

MAISHA YA NABII WA MWISHO

MAISHA YA NABII WA MWISHO MAISHA YA NABII WA MWISHO MUHTSARI Ni maarufu kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alizaliwa yatima. Na mama yake Amina binti Wahabi aliona baadhi ya alama zilizojulisha kuwa mwanae atakuwa na jambo kubwa na cheo cha juu. Hakukuwa na kalenda maarufu ya kuhifadhi kumbukumbu za matukio, hivyo historia ya kuzaliwa Mtume (s.a.w.w.) imehifadhiwa na tukio la kuhujumiwa kwa Kaaba, tukio ambalo hujulikana kwa jina la tukio la tembo. Qur’ani imeashiria tukio hili la kihistoria ndani ya Sura Al-Fiylu. Ukoo wa Abdul Muttalib ulimjali sana Muhammad bin Abdullah (s.a.w.w.). Hilo lilidhihirika pale walipompeleka kunyonya kwa Bani Saad kwani baada ya maziwa ya mama yake walimpeleka kijijini ili akanyonye katika mazingira ya afya na ufasaha wa lugha. Mtume ana majina mazuri, sifa nzuri na majina mazuri ya heshima. Maisha ya Mtume (s.a.w.w.) yalichukua miaka sitini na tatu huku yakigawanyika vipindi viwili vikuu: Cha kwanza: Kuanzia alipozaliwa mpaka alipokabidhiwa unabii. Muda wake ni miaka arubaini. Cha pili: Kuanzia alipokabidhiwa unabii mpaka alipofariki. Muda wake ni miaka ishirini na tatu.

Ufafanuzi

MCHANGO WA MAZINGIRA SAFI KATIKA MALEZI

MCHANGO WA MAZINGIRA SAFI KATIKA MALEZI MCHANGO WA MAZINGIRA SAFI KATIKA MALEZI MUHTASARI Hakika Mwenyezi Mungu aliweka umuhimu maalumu kwa manabii wake, hivyo akawezesha wazaliwe toka ndani ya familia takasifu ili wawe na uwezo wa kuwasafisha watu dhidi ya shirki. Hivyo ndivyo alivyomteua nabii Muhammad (s.a.w.w.). Hakika alihama toka mifupa ya migongo mitakasifu yenye imani na toka mapaja ya utawa mpaka dunia ilipopata sharafu kwa kuzaliwa kwake. Familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ilikuwa ni familia na damu yenye kuheshimika, kwani yeye ametokana na nabii Ibrahim (a.s.). Pia ilikuwa ikijihusisha na kulinda Haram ya Makka na kuitetea dhidi ya maadui. Babu wa Mtume Abdul Muttalib aliishi zama ambazo ujumbe wa Mwenyezi Mungu ulikuwa umetoweka huku nguvu za shirki zikiwa zimedhihiri na ufisadi na dhuluma vikishamiri, lakini pamoja na hayo yote alikuwa ni mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu huku akilingania maadili mema, na njia hiyo ndiyo waliyopita watoto wake. Abdul Muttalib alimjali sana mwanae Abdullah, hivyo akamwozesha mwanamke bora toka familia na damu yenye heshima. Lakini matak- wa ya Mwenyezi Mungu yalitaka Abdullah afariki kabla ya kuzaliwa mwanae Muhammad (s.a.w.w.).

Ufafanuzi

MUHAMMAD BIN ABDULLAH (S.A.W.W.) NI UTABIRI WA MANABII (A.S.)

MUHAMMAD BIN ABDULLAH (S.A.W.W.) NI UTABIRI WA MANABII (A.S.) MUHAMMAD BIN ABDULLAH (S.A.W.W.) NI UTABIRI WA MANABII (A.S.) MUHTASARI Matukio ya kihistoria yanaonyesha kuwa mwenendo wa manabii ni wa kiukamilifu wenye lengo moja na njia moja. Pia mwenendo wa Mwenyezi Mungu ni manabii waliyopo kuwabashiri watakaochukua nafasi zao katika unabii. Ikiwa ni huruma toka kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya mzigo walio nao wanadamu katika kuamini na kukubali na ni kumrahisishia nabii anayefuata kazi ya uhubiri na ulinganio. Na kwa kuwa Uislamu na Mtume Muhammad vina umuhimu mkub- wa katika historia ya binadamu, na ukizingatia kuwa Uislamu ni dini inayohusu kila kitu na ndiyo dini ya mwisho huku Mtume (s.a.w.w.) akiwa ndiyo mtume wa mwisho, basi Uislamu huo ulibashiriwa tangu zamani na hilo limeelezwa na Qur’ani tukufu. Kuna habari zilizoenea kabla ya Mtume kukabidhiwa utume ambazo zilikuwa zimebeba wasifu kamili wa Mtume Muhammadin (s.a.w.w.) na mazingira yake, zikiwataka watu wamwamini na wajiepushe na upotovu kwa kumfuata yeye. Habari hizi zilisaidia baadhi ya Ahlul-Kitabu na wengineo kuamini dini ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) bila ya kuomba muujiza wowote mahsusi.

Ufafanuzi

HATUA YA MWANZO KUELEKEA KWENYE MASOMO YA SERA NA HISTORIA YA UISLAMU

HATUA YA MWANZO KUELEKEA KWENYE MASOMO YA SERA NA HISTORIA YA UISLAMU MUHTASARI Sera ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na sera ya kizazi chake kitakasifu ni chanzo muhimu kati ya vyanzo vya maarifa na sheria ya kiislamu. Huzingatiwa pia kuwa ni nyenzo kati ya nyenzo za kufikia wema na mafanikio, kwa sababu kuwafuata wao ni mfano halisi wa kufuata njia ya Mwenyezi Mungu iliyonyooka. Historia ya kiislamu ndio historia ya Uislamu na ndio historia ya watetezi ambao walizama ndani na kujitoa muhanga kila dakika ya maisha yao katika njia ya Uislamu. Nao ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake kitakasifu kilichotakasika dhidi ya kila aina ya uchafu na kila aina ya dosari. Qur’ani ndio chanzo muhimu cha historia na sera ya Mtume (s.a.w.w.) na historia ya kiislamu. Kwa ajili hiyo vyanzo vyote vingine vya sera na historia vinapimwa kwa Qur’ani, kwa sababu vyanzo vingine vimekosa sifa ya “kumdiriki Mtume (s.a.w.w.)”, “kudiriki yote, umakini, na kutoegemea” kwenye maslahi ya makundi na madhehebu ambayo yalizuka baada ya zama za Mtume (s.a.w.w.). Zama za Mtume wa mwisho (s.a.w.w.) huchukuliwa kama mwanzo wa zama za historia ya kiislamu kisha hufuatiwa na zama za Maimam wema (a.s.).

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini