Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Makala

MAKALA MBALIMBALI
MCHANGO WA HIJA KATIKA SUALA LA UMOJA

MCHANGO WA HIJA KATIKA SUALA LA UMOJA

MCHANGO WA HIJA KATIKA SUALA LA UMOJA Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa moja ya haja za dharura za kipindi cha sasa ni kutilia maanani umoja na mshikamano wa Kiislamu. Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo katika hadhara ya wafanyakazi wa sekta ya utamaduni na wasimamizi wa misafara ya hija ya mwaka huu ya Iran. Amesisitiza kuwa ibada ya hija inapaswa kuwa dhihirisho la azma kubwa ya umma wa Kiislamu mkabala wa hatua zozote za kuzusha mfarakano na zinazopinga umoja na maendeleo ya dunia ya Kiislamu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa hija ni fursa adhimu na yenye thamani kubwa na akaongeza kuwa fursa ya kuwa kando ya msikiti mtakatifu wa Makka, msikiti wa Mtume, haram za Maimamu watoharifu na masahaba wa Mtume inapaswa kutumiwa kwa ajili ya kuzidisha rasilimali ya imani, masuala ya kiroho na unyenyekevu mbele ya Mola Mlezi. Amesema kuwa mahujaji wanapaswa kuwa macho ili fursa hiyo ya thamani isitumike katika kazi zisizokuwa na thamani za kidunia.

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)
KUZALIWA KWA MTUME (S.A.W.W)

KUZALIWA KWA MTUME (S.A.W.W)

KUZALIWA KWA MTUME (S.A.W.W) Kuzaliwa kwa Nabii Muhammad kuliandamana na miujiza mingi ikiwemo ya kusambaratika kwa nguzo za dhulma na kuzimika moto wa Fars. Nabii Muhammad ambaye jina lake lina maana ya aliyesifiwa, ni mtume wa mwisho kati ya mitume wote waliotumwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumuongoza mwanadamu katika njia nyoofu kuelekea ufanisi na saada ya milele. Tunawapongeza wapenda haki na Waislamu wote duniani dunia kwa mnasaba huu adhimu wa kuzaliwa Mtume Mhammad (SAW) pamoja na mjukuu wake Imam Swadiq (AS). Kuzaliwa kwa Nabii Muhammad kuliandamana na miujiza mingi ikiwemo ya kusambaratika kwa nguzo za dhulma na kuzimika moto wa Fars. Nabii Muhammad ambaye jina lake lina maana ya aliyesifiwa, ni mtume wa mwisho kati ya mitume wote waliotumwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumuongoza mwanadamu katika njia nyoofu kuelekea ufanisi na saada ya milele. Huyu ni Mtume ambaye alikuwa na siri zote za kuumbwa dunia kwenye kifua chake na kuziongoza nyoyo zilizojaa chuki kwenye njia ya haki na ukweli. Mwenyezi Mungu anasema hivi kuhusiana na Mtukufu huyo: "Amekufikieni Mtume aliye jinsi moja na nyiye, yanamhuzunisha yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni. (Na) kwa walioamini ni mpole na mrehemevu (kabisa) (Tauba 9-128)." Pia amesema: "(Alikuwa) mwenye kuzishukuru neema Zake (Mwenyezi Mungu zilizo juu yake), aka chagua na kumwongoza kwenye njia iliyonyooka (16-121)."

MAKALA MBALIMBALI
ATHARI YA UISLAMU NDANI YA UINGEREZA

ATHARI YA UISLAMU NDANI YA UINGEREZA

ATHARI YA UISLAMU NDANI YA UINGEREZA Waziri wa Sheria wa Uingereza amesema kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamekuwa na athari kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba athari hizo pia zinaonekana miongoni mwa Waislamu wa Uingereza. Akizungumza katika mazungumzo ya meza duara yaliyokuwa yakijadili mchango wa Waislamu katika jamii ya Uingereza, Jack Straw amesema kuwa athari za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwishoni mwa muongo wa sabini zilihisika pia nchini Uingereza ambapo Waislamu wa nchi hiyo pia walijihisi kuwa na nguvu. Katika sehemu nyingine, Straw amesema kuwa Waislamu, Wakristo na Mayahudi wanapasa kuimarisha uhusiano wao na kwamba serikali ya London inapasa kusisitiza umuhimu wa suala hilo kupitia vyombo vya habari. Hata hivyo Straw amedai kwamba Uislamu umekuwa ukitumiwa vibaya na baadhi ya makundi ya kisiasa katika miongo ya hivi karibuni.

MAKALA MBALIMBALI
SHEREHE ZA KRISMAS

SHEREHE ZA KRISMAS

SHEREHE ZA KRISMAS Katika moja ya hotuba zake za swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Omar bin Khattab huko Doha nchini Qatar, Sheikh Yusuf Qardhawi amezungumzia masuala matatu muhimu yanayowahusu Waislamu. Ameanza kwa kuzungumzia kuenea kwa madhihirisho ya sherehe za Kikristo za Krismasi nchini Qatar na kukosoa vikali tabia ya Waislamu ya kujishughulisha na sherehe hizo zisizoambatana na utamaduni wa Kiislamu. Sheikh huyo amesikitishwa mno na tabia hiyo na kuuliza maswali mengi kwa kusema; Je, sisi tunaishi katika jamii ya Kiislamu au Kikristo? Ni sherehe gani hizi zinazofanyika katika mitaa na maduka kwa jina la sikukuu ya Kikristo au Krismasi, ni kana kwamba sisi tunaishi katika mojawapo ya nchi za Ulaya zinazofuata mafundisho ya Kikristo? Huku akiashiria kumalizika hivi karibuni tu kwa idi kubwa ya Waislamu ya Adh'ha, na kutofanyika sherehe kubwa kama hizo zinazoonekana hivi sasa za Krismasi nchini Qatar, Sheikh Yusuf Qardhawi ameashiria kuwepo hitilafu kubwa miongoni mwa Wakristo wenyewe kuhusiana na iwapo kweli Nabii Isah (as) au kwa jina jingine, Yesu, alizaliwa tarehe 25 Disemba au tarehe 7 Januari. Alisema hitilafu hizo pia zinahusiana na iwapo Yesu alizaliwa katika msimu wa joto au wa baridi. Hata hivyo ameashiria aya ya Qur'ani Tukufu kuhusiana na uzawa wa Isah Masih (as) na kusema kuwa kwa mujibu wa aya hiyo, mtukufu huyo alizaliwa katika msimu wa joto ambapo tende zilikuwa zikivunwa.

Imam Husein (A.S)
NAFASI YA IMAMU HUSEIN

NAFASI YA IMAMU HUSEIN

NAFASI YA IMAMU HUSEIN Kila mwaka unapowadia mwezi wa Muharram nyoyo za wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume wetu Muhammad saw na Ahlubaiti zake zinashikwa na hali ya huzuni na majonzi makubwa. Siku hizi zinakwenda sambamba na harakati na vikao vya kuhuisha mapambano makubwa ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein bin Ali (as) katika ardhi ya Karbala. Kwa mnasaba huo pia tunatuma sala na salamu zetu kwa mkombozi mkubwa wa mwanadamu Nabii Muhammad amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, Ali zake na Ahlubaiti wake waliotakaswa na dhambi na mambo machafu. Sala za salamu za Mwenyezi Mungu zikufikie wewe Abu Abdillah Hussein bin Ali na roho zilizouawa shahidi katika kupigania haki na dini ya Allah. Salamu zaAllah ziwafikie usiku na mchana hadi siku ya kufufuliwa viumbe kwa ajili ya hesabu. Risala na ujumbe mkubwa wa Manabii na mawalii wote wa Mwenyezi Mungu ilikuwa ni kupambana na dhulma na uonevu na kusimamisha haki na uadilifu. Mitume na mawalii wote walikuwa na jukumu la kusimamisha dini ya haki, uhuru na kumuonesha mwanadamu njia ya saada na uongofu.

MAKALA MBALIMBALI
KUYAHUDISHWA KWA AQSA

KUYAHUDISHWA KWA AQSA

KUYAHUDISHWA KWA AQSA Viongozi wa Palestina wametahadharisha juu ya njama zinazofanywa na Wazayuni za kubomoa na kuharibu nyumba za Wapalestina katika mji unaoukaliwa kwa mabavu wa Quds kwa ajili ya kuufanya mji huo kuwa wa Kiyahudi. Kwa mujibu wa ripoti ya televisheni ya al-Alaam viongozi wa Palestina wanasema kuwa kitendo hicho ni sawa na kutangazwa vita, mauaji ya kizazi na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina. Wanasisitiza kwamba, siasa hizo za Wazayuni zinahatarisha kizazi kizima cha Wapalestina katika mji huo mtakatifu. Kuhusiana na suala hilo, Maad az-Zatari, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya al-Maqdis ameiambia televisheni ya al-Alaam kwamba, utawala wa Israel unatekeleza siasa za kubomoa na kuharibu nyumba za Wapalestina wanaoishi katika mji wa Quds ili kuwalazimisha kuondoka katika mji huo na hivyo kutoa fursa ya kufanywa kuwa wa Kiyahudi.

MAKALA MBALIMBALI
UCHOCHEZI NA FITINA

UCHOCHEZI NA FITINA

UCHOCHEZI NA FITINA Licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufanya juhudi za pande zote na pia wasomi na wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu kuchukua hatua muhimu za kuleta umoja miongoni mwa Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia, kwa bahati mbaya bado inasikika sauti ya fitina na mifarakano kutoka kwa baadhi ya watu na nchi zisizopenda kuona umoja na utulivu ukidumishwa katika umma wa Kiislamu. Bila shaka sauti hii haitakuwa na manufaa ila kwa maadui wa Uislamu. Ni wazi kuwa sauti hii ni hatari kubwa inayopasa kuleta muamko miongoni mwa Waislamu na kuwafanya waepuke kutumbukia kwenye shimo la fitina na mifarakano. Je, ni kwa hoja gani juhudi za miaka mingi za kuleta umoja na mshikamano kati ya Waislamu, zilizofanywa na wasomi pamoja na wanafikra wakubwa wa Kiislamu wakiwemo Sayyid Jamal, Sheikh Shaltut na Imam Khomeini zimechukuliwa kuwa mchezo na baadhi ya watu ambao wanajichukulia kuwa ndio walio kwenye njia ya haki na kuwatuhumu waumini kwa mambo yasiyo na msingi, bila ya kuwa na hoja yoyote ya maana? Ni wazi kuwa Mawahabi wa Saudi Arabia wameazimia kuwahudumia kwa nguvu zao zote maadui wa umoja wa Uislamu, na hakuna njia nyingine yoyote ya kufikia lengo hilo isipokuwa kuchochea fitina na mifarakano katika jamii ya Kiislamu.

MAKALA MBALIMBALI
WAISLAMU NA UMOJA WAO

WAISLAMU NA UMOJA WAO

WAISLAMU NA UMOJA WAO Kikao cha 23 cha kimataifa cha Umoja wa Kiislamu ambacho kinawashirikisha wasomi, wanafikra na wanazuoni wa Kiislamu wapatao 500 kutoka pembe mbalimbali za dunia kilicho anza Machi Pili mjini Tehran Iran na kuendelea hadi Alkhamisi Machi Nne, ikiwa ni katika siku za kuadhimisha Wiki ya Umoja wa Kiislamu. Kikao hicho kilifunguliwa rasmi kwa hotuba ya Ayatullah Hashimi Rafsanjani, Mkuu wa Majlisi ya Kumchagua Kiongozi Mkuu wa mfumo wa Kiislamu wa Iran ambaye pia ni Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu nchini Iran. Kikao hicho cha siku tatu ambacho kinawajumuisha wanafikra na wasomi wa Kiislamu kutoka humu nchini na pembe nyinginezo za dunia kitajadili masuala na changamoto mbalimbali zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu na hasa kuhusiana na suala la kuimarisha umoja na mshikamano kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu chini ya anwani isemayo: "Umma wa Kiislamu, Tokea Madhehebu Tofauti hadi Mielekeo ya Kimakundi."

Imam Ali (a.s)
GHADIR KHUM

GHADIR KHUM

GHADIR KHUM Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alipo kutana na maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali waliokwenda kuonana naye kwa mnasaba wa sikukuu ya Ghadiri Khum (siku Imam Ali bin Abi Twalib alipotawazwa rasmi na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa Imam na kiongozi wa umma wa Kiislamu baadaye yake) alisema kuwa suala la Ghadir ni kigezo cha milele cha Mwenyezi Mungu kinachoainisha njia sahihi ya umma wa Kiislamu. Ayatullah Khamenei aliashiria urongo mkubwa unaoenezwa na Wazayuni na nchi za kigeni kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran kwa shabaha ya kupotosha fikra za walimwengu na akasema kuwa urongo huo utawafedhehesha zaidi maadui wa taifa la Iran baada ya kudhihiri ukweli wa mambo. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amewapongeza wananchi wa Iran na Waislamu wote ulimwenguni kwa mnasaba wa sikukuu ya Ghadir. Akifafanua sababu ya sikukuu hiyo kuitwa sikukuu kubwa zaidi ya Mwenyezi Mungu (Idullahil Akbar), Ayatullah Khamenei amesema, tukio la Ghadiri Khum lilikuwa na maana kubwa zaidi kuliko idi na sikukuu nyingine za Kiislamu, kwani kwa mujibu wa vigezo vya Mwenyezi Mungu, wajibu wa Waislamu kuhusu uongozi na serikali uliainishwa katika siku hiyo.

Imam Jawad (a.s)
TAALUMA NA MAFUNZO YA AMALI

TAALUMA NA MAFUNZO YA AMALI

TAALUMA NA MAFUNZO YA AMALI Tuko katika siku za mwisho za mwezi wa Dhul Qaada, ambazo ni siku za kuuawa shahidi mmoja wa Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw). Katika siku kama hizi mwaka 220 Hijiria, Imam Jawad (as), kiongozi mkubwa na mtukufu wa Kiislamu, aliaga dunia na hivyo kuuachia ulimwengu wa Kiislamu huzuni kubwa. Watu wa Nyumba ya Mtume katika utekelezaji wa majukumu yao makubwa waliyopewa na Mwenyezi Mungu, walikuwa waanzilishi wa matukio makubwa ya kifikra, kiutamaduni na kijamii katika ulimwengu wa Kiislamu. Iwapo tutatalii vyema historia na maisha ya Ahlul Beit (as), tunaona kuwa walikuwa na nafasi muhimu katika kulinda misingi na nguzo za dini. Walisimama na kupambana vikali na madhihirisho ya dhulma, upotovu na ufisadi na kufanya jitihada kubwa za kulinda misingi ya Uislamu halisi ili dini hii tukufu idumu milele. Imam Jawad (as) ni miongoni mwa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) ambaye katika kipindi cha miaka 17 ya uimamu wake, daima alikuwa akifanya jitihada za kueneza Uislamu na kuimarisha mafundisho yake tajiri ulimwenguni. Huku tukitoa mkono wa pole kwa Waislamu wote wapenda haki kwa mnasaba wa kuwadia siku ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Jawad (as), tunazungumzia hapa angaa kwa ufupi, maisha ya mtukufu huyo.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini