Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Makala

MAKALA MBALIMBALI
UCHOCHEZI NA FITINA

UCHOCHEZI NA FITINA

UCHOCHEZI NA FITINA Licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufanya juhudi za pande zote na pia wasomi na wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu kuchukua hatua muhimu za kuleta umoja miongoni mwa Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia, kwa bahati mbaya bado inasikika sauti ya fitina na mifarakano kutoka kwa baadhi ya watu na nchi zisizopenda kuona umoja na utulivu ukidumishwa katika umma wa Kiislamu. Bila shaka sauti hii haitakuwa na manufaa ila kwa maadui wa Uislamu. Ni wazi kuwa sauti hii ni hatari kubwa inayopasa kuleta muamko miongoni mwa Waislamu na kuwafanya waepuke kutumbukia kwenye shimo la fitina na mifarakano. Je, ni kwa hoja gani juhudi za miaka mingi za kuleta umoja na mshikamano kati ya Waislamu, zilizofanywa na wasomi pamoja na wanafikra wakubwa wa Kiislamu wakiwemo Sayyid Jamal, Sheikh Shaltut na Imam Khomeini zimechukuliwa kuwa mchezo na baadhi ya watu ambao wanajichukulia kuwa ndio walio kwenye njia ya haki na kuwatuhumu waumini kwa mambo yasiyo na msingi, bila ya kuwa na hoja yoyote ya maana? Ni wazi kuwa Mawahabi wa Saudi Arabia wameazimia kuwahudumia kwa nguvu zao zote maadui wa umoja wa Uislamu, na hakuna njia nyingine yoyote ya kufikia lengo hilo isipokuwa kuchochea fitina na mifarakano katika jamii ya Kiislamu.

MAKALA MBALIMBALI
WAISLAMU NA UMOJA WAO

WAISLAMU NA UMOJA WAO

WAISLAMU NA UMOJA WAO Kikao cha 23 cha kimataifa cha Umoja wa Kiislamu ambacho kinawashirikisha wasomi, wanafikra na wanazuoni wa Kiislamu wapatao 500 kutoka pembe mbalimbali za dunia kilicho anza Machi Pili mjini Tehran Iran na kuendelea hadi Alkhamisi Machi Nne, ikiwa ni katika siku za kuadhimisha Wiki ya Umoja wa Kiislamu. Kikao hicho kilifunguliwa rasmi kwa hotuba ya Ayatullah Hashimi Rafsanjani, Mkuu wa Majlisi ya Kumchagua Kiongozi Mkuu wa mfumo wa Kiislamu wa Iran ambaye pia ni Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu nchini Iran. Kikao hicho cha siku tatu ambacho kinawajumuisha wanafikra na wasomi wa Kiislamu kutoka humu nchini na pembe nyinginezo za dunia kitajadili masuala na changamoto mbalimbali zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu na hasa kuhusiana na suala la kuimarisha umoja na mshikamano kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu chini ya anwani isemayo: "Umma wa Kiislamu, Tokea Madhehebu Tofauti hadi Mielekeo ya Kimakundi."

Imam Ali (a.s)
GHADIR KHUM

GHADIR KHUM

GHADIR KHUM Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alipo kutana na maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali waliokwenda kuonana naye kwa mnasaba wa sikukuu ya Ghadiri Khum (siku Imam Ali bin Abi Twalib alipotawazwa rasmi na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa Imam na kiongozi wa umma wa Kiislamu baadaye yake) alisema kuwa suala la Ghadir ni kigezo cha milele cha Mwenyezi Mungu kinachoainisha njia sahihi ya umma wa Kiislamu. Ayatullah Khamenei aliashiria urongo mkubwa unaoenezwa na Wazayuni na nchi za kigeni kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran kwa shabaha ya kupotosha fikra za walimwengu na akasema kuwa urongo huo utawafedhehesha zaidi maadui wa taifa la Iran baada ya kudhihiri ukweli wa mambo. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amewapongeza wananchi wa Iran na Waislamu wote ulimwenguni kwa mnasaba wa sikukuu ya Ghadir. Akifafanua sababu ya sikukuu hiyo kuitwa sikukuu kubwa zaidi ya Mwenyezi Mungu (Idullahil Akbar), Ayatullah Khamenei amesema, tukio la Ghadiri Khum lilikuwa na maana kubwa zaidi kuliko idi na sikukuu nyingine za Kiislamu, kwani kwa mujibu wa vigezo vya Mwenyezi Mungu, wajibu wa Waislamu kuhusu uongozi na serikali uliainishwa katika siku hiyo.

Imam Jawad (a.s)
TAALUMA NA MAFUNZO YA AMALI

TAALUMA NA MAFUNZO YA AMALI

TAALUMA NA MAFUNZO YA AMALI Tuko katika siku za mwisho za mwezi wa Dhul Qaada, ambazo ni siku za kuuawa shahidi mmoja wa Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw). Katika siku kama hizi mwaka 220 Hijiria, Imam Jawad (as), kiongozi mkubwa na mtukufu wa Kiislamu, aliaga dunia na hivyo kuuachia ulimwengu wa Kiislamu huzuni kubwa. Watu wa Nyumba ya Mtume katika utekelezaji wa majukumu yao makubwa waliyopewa na Mwenyezi Mungu, walikuwa waanzilishi wa matukio makubwa ya kifikra, kiutamaduni na kijamii katika ulimwengu wa Kiislamu. Iwapo tutatalii vyema historia na maisha ya Ahlul Beit (as), tunaona kuwa walikuwa na nafasi muhimu katika kulinda misingi na nguzo za dini. Walisimama na kupambana vikali na madhihirisho ya dhulma, upotovu na ufisadi na kufanya jitihada kubwa za kulinda misingi ya Uislamu halisi ili dini hii tukufu idumu milele. Imam Jawad (as) ni miongoni mwa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) ambaye katika kipindi cha miaka 17 ya uimamu wake, daima alikuwa akifanya jitihada za kueneza Uislamu na kuimarisha mafundisho yake tajiri ulimwenguni. Huku tukitoa mkono wa pole kwa Waislamu wote wapenda haki kwa mnasaba wa kuwadia siku ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Jawad (as), tunazungumzia hapa angaa kwa ufupi, maisha ya mtukufu huyo.

utafiti mbali mbali
VIZUIZI VYA UMOJA

VIZUIZI VYA UMOJA

VIZUIZI VYA UMOJA Ulimwengu wa Kiislamu umekuwa ukikabiliwa na matatizo mbalimbali katika juhudi zake za kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu. Matatizo hayo yamekuwa yakitoka nje na ndani ya ulimwengu wa Kiislamu wenyewe. Waislamu wenyewe ndio wamekuwa wakijisababishia matatizo ya ndani, matatizo ambayo yanatokana na fikra finyu na za upande mmoja. Fikra hizo finyu kwa hakika zimekuwa zikisababisha harakati na matokeo hatari kwa ulimwengu wa Kiislamu. Vizuizi vya nje vimekuwa vikitokana na ujanja, hila na njama za dhahiri na siri za madola makubwa ya kikoloni ambayo yanautazama umoja wa Waislamu kama hatari kubwa kwao na hivyo kutoustahimili kabisa. Kwa kuzusha mifarakano, ugomvi na fitina miongoni mwa Waislamu, madola hayo yamekuwa yakijaribu kila njia iwezekanayo kuzuia kupatikana umoja wa kutegemewa miongoni mwa Waislamu, umoja ambao unaweza kuwapelekea kuunda harakati moja yenye nguvu duniani. Ni wazi kuwa mambo na vizuizi vinavyozuia kupatika umoja na nguvu katika ulimwengu wa Kiislamu ni hatari kubwa kwa Waislamu kwa sababu jambo hilo linazuia kabisa kupatikana njia za kielimu za kukabiliana na suala hilo. Pia ni wazi kuwa kughafilika na juhudi za kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu ni jambo linalopasa kuepukwa kwa kila njia. Pamoja na hayo tunapolinganisha madhara ya vizuizi vya ndani na nje katika kuzuia umoja wa Kiislamu tunaona kwamba vizuizi vya ndani ndivyo vilivyo na madhara makubwa zaidi kwa umoja huo.

Imam Sajjaad (a.s)
DUA YA IMAM ZAYNUL ABIDIN

DUA YA IMAM ZAYNUL ABIDIN

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM DUA YA IMAM ZAYNUL ABIDIN (a.s.) KATIKA KUOMBA TAWBA Ewe Mola wangu, ambaye sifa za kukusifu za wenye kukusifu haziwezi kutajika. Ewe mwenye mategemeo ambaye mategemeo hayawezi kwenda zaidi yako.Ewe ambaye kwako wewe malipo ya waja wako hayatapotea. Ewe unayeogopwa na waja wako. Ewe uliye khofu ya mja wako na hii ndiyo nafasi imemkuba ghafla kwa madhambi. Ambaye amevutwa na zama za makosa na ambayo yameghalibiwa na sheitani. Kwa hivyo ameshindwa kabisa kutimiza yale uliyokuwa umemwamrisha kuyafanya na yeye hakuyafanya. Yeye amegang'ania tu katika yale uliyokuwa umeyaharamisha na kuyakataza kama kwamba haelewi uwezo ulionao juu yake. Au kama yule anayekanusha ukarimu wako mtukufu kwake yeye hadi macho ya hidaya kufunguliwa kwa ajili yake na mawingu (kiza) cha upofu (wa hidaya) ulipoondolewa kutoka kwake, na alipotambua kwa ukamilifu vile alivyojidhulumu nafsi yake na kuyazingatia kuwa amemwasi Muumba wake.

MAKALA MBALIMBALI
SABABU YA KUCHUKIWA UISLAMU NI UJAHILI

SABABU YA KUCHUKIWA UISLAMU NI UJAHILI

SABABU YA KUCHUKIWA UISLAMU NI UJAHILI Rita De Milo, mhadhiri wa masuala ya utafiti wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Rome, mji mkuu wa Italia amesema kuwa ujahili wa wasiokuwa Waislamu na raia wengi wa nchi za Magharibi kuhusiana na Uislamu ni sababu kuu ya kuenea chuki yao dhidi ya Uislamu na hivyo kuwapelekea kuiogopa dini hii. Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharqul Ausat, Rida De Milo amesema kuwa Uislamu umebainisha vyema na kwa kina masuala mbalimbali yanayomuhusu mwanadamu, likiwemo suala la haki za binadamu na hasa haki za mwanamke. Amesisitiza kuwa hakuna taasisi wala dini nyingine ilivyobainisha vyema na kutetea haki za mwanamke kama ulivyofanya Uislamu. Amesema sheria za Kiislamu ni nguzo muhimu inayopasa kupewa umuhimu mkubwa katika sheria za kimataifa kwa kutilia maananni kwamba zinabainisha vyema umuhimu wa kulindwa haki za binadamu bila ya kujali dini, rangi, ukabila wala utaifa wao. De Milo ameendelea kusema kuwa kuenea kwa dini tukufu ya Kiislamu katika nchi za Magharibi ni dalili ya wazi kuwa mafundisho ya dini hii yanawahusu wanadamu wote. Amesema kuwa hata kama kuna hujuma ya makusudi inayoenezwa na makundi fulani dhidi ya dini hii lakini ni wazi kuwa hujuma hiyo haitadumu kwa muda mrefu kwa sababu Waislamu nao wameanzisha mbinu za kujitetea na kulinda thamani za dini yao dhidi ya hujuma hiyo.

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)
SERIKALI YA MTUE (S.A.W.W)

SERIKALI YA MTUE (S.A.W.W)

SERIKALI YA MTUE (S.A.W.W) Ushahidi na nyaraka za historia za kabla ya kudhihiri Uislamu zinaonyesha kuwa hakukuwepo utawala na serikali katika ardhi ya Hijaz na kwamba maisha ya Waarabu wa jangwani hayakutawaliwa na mfumo makhsusi wa kisiasa. Ni baada ya kudhihiri dini ya Uislamu huko Makka na kuhamia Mtume Muhammad katika mji wa Madina ndipo mtukufu huyo alipoanzisha serikali kuu na kubadili mfumo wa kikabila uliokuwa ukitawala kwa kuasisi mfumo mpya wa kisiasa na kijamii. Mbali na kutoa mafunzo na malezi kwa jamii ya watu wa Hijaz, Mtume Muhammad (saw) pia aliongoza yeye binafsi jamii changa ya Kiislamu na kushika hatamu za mfumo wa kijamii wa Waislamu katika nyanja mbalimbali za sheria, utamaduni, siasa, masuala ya kijeshi na kiuchumi.(2) Suala hilo linaonekana wazi zaidi katika mtazamo wa aya za Qur'ani na ushahidi wa kihistoria kiasi kwamba hata wataalamu wa masuala ya Mashariki (orientalist) wasiokuwa Waislamu wamelifafanua kwa uwazi zaidi. Msomi wa Kitaliano Fel Lino anasema: Mtume Muhammad (saw) aliasisi dini na dola kwa pamoja na masuala yote hayo mawili yalipanuka na kukuwa sambamba katika kipindi cha uhai wake.

MAKALA MBALIMBALI
MBINU ZA MAADUI KUZUSHA FITINA

MBINU ZA MAADUI KUZUSHA FITINA

MBINU ZA MAADUI KUZUSHA FITINA Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo amehutubia umati mkubwa wa maelfu ya wanafunzi wa vyuo vya kidini, maulamaa, walimu na maimamu wa swala za jamaa wa misikiti ya Tehran kwa mnasaba wa kukaribia mwezi wa Muharram akisema kuwa ulinganiaji sahihi ni kuwazindua wananchi na kuwawezesha kumaizi mambo katika jamii hususan katika kipindi cha fitina. Ayatullah Khamenei ameashiria matukio ya baada ya uchaguzi wa Rais hapa nchini hususan hatua ya hivi karibuni ya maadui wa taifa la Iran ya kumvunjia heshima Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu na akawashukuru wananchi kwa kuwa macho na kujitokeza kwa wingi kupinga kitendo hicho. Vilevile amewataka wananchi wote kuwa watulivu hususan tabala la wanafunzi wa vyuo vikuu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa jengo hili imara ambalo uhandisi wake ni wa Mwenyezi Mungu, umetayarishwa na rijali wa Mwenyezi Mungu na litabakia kwa himaya ya taifa linalomwamini Mwenyezi Mungu, litabakia imara daima na maadui hawatafikia malengo yao. Ayatullah Ali Khamenei ameashiria matukio ya baada ya uchaguzi wa Rais hapa nchini na akasema inasikitisha kwamba baada ya uchaguzi huo baadhi ya watu walivunja sheria na kuanzisha ghasia na kutayarisha uwanja uliowapa matumaini maadui waliokuwa wamekata tamaa kiasi cha kuthubutu kumvunjia heshima Imam Khomeini mbele ya macho ya wanafunzi wa vyuo vikuu wafuasi wa Imam, Mapinduzi na mfumo wa Kiislamu hapa nchini. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa kitendo hicho cha kumuvunjia heshima Imam ni matokeo ya ukiukaji huo wa sheria na kuridhishwa na uungaji mkono wa vyombo vya habari vya wageni, na baada ya makosa hayo kutukia zinafanyika jitihada za kuyaficha kwa kutoa visingizio mbalimbali.

Wanavyuoni wa Kiislamu
HIJA MBELE YA IMAMA KHOMEINY

HIJA MBELE YA IMAMA KHOMEINY

HIJA MBELE YA IMAMA KHOMEINY Ibada ya hija, ni moja ya masuala ya kiibada na kisiasa ambayo yamefaradhihwa katika dini tukufu ya Kiislamu. Ibada hii muhimu hutekelezwa kila mwaka katika ardhi tukufu ya wahyi, na mamilioni ya watu walio na hamu kubwa, kutoka kila pembe ya dunia, watu ambao kwa hakika huwa ni wa mataifa, jamii, rangi na lugha mbalimbali. UMUHIMU WA HIJA NA ATHARI ZAKE Ibada ya hija, ni moja ya masuala ya kiibada na kisiasa ambayo yamefaradhihwa katika dini tukufu ya Kiislamu. Ibada hii muhimu hutekelezwa kila mwaka katika ardhi tukufu ya wahyi, na mamilioni ya watu walio na hamu kubwa, kutoka kila pembe ya dunia, watu ambao kwa hakika huwa ni wa mataifa, jamii, rangi na lugha mbalimbali. Kuna ibada chache kati ya faridha nyingi za Kiislamu iliyopewa uzito na kusisitiziwa Waislamu kama ilivyo hija. Sisitizo la kitabu kitakatifu cha Qur'ani pamoja na nasaha zilizotolewa na viongozi watukufu wa kidini ni nyingi mno na zisizoweza kubainishwa kwa maneno. Abdallah bin Sinaan.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini